Wednesday, February 20, 2013

YANGA YAENDELEA KUANDAA DOZI YA AZAM

.
yanga wakiwa mazoezini(picha na maktaba)
 
kikosicha Young Africans leo asubuhi kimeendelea na mazoezi katika uwanja wa Mbegani nje kidogo ya mji wa Bagamoyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wake dhidi ya timu ya Azam Fc siku ya jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Young Africans ambayo imeweka kambi katika hoteli ya Kiromo - Bagamoyo tangu jana mchana kujiandaa na mchezo huo, leo asubuhi imefanya mazoezi chini ya kocha mkuu Brandts, kocha msaidizi Fred Felix 'Minziro' na kocha wa makipa Razaki Siwa huku wachezaji wote wakiwa katika hali nzuri kiafya na kiakili kuelekea katika mchezo wa jumamosi.

Kikosi cha mholanzi Ernest Brandts kinaonekana kuwa kwenye hali nzuri na wachezaji wote wanaoekana kuwa kwenye ari ya mchezo huo wa jumamosi kwani mechi hiyo ndio itakayotoa taswira ya msimamo wa Ligi Kuu kuelekea katika mbio za kutwaa Ubingwa.


Young Africans ambayo katika mchezo wake wa mwisho iliibuka na ushindi wa jumla ya mabao 4-0 dhidi ya timu ya African Lyon huku safu ya ushambuliaji wa timu ya Yanga ikionekana kuwa na uchu wa kucheka na nyavu katika kila mchezo.

Akiongea na www.youngafricans.co.tz Brandts amesema kikosi chake kipo katika hali nzuri, mazingira ya kambi ni mazuri, wachezaji wanapata fursa ya kukaa pamoja na kushiriki mazoezi kwa pamoja katika hali ya utulivu hali inayongeza umakini katika kuelewa maelekezo yake
 
Najua macho na masikio ya wapenzi wa soka nchini yansubiri kuona nini kitatokea siku ya jumamosi, ukweli ni kwamba huo ni mchezo muhimu sana kwetu ili kujijweka katika hali nzuri ya kuendelea kuongoza ligi , hivyo nachoweza kusema ni kwamba nimekiandaa kikosi changu ili kiweze kuibuka na ushindi katika mcheo huo siku ya jumamosi 'alisema Brandst'

Aidha Brandts alisema anafarijika kuwa na wachezaji wake wote 26 kambini kujiandaa na mchezo huo wa jumamosi, wachezaji wote wapo safi kiafya, kiakili na morali ya kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo huo, hivyo nashukuru kuwa fit kwa kikosi changu chote nitapata fursa ya kumtumia yoyote kati yao

Young Africans inaongoza msimamo wa VPL kwa kuwa na pointi 36 huku ikiwa imecheza michezo 16, imeshinda jumla ya michezo 11, imetoka sare michezo mitatu (3) na kupoteza michezo miwili (2) huku ikiwa imefunga jumla ya mabao 33 na kufungwa mabao 12 tu.


Nafasi ya pili inashikiliwa na timu ya Azam FC yenye pointi 33 ikiwa na mabao 27 ya kufunga na ikiwa imefungwa mabao 14 ambayo leo inashuka dimba la chamanzi kucheza na timu ya JKT Ruvu katika muendelezo wa michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom.