William Ruto |
Majaji katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC
wameahirisha kesi ya naibu Rais wa kenya William Ruto kwa juma moja ili kumpa
mda kurejea nyumbani kushughulikia hali ya kiusalama inayokumba taifa hilo.
Watu wanoaminika kuwa
magaidi wa Al Shabaab wameteka jumba la kifahari lenya maduka la Westgate
jijini Nairobi na kuwazuilia mateka wakenya kadhaa.
Bwana Ruto anakabiliwa
na mashtaka ya uhalifu wa kibinadamu kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi wa
2007 nchini kenya.
Ruto na Rais Uhuru
Kenyatta, wanakabiliwa na tuhuma za za uhalifu dhidi ya binadamu baada ya
kudaiwa kuhusika na ghasia za kikabila baada ya uchaguzi wa mwaka 2007-2008
ambapo watu zaidi ya elfu moja waliuawa.
Mahakama iliakhirisha
kesi baada ya kikao cha dharura kuitishwa huku upande wa mashtaka ukisema kuwa
hauna pingamizi lolote ikiwa kesi zitaakhirishwa kwa muda mfupi.
HABARI HIZI KWA HISANI YA BBC SWAHILI