Saturday, August 11, 2012

MTAZAMO WANGU KUHUSU SUALA LA GESI YA MNAZIBAY NA KUFADIKA KWA WANANCHI WA MTWARA





 Mtwara ni mji nchini Tanzania ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Mtwara. Kulingana na sensa ya mwaka 2002 idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 92,602 [1] .

Mtwara ni mji wa bandari kando la Bahari Hindi karibu na mpaka wa Tanzania na Msumbiji. Kiutawala Mtwara ni wilaya ya Mtwara mjini umeunganishwa pamoja na mji wa kihistoria wa Mikindani katika halmashauri ya manisipaa ya Mtwara-Mikindani.

Mtwara ni mji mpya ulioanzishwa tangu 1947 mahali ambako palikuwa na kijiji kidogo cha wavuwi tu. Waingereza waliotawala Tanganyika wakati ule walipanga mradi mkubwa wa kilimo katika Tanganyika ya Kusini wakahitaji bandari kwa ajili ya kubeba mazao yake. Mji ulipangwa kitaalamu kwa ajili ya wakazi 200,000 na mahali palichaguliwa kwa sababu ya badari asilia iliyofaa hata kwa meli kubwa.

Bandari ilijengwa na mji mpya ulianzsihwa lakini tangu 1950 ilionekana ya kwamba mradi wa kilimo kilishindikana. 1953 mji ulikuwa na wakazi 36,999 pekee. Mji haukuendelea ukarudi nyuma hasa kwa sababu pwani la Kusini ilikosa barabara na njia za mawasiliano. Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Msumbiji ilizuia biashara ya mpakani.

Tangu miaka ya 1990 uchumi ulianza kusogea mbele polepole. Barabara ya lami inaendelea kutengenezwa kutoka Daressalaam kuelekea Mtwara. Tangu kukamilishwa kwa daraja la mto Rufiji mawasiliano kwa barabara yameboreshwa hata wakati wa mvua. Vilevile feri inayovuka mto Ruvuma imeongeza biashara ya mpakani na Msumbiji.

Kuna pia mipango ya kujenga barabara imara kutoka Mtwara kwenda Songea na Ziwa Nyasa itakayowezesha badari kuhudumia kusini yote ya Tanzania pamoja na Malawi.

Mtwara ni kitovu cha usafiri katika kusini-mashariki ya Tanzania. Mabasi kadhaa hufika kila siku kutoka Daressalaam. Meli hufika mara kwa mara. Uwanja wa ndege hufikiwa na Air Tanzania mara tano kila wiki. Barabara ya lami imefikia Lindi na Masasi. Feri ya mto Rovuma inabeba magari na mizigo karibu kila siku. Daraja kwenda Msumbiji unapangwa.

Kuna pia mipango ya kujenga barabara ya lami kutoka Mtwara kwenda Songea na Ziwa Nyasa itakayowezesha bandari ya mji kuhudumia kusini ya Tanzania pamoja na Malawi.

Moja katia ya sifa za nchi kuwa na maendeleo ni pamoja na wananchi wake kukua kiuchumi zaidi kutokana na raslimali zake zilizopo 

Ukizungumzia Mikoa yenye Raslimali nyingi hapa nchini mkoa wa mtwara hutaacha kuutaja kwa kuwa na raslimali nyingi ambazo zimekuwa hazimnufaishi moja kwa moja mwananchi wake. Na hii inatokana na baadhi ya viongozi kutoka kutowajibika ipasavyo katika kutetea maslhai ya wananchi wake ambao ndio waliompa dhamana ya kuwatetea kwa kila jambo lenye tija 

Miaka kadhaa nyuma hakuan mtu ambae alidhani  mkoa wa Mtwara ungekuwa ni Moja kati ya Mikoa inayoangaliwa kwa jicho la pekee na wawekezaji kute duniani, Lakini kutokana na kugundulika kwa gesi miaka kadhaa iliyopita kumepelekea mkoa wa mtwara kuwa ni mkoa ambao hivi sasa unaangaliwa kwa jnicho la pekee na serikali katika sekta mbalimbali ikwemo sekta ya nishati na madini

Kugunduliak huku kwa gesi hii wananchi wa mtwara walikuwa wakitegemea kuwa ndio kwanza watakuwa wameondokana na u8maskini kutoka na upatikanaji wa wingi wa huduma ya umeme ambao utakuwa ni wa bei rais kwao kwa kuwa ni moja kati ya raslimali zao.

Sehemu yeyote inayofayika utafiti na mali za wananchi zikaathirika kutokana na utafiti huo basi wananchi wanatakiwa kufidiwa kile walichokipoteza kutoka na utyafiti huo unaofanywa sehemu yao...Baada ya zoezi la utafiti kufanyika na kugundua uweopo wa gesi huko msimbati na kuanza ujenzi wa miundombinu ya kuhakikisha gesi inafikishwa mtwara mjini ndipo hapo wanachi waahidiwa kulipwa kutokana na kile kilichoharibiwa wakati wa utafiti huo

Sasa imepita mwaka toka utafiti huo ufanywe na wananchi wakitegemewa kulipwa pesa zao leo hii kunafanyika tena upimaji wa mali za wananchi ili waweze kulipwa..swali je kile kilichokutwa mara ya mwanzo kinakuwepo kwa sasa? huu sio mpaqngo wa kutaka kuwanyima haki yao ya msingi wananchi kutokana na uhakiki wa mwanzo uliofanywa?..wakati huohuo wananchi wa mtwara wakiwa wanalalamika kwa nini gesi iondolewa kupelekwa dar es salaam kabla ya wana mtwara kunufaika nayo? 

wasiwasi wangu mimi tusijekuona wananchi wanaingia barabnarani kudai haki zao za msingi kuhusiana na suala hili.....................................viongozi kuweni makini katika hili mapema 

........swaumu njema  wadau wengu