Friday, May 3, 2013

DIAMOND ASHAMBULIWA NA MASHABIKI WAKE BAADA YA KUKOSEA KUANDIKA LUGHA YA KIINGEREZA, SOMA HAPA


Wabongo kwa kukosoa hawajambo.. Katika pitapita yangu instagram kuna picha mkali Diamond Platnumz alipost (hiyo hapo juu), na hapo wakatokea watu kukosoa kingereza alichotumia huku wengine wakionekana kutetea. JAMANI ENGLISH si Lugha yetu jamani. angalia hapa chini watu walivyokua wakicomment

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Thursday, May 2, 2013

HUSANA IDD NA NAOMI WA BONGO MOVIE WAGOMBEA PENZI LA JANUARY


Msanii anayechipukia kwenye soko la filamu na muziki, Naomi Mbaga ameibuka na kumuonya Husna Idd ‘Sajent’ amuachie bwana wake, January.

Akizungumza na mwandishi wetu, Naomi aliweka bayana kuwa January ambaye ni Mwanamuziki wa Bendi ya Victoria ni mpenzi wake wa muda mrefu hivyo alishangazwa kuona habari mitandaoni kuwa Sajent amejituliza kwa mpenzi wake huyo baada ya kumwagana na mzazi mwenzake, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’.

“Aniachie bwana wangu, kama ameachika kwa huyo Chaz Baba atafute bwana mwingine na siyo wa kwangu. Ole wake nimkute naye siku, atanitambua,” alisema Naomi.

SIJAJA BONGO KUFUATA PENZI LA DIAMOND 'AVRIL'

 
Diamond na Avril

jana ilikuwa ni birthday ya msanii wa Ogopa Djs ya Kenya, Judith Nyambura Mwangi a.k.a Avril ambaye alitua jijini dar es salaam juzi na sababu ya ujio wake ilikuwa ni vitu vikubwa viwili.

Akihojiwa katika kipindi cha XXL kupitia Clouds fm Avril amesema ujio wake hapa bongo kwanza ni ku-celebrate birthday yake na fans wa Tanzania, na pili ni ku-launch single yake mpya aliomshirikisha Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa yuko ziarani barani Ulaya, party ilifanyika usiku wa kuamkia jana (April 30) pale Elements club.

Kuhusiana na maneno ambayo yamekuwa yakisemwa juu ya tetesi za kuwepo kwa mahusiano baina yake na Diamond Platnumz ambaye alimshirikisha Avril katika video ya Kesho, Avril amekana kuwepo kwa uhusiano wowote zaidi ya kuwa marafiki wa kawaida na wa kikazi. "Hakuna kitu chochote kati yangu na diamond na sijaja Tanzania kufuata penzi lake... we are just friends na relationship yetu ni proffesional relationship katika muziki", alisema Avril.

Hii ndo birthday party ya kwanza kwa Avril kufanya, birthdays zake zote zilizopita alikua anasheherekea kwa kuchill tu nyumbani na familia yake.

MITIKASHI SASA KWENYE VIDEO

Ngoma ya mitikashi inayofanya poa mtwara town iliyoimbwa na kibega inatarajiwa kufanyiwa video siku sio nyingi kutoka hii leo

kibega

ishu za kushutiwa video ngoma hiyo imethibitishwa leo na mwenyewe kibega wakati alipokuwa anazungumza na Swiraty blog na kusema kuwa videoo hiyo itatengenezwa mtwara town na sehemu nyinginezo ikiwemo daraja na mkapa pamoja na baadhi ya klip zitapigwa nchi jirani ya msuimbiji

Ngoma ya mitikashi imeonekana kufanya poa sana kwa upande wa audio na sasa mashabiki waliokuwa wengi wansubiria video yake itakuaje

video ya ngoam  hiyo itafanywa na kikulacho ambaye ndo amekuwa anazipika viudeo za wasanii wengi mtwara town

SOMA HAPA ALICHOPANDIKA DJ ASKOF

DJ askof na Salama Jabir

Kutokana na vijana weng wa mjin kujiita wanyama,Unadhani kuna u-lazima serikali kuandaa mbuga moja kubwa ya Wanyama iwe Hata Dsm?Mtazamo wako...

