Sunday, August 4, 2013

Wasanii wa Mtwara wapewa somo

Mziki unakuwa kila kukicha na wasanii wanaongezeka sio tu kwa dar es salaam ila kwa kila mkoa, wilaya na hata kata na vijiji 

Wadadisi wa Mambo ya Burudani walishawahi kusema kuwa kila ukipita nyumba 3 lazima ukutane na familia moja yenye msanii

Kuongezeka kwa wasanii hawa inatokana na maslahi yaliyokuwepo kwa sasa kwa wasanii wenyewe ambapo kwa sasa kama unatoa nyimbo inayokubalika kwa jamii tegemea kipato chako sio chini ya milioni 2 kwa kila ukipata jukwaani

Mkoa wa Mtwara ni moja kati aya mikoa ambayo inahazina kubwa ya wasanii hususani wale kwa kizazi kipya (bongo fleva)

Miongoni mwao wanautangaza mkoa huu wa Mtwara katika ngazi za kitaifa mfano Pasha, Kigwema Das Lameck na wengineo

Uwepo wa wasanii hao na wengine wanaochipukia wakiwemo Gitaa, Young Stable, Kibega,Pg,Young Chibo na wengineo unaufanya mkoa huo wa Mtwara kuwa na hazina kubwa ya wasanii endapo watatambua kazi zao ni nini hasa kwa jamii

Licha ya uwepo wa Production Nzuri ikiwemo 29 Reccods, Pisha Reccod na mama land pia bado  wasanii hao wamekuwa wanashindwa kuzitumia vizuri kupata mafaniko makubwa kutokana na kazi zao

Mafaniko ninayoyazungumzia hapa sio ya kutoa nyimbo tu bali pia kupata mialiko mbalimbali kutokana na ubora wa kazi zao na hii inategemea na wasanii wenyewe walivyojirahisisha kwa mashabiki wao

Tatizo kubwa ninaloliona hapa ni wasanii wa Mtwara kwa sasa kuwa na shida ya kusikika tu Radio nyimbo zao zikipigwa na sio harakati za kufanya hata shoo kadhaa kutokana na kazi zao

Nimefanya utafiti wa kutosha juu ya hili ambapo nimegundua hilo kwa wasanii waliokuwa wengi waliopo mtwara kwa sasa hawana mipango mingine baada ya nyimbo zao kupigwa radio kitu ambacho kinapelekea hata mashabiki wao nao kutokuwa na jipya kutoka kwa wasanii wao pale wanapo waona zaidi ya kusema 'nakukubali sana mwanangu kaza buti utatoka tu'

Utoaji wa nyimbo kwa kila baada ya mwezi au hata wengine baada ya wiki mbili nalo limekuwa tatizo la wasanii hawa maana wanashindwa kujua kama nyimbo iliyotolewa mwanzo kama imefanya vizuri ama la na hii inatokana na pia studio ama produza nao kujirahisisha kwa wasanii wao kitu kinachopelekea msanii kila siku atoe nyimbo

Mfano kama produza anatengeneza nyimbo kwa shilingi 150000 atakaetoa pesa hizo kati ya kumi ni mmoja kwa mujibu wa Sully Produza kutoka 29 Rekodi kitu ambacho hata utengenezaji wa kazi zao nao hautakuwa na ubora mkubwa kutokana na kutolipa kiasi kinachotakiwa

pasha
Nilibahatika kuongea na Sully na kumpa changamoto hii ya kuwalemaza wasanii wa Mtwara kwa kutowalipisha gharama zinazostahili katika utengenezaji na kazi zao kitu kinachopelekea wasanii hao kuwa hatarini kupotea endapo tu mfumo wa ulipaji wa pesa inayostahili utakapoanzishwa moja kwa moja na maproduza hao maana walishazoea sana kuslaidi kama msemo wa ndugu yangu pg anavyosema

Sully alinihakikishia kwa sasa ameanza utaratibu huo wa kuwataka wasanii sasa walipe pesa zote za kurekodi nyimbo vinginevyo atakuwa tayari kufanya kazi na wasanii waliokuwa lebo kwake ama wenye uwezo wa kupia kiasi anachokitaka

sully
Tunataka kuona sasa mabadiliko katika sanaa ya kizazi kipya Mtwara kwa kuona harakati nyingine zaidi baada ya nyimbo kutolewa na kusikika radio, mfano shoo nyingi na sio tu kutegemea upigiwe simu kuambia kuna shoo na utalipwa shilingi ngapi , bali hata kutengeneza ukaribu na watu wenye kumbi na vyombo vya mziki katika kuandaa shoo za pamoja ili kuendelea kuwafanya mashabiki wako kuona unaharakati za kuwafanya wawe karibu yako zaidi kutokana na kazi zako na harakati zako

Sio kusubiri kuambiwa kuna shoo kitu ambacho unaweza kukaa hata mwaka mzima haujafanya shoo yeyote ile kwa mazingira ya Mtwara

Zipo kumbi nyingi za bududani kwa sasa Mtwara ikiwemo masiha Club na makonde royal night club kumbi ambazo hujaza mashabiki nykati za wikiendi na hata wanapokuja wasanii kutoka dar es salaam wamekuwa wanajaza mashabiki wengi kitu ambacho hata wasanii wa kusini wanaweza kufanya endapo tu wanatakuwa karibu na wamiliki wa kumbi hizo kwa kuandaa hata shoo ya wasanii wa kusini kila jumamosi ya mwisho wa mwezi na kadhalika 

Uwezo wa kuwafanya mashabiki waokulipa kiingilio cha elfu tano kwenda kuwaona wasanii wa kusini upo endapo watajitambua tu 

Hii ni changamoto kwenu wasanii wa kusini sasa kuamka na kuchangamkia fursa zilizopo kwa sasa mkoani mtwara 

NB; Huu ni mtaamo wa mmiliki wa blog hii na isichukuliwe kama wasanii hawa wamedharauliwa na hawawezi mziki ila tunataka kuona matokeo chanya ya kazi zao kwa jamii