Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kimeamua kuwatolea uvivu kwa kuwavua uanachama na uongozi
madiwani wake wanane katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
Imeelezwa kwamba hatua hiyo imechukuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM
mkoa wa Kagera kutokana na kudaiwa kupuuza maelekezo yaliyotolewa na Mwenyekiti
wa CCM, Taifa, Rais Jakaya Kikwete.
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa CCM wa mkoa huo Avelin
Mushi, na theNkoromo Blog kuipata, imesema kuwa uamuzi huo umekuja kutokana na
chama kujali maslahi ya wananchi tofauti ya watu binafsi.
Mushi amewataja madiwani hao nane kuwa Yusuph Ngaiza (Kata
Kashai) ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya Bukoba, Samwel Ruangisa (Kitendagulo)
ambaye ni Meya mstaafu na Mkuu wa mkoa wa mkoa wa kwanza wa mkoa wa Kagera,
Murungi Kichwabuta (Viti maalumu) Deusdedith Mutakyawa (Nyanga) Richard Gaspal
(Miembeni)Alexander Ngalinda (Buhembe) ambaye pia alikuwa Naibu MeyaDauda
Kalumuna (Ijuganyondo) na Robert Katunzi wa kata Hamugembe.
Mushi amesema kuwa kufukuzwa kwa madiwani hao ni kutokana na
mgogoro ulidumu kwa muda mrefu juu ya mbunge na meya ambapo Rais Kikwete akiwa
ziarani Kagera alitoa agizo la wanachama hao kutoendelea na mgogoro huo.
Pia, amesema kuwa vikao vya chama vimekuwa vikiendelea kwa kufuata
kanuni na taratibu kwa kuwaonya juu ya kuhujumu serikali ya CCM kwa
kushirikiana na madiwani kambi ya upinzani kutotekeleza maendeleo ya wananchi
lakini wahusika wote wamekuwa wakikahidi maagizo ya kuitwa kwenye vikao.