Saturday, April 20, 2013

JOSE MOURINHO AMTIMIZIA NDOTO KIJANA MSAFISHA MITAA ALIYESAFIRI KUTOKA MAREKANI KWENDA SPAIN KUONA EL CLASSICO - NA KUMPA KAZI REAL MADRID

 


 
Soka ina muda mchache kwa stori za kugusa moyo siku za hivi karibuni, lakini kama kuna mtu anaweza akatengeneza stori za kugusa mioyo ya watu basi ni Jose Mourinho Special One.

Katika stori ya kusisimua, Meneja wa Real Madrid ameweza kuyabadilisha maisha ya raia mmoja wa Mexico kutoka kuwa msafisha stesheni za treni mpaka kuwa mmoja ya watu muhimu ndani ya timu yake.

Abel Rodriguez, 41, ambaye alikuwa akifanya kazi ya kusafisha stesheni za treni jijini Los Angeles, alitumia fedha zake chache anazopata kupitia kazi kusafiri mpaka ulaya na kujaribu kuangalia El Clasico dhidi Barcelona mapema mwezi wa pili mwaka huu.
Bila kuwa na tiketi, au hata sehemu ya kufikia jijini Madrid, kijana huyo wa kimexico alikuwa na tumaini kwamba angepata nafasi ya kuuona mchezo huo mkubwa duniani pamoja na kuweza kukutana na wachezaji.

Kibahati bahati, Rodriguez alifanikiwa kufika kwenye uwanja wanaofanyia mazoezi Real -Valdebebas training complex mara baada ya kufika Spain, akiwa na mpango wa kuwaona mashujaa wake wakiwa kwenye maandalizi ya mechi.

Hakuwa na namna yoyote ya kuweza kuruhusiwa kuonana nao, ingawa miezi michache zilizopita alifanya ya bila malipo kama kijana muokota mipira (ball boy) wakati Real Madrid wakiwa kwenye pre-season huko California, lakini hilo halikuwafanya walinzi wamruhusu kuwasogolea wachezaji wa Madrid.

Akiwa hana shilingi, hana pa kwenda huku matumaini ya kuwaona mashujaa wake kwenye El Clasico,Rodriguez alikuwa amejikalia pembezoni mwa barabara kwa takribani masaa matano - then miujiza ikatokea.

Rodriguez aliyezunguzishiwa duara akiwa ndani ya Old Trafford na Cristiano Ronaldo

'Ilikuwa ni miujiza nilimuona yule kijana,' Mourinhoanakumbuka kwa kuwaelezea Sports Illustrated. 'Nilimuona Abel akiwa amekaa pembezoni mwa barababa nje ya uwanja wa mazoezi.
'Nilikuwa naondoka kwenye gari la msaidizi wangu Rui Faria, na kulikuwa na watu wengi nje, lakini nikwambia Rui asimamishe gari, "Simamisha gari - ni yule kijana wa Los Angeles".'
'Amigo! fanya nini hapa?? Mourinho alimuuliza Abel akiwa ndani ya gari.
'Nimekuja kuwatembelea nyie,' Abel Rodriguez alijibu. 'Ni mara yangu ya kwanza kujs ulaya, na ndoto yangu ilikuwa kuja kuona mechi zenu. Hasa El Clasico.'
'Lakini zimeshaisha zote,' Mourinho alisema. 'Unaishi wapi sasa??'
'Sijafanya chochote kuhusu jambo hilo,' Mmexico akajibu. 'Kipaumbele changu kilikuwa ni kuwaona nyinyi halafu ningepanga mipango yangu. Kama nisingewaona - ningeenda uwanjani kujaribu kupata tiketi. Na kama hilo lisingefanikiwa basi ningerudi nyumbani.'

Then Mourinho akaamua kumpangia Rodriguez ambayo Real walikuwa wanakaa kujiandaa na mchezo dhidi ya Barcelona na akampa tiketi ya VIP.

Lakini Mourinho hakuishia hapo.
Duties: Rodriguez helped lay out the Real Madrid strip before their Champions League tie at Old Trafford
Rodriguez aliwasaidia Real Madrid kuvaa jezi hizi kwenye mechi ya mtoano ya Champions League pale Old Trafford

Wakati wa chakula cha usiku kuamkia siku ya Clasico, Mourinho akampa ofa rafiki yake mpya Rodriguez ya kuwa mmoja ya wafanyakazi wa Real - kama mtunza vifaa wa muda wa Los Blancos - wakati zikiwa zimebaki siku mbili kupambana na Manchester United.

Mourinho alisema: 'Nilimwambia hakuna namna angerudi nyumbani kwao, nikamwambia nitaenda nae jijini Manchester akafanye kazi kama mtunza vifaa vyetu. Nilimwambia atusadie kwa mechi hiyo na atapata nafasi ya kushuhudia mechi kubwa ya ligi ya mabingwa wa ulaya ndani ya Old Trafford.'
Rodriguez alirudi chumbani kwake na kuchukua passport yake ili maandalizi ya kazi yake mpya yaanze kufanyika. Kwa kufurahishwa na kilichotokea akaanza kulia katika meza ya chakula waliyokaa wachezaji wa Madrid.

Siku chache baadae, alikuwa ndani ya Old Trafford, akiwa amevaa sare rasmi ya Real na akiwapangia jezi wachezaji ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo.

Celebration time: Rodriguez also saw his beloved Real Madrid beat Barcelona in the Clasico at the Bernabeu
Rodriguez alipata nafasi ya kuiona timu yake ya Madrid ikishinda dhidi ya Barcelona kwenye el clasico ndani ya uwanja wa Bernabeu

Baada ya ushindi uliozua utata ndani ya Old Trafford, Rodriguez akijikuta ndani ya chumba cha Manchester United akikusanya jezi za wachezaji wa United zilizosainiwa na wachezaji wenyewe na akafanya hivyo pia kwa upande wa wachezaji wa Madrid.
Pia aliagizwa na Sir Alex Ferguson akamwite Mourinho kwa ajili ya utamaduni wao wa kunywa mvinyo kila baada ya mchezo unaowakutanisha.

Rodriguez alirudi nyumbani kwao LA na jezi zilizovaliwa na wachezaji kama Javier Hernandez, Mesut Ozil, Kaka na Michael Essien, na mmoja wa mpira uliochezewa siku hiyo.

Akikumbuka wakati akimuaga mkewe aitwaye Olga na watoto wake watatu wa kike huko LA wakati akija ulaya kujaribu kuiona timu yake aipendayo, Rodriguez alisema: 'Nilikuwa na mashaka sana juu ya kwenda ulaya, lakini ushawishi mkubwa ulikuja kutoka kwa mke wangu, ambaye aliniambia, 'Inabidi uende. Imekuwa ndoto yako kwa muda mrefu.'