ANGALIA ALICHOSEMA LULU WA SAFARI RADIO

lulu

Mmoja kati ya wasanii toka kundi la Dallaz connection 'lulu' amefunguka kuhusu ishu za yeye kufanya kahojiano na mtu yeyeote na media yeyote ile njia gan azipitie ili mchongo ukae p[oa

Lulu amefunguka kuwa kwa sasa yeye yuko chini ya Dallaz so kwa yeyoote anayehitajki kupiga nae interview anatakiwa awasiliane na uongozi wake kwanza then yeye apewe taarifa ya uongozi wa dallaz ambao uko chini ya DJ SAM

Akiongea na Swiraty blog LULU amesema yeye hakatai interview ila ishu ni kwamba lazima afuate utaratibu wa kundi

"sikia bandugu hapa ishu ni kufuata utaratibu kwa sababu mimi kwa sasa nipo chini ya dallaz kwa hiyo itakuwa ngumu kuweza kufanya mahojiano bila uongozi kujua' alisema lulu

Dj sam kwa upande wake kadai huo nido utaratibu kwa dallaz kwa wasanii wao waalio ndani ya kundi hilo

Ishu imefi9kia hapo baada ya hosti wa shoo moja ya tv hapa mtwara town idrisa bandali kumuomba lulu kufany7a nae mahojiano ya live kwenye kipindi chake jumamosi hii

alipoulizwa idrisa alisema' yes ni kweli mzazi ishu ziko hivyo sikua nafahamu kama lulu yuko dallz ningefata utaratibucoz sio kwke tu wasanii wengi walio ndani ya kundi huo ndio utaratibu wao sio ishu ngeni sana kwangu ' alisema bandali

Wednesday, May 1, 2013

WOSIA WANGU KAMA IKITOKEA NIMETANGULIA KUFA KABLA YA RUGE AU JOE KUSAGA

Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.
Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.
Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.
Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.

Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.
Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.
Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.
Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao.
Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.
Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame. Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.
Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai. Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.
Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.
Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.
Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.
Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..
Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..
Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.
Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani?? Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??
Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.
Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma?? Roho gani hiyo??
Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu
JIDE

HAPPY BIRTHDAY DJ SAM

Uongozi wa SWIRATY BLOG unamtakia kila la heri katika siku yake ya kuzaliwa C.E.O wa Dallaz Connection toka safari radio DJ SAM

"Wengi walipenda kuwepo na kuiona siku kama hii kwako ya kuazaliwa kwao lakini mungu kawapenda zaidi hawakuweza kuiona siku hii so muombe mungu kila leo ili uweze kufanikiwa katika harakati zako mzeee...

happy birthday...happy birthday......dj saaaaaaaaaaaaaaaammm......

dj sam akiwa na lulu

mwenyewe dj sam kaandika hivi katika ukurasa wake wa facebook

''''' nashkr mungu muweza kwa kuniweka pumzi mpk leo hii ikiwa leo ikiwa nafurahia tarehe yng ya kuzaliwa,mungu mkubwa sn na ndio tegemez la kila mwanadam na viumbe vyake vyote umeweza kunilinda kwa wakat wote na kuniongoza vyema kwa kila jambo nilifanyalo,inshaalawah naomba rehema zako ziongeze kwa mja wako kwa siku zijazo tena,mungu bariki familia ya ngu,pia waweke mahali pema pepon (mr &mrs mtepa) ameen.

ADAM MCHOMVU KUTAMBULISHA SINGLE 2 MPYA NDANI YA BILICANAS



 
Mtangazaji wa Clouds Fm ambae pia ameamua kujiingiza katika mziki "Adam Mchomvu" A.K.A Baba Jonii, siku ya jumapili atatambulisha ngoma zake mbili mpya ndani ya Maisha Club.Siku hiyo Adam atatambulisha ngoma ambayo siku za nyuma aliwaonjesha kidooogo mashabiki wake kupitia kipindi cha XXL ikiwa kama demo, lakini kwa hivi sasa imeshakamilika "Unaakili wewe", pamoja na pini lingine alilolifanya na wasanii kutoka Rada entertainment, ambapo chini ya Rada kuna Ngwea, TID, Romy Jones na wengineo. Wasanii hao pia kutoka Rada entertainment wakuwepo kwa ajili ya kutoa perfomace, kumbuka ni jumapili hii ndani ya Maisha Club
Adam Mchomvu
ok jumapili @ club bilicanas BABA LA BABA (BABA JONII) ntazindua track zangu mbili ... ebu dondoka pale uone utofauti ya mimi na wao, ofcuz nimepika na mzee mnya ma T.i.D, ZAMBADA M2 MBAYA KAIZA SOSA BABUU WA KITAA, ROMMY JONES its rader ent baby... miss dar indian ocen watapiga show fupi.. so watu wabaya tukutane ubayani... mzee amesema!!!!!!

CHECK OUT:SINGLE MPYA YA IZZO"LOVE ME" ILIVYOPOKELEWA NA MASHABIKI NDANI YA AMBASSADORS LOUNGE


Baada ya miezi mitatu tu tangu Izzo alipoachia single yake akiwa na Ngwea na Quick "Ball Player",sasa usiku wa kuamkia leo ndani ya Ambassadors Lounge ameachia single nyingine mpya "Love Me" ambayo ipo ki mapenzi zaidi akiwa na Shaa pamoja na Barnaba.

