Kesi ya jinai
inayomkabili muigizaji Wema Sepetu, ya tuhuma za kumpiga vibao vitano meneja wa
hoteli ya Mediterano , pamoja na kuharibu mali za hoteli hiyo, imeahirishwa leo
hii pia mpaka tarehe 20 mwezi wa nane.
sakata hilo lilitokea
siku ya tarehe 4 mwezi wa 4, kesi yake ya kwanza ilisomwa siku ya tarehe 17, na
kuahirishwa mpaka leo hii, na baada ya kufika mahakamani leo hii na Wema
kukataa mashtaka hayo, kesi imeahirishwa tena mpaka tarehe 20 mwezi wa 8.
"Siku ya kwanza
ya keshi hiyo wanaume walikuwa wengi, lakini leo hii imekuwa tofauti, wasichana
walikuwa wengi yaani marafiki zake wakiongozwa na Kajala, walifika majira ya
saa mbili na robo na waliitwa sehem maalum (chemba) kwa ajili ya kusikilizwa
kesi hiyo, na keshi hiyo ilisomwa ila ilihairishwa mpaka tarehe
20/08/2013" amesema Mwahija (mwandishi wa habari wa kujitegemea).