Baada ya maneno na tuhuma nzito za Ney wa Mitego dhidi ya Mshindi
wa Epiq Bongo Star Search mwaka 2012, Walter Chilambo kuwa huenda amedhulumiwa
zawadi yake ya ushindi, Shilingi Milioni 50 na waratibu wa shindano hilo kwa
sababu mpaka sasa yupo katika maisha duni, Msanii huyu amevunja ukimya na
kusema kuwa yeye yupo vizuri kifedha.
Walter amesema kuwa maneno ya Nay hayana ukweli wowote na yeye anaishi vizuri na hadhani kama Nay wa mitego alikaa chini na kufikiria kabla ya kuongea kuhusiana na issue hii katika wimbo wake, wala hakufanya uchunguzi wowote ambao uliomhusisha yeye.
Walter amemaliza kwa kusema kuwa, Maneno haya hayamuumizi kwa vile hayana ukweli wowote, na vilevile hayawezi kumuondolea mashabiki wake.