Roma |
Kampuni ya bia ya
Tanzania Breweries Limited (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro
Premium Lager, inang'oa nanga katika awamu ya pili ya tamasha lake kali
za muziki la ‘Kili Music Tour 2013’ wikiendi hii Jijini Mwanza.
Tamasha hili kubwa litafanyika jumamosi ya tarehe 17 Agosti, 2013 mjini Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba na litajumuisha wasaniii 11 ambao ni Diamond, Snura Mushi, Professor J, Lady Jay Dee, Roma, Dabo, Bob Junior, Ben Pol, Kala Jeremiah, Fid Q na AT.

Lady Jay Deee |
Kwa mujibu wa
taarifa iliyotolewa na Meneja wa bia ya Kilimanjaro George Kavishe, matamasha
ya Kili Music Tour 2013 yalikuwa yamepumzika kwa muda wa mwezi mmoja sasa,
yanaendelea tena kwa kishindo kwenye mikoa mitano iliyobakia.
Bw. Kavishe
ameeleza kuwa “Bia ya Kilimanjaro Premium Lager inaendelea kutoa bonge la
kiburudisho kwa watanzania kwa kuhakikisha kuwa kila mkoa unapelekewa wasanii
mahiri kabisa wa muziki wa Bongofleva hivyo mashabiki wa muziki wakae mkao wa
burudani.