Hizi ni picha za mastaa na watu mbalimbali waliofika Ambassadors Lounge kusikiliza Single mpya ya Izzo Biashara ambayo ilipilipigwa live


masta jay nae alikuwepo ambassadors
 

 
lina na wadau wake
 
barnaba nae alikuwepo
 

NEY WA MITEGO ACHUKUA MCHUMA WA MILION 35


msanii anewakilisha Manzese, Ney wa Mitego, amethibitisha kumiliki gari lenye thamani ya sh milioni 35 aina ya Mark X.

"yaa ndio gari yangu mpya hiyo, nimenunua juzi kwenye show room ya jamaa mmoja hivi anaitwa Monea, kama milioni 35 hivi, mpaka ileee mi nakuwa nayo mkononi." amesema Nay

Kwa mziki anaofanya Nay, watu wengu wamejiuliza kama kweli mziki ndio ulimfanya kumiliki gari hilo ama kuna ishu zingine zimemuwezesha kupata ndinga hiyo.

"Mziki unachangia kwa asilimia kadhaa pia, ijapokuwa siwezi nikasema moja kwa moja ni mziki, lakini mziki umechangia, kuna hela ya mziki pia katika hili, mi ni mfanya biashara, nafanya biashara nyingi, aaah na mziki pia ni moja kati ya biashara zangu, so mziki pamoja na biashara zingine zinafanya mi naendesha maisha yangu, na nna miliki hivi ninayomiliki" amesema Nay

Ney pia amezungumzia kuhusu picha ambayo inaonekana kwenye mtandao wa facebook, inayomuonyesha akiwa hana shati, na akiwa ameshikilia bastola..
"Aaaah,mi nahisi siko tayari kulizungumzia hilo, siko tayari tu kuongelea chochote kuhusu hiki ambacho unaniuliza sasa hivi, lakini aaah nitakapo kuwa tayari nitasema nipo tayari na nitaongea kile ambacho ntaweza kukiongea." amesema Nay

Tuesday, April 30, 2013

SOMA HAPA ALICHOKIANDIKA ROMA MKATOLIKI

Rapper Roma Mkatoliki ni mshindi wa tuzo za KTMA 2012 lakini mwaka huu 2013 hajapata nafasi yoyote ya kuwa nominated kwenye list, ni miongoni mwa mastaa wa hiphop ambao hawako kwenye list kabisa mwaka huu ambapo moja ya vigezo vya msanii kushiriki kwenye tuzo za ni lazima wimbo wake uwe umefanya vizuri kwa mwaka uliopita.
.
.
.
.

TOP 20 ZA JOGOO FM ZAJIBU MALALMIKO YA WADAU WAKE


Mtangazaji wa kituo cha Radio cha JOGOO FM iliyoko Mkoani Ruvuma, Radio hii ni moja kati ya Radio zinazotikisa Mkoani Ruvuma …Anaejulikana kwa jina na Millan Allan ametamka maneno haya

Wengi wamekuwa wakizungumza kwa nini Top 20 za JOGOO FM hazisikiki nyimbo za manton (mbele), ishu kubwa ni kwamba nataka kuinua mziki wetu wa nyumbani….kuendeleea kupiga nyimbo za wasanii wa mbele ni kuudidimiza mziki wetu wa bongo ambao unatutegemea sisi tuuinua hapa ulipo

So wadau wafahamu hivyo na itaendelkea kuwa hivyo wa top 20 za JOGOO FM kwa sababu tumeamua kuwasaidia wasanii wetu kwa nini sasa tusipige nyimbo zao mara nyingi tuwezavyo?

DIAMOND NDANI YA SPORAH SHOW...

Napenda kumshukuru Mwenyzi Mungu kwa siku ya leo.....
Nikiwa mbali na uso wa nyumbani...
Nikiwa Mwenye Afya tele na Furaha tele....Mimi na
Dancers wangu kwa ujumla tukiwa bado kwenye
Tour yangu Nchinu Uingereza....!! Siku ya leo baada ya kuwaa
na mizunguko ya hapa na pale
midaa ilipowadia nilikuwa na Mualiko wa Interview kwenye
kipindi chenye Umaarufu mkubwa
nchini Uingereza na Africa nzima kinachoendeshwa na
Mwanadada Nguli Mtanzania,Sporah..!!
Kipindi kinachoruka kwenye channel nyingi barani
africa na Tanzania wa ujumla...!!

Zifuatazo ni picha kadhaa wakati nawasili kwenye Kipindi
cha Sporah show na Interview Nzima!

On set Nikijiweka tayari....msaf as always .....presdent himself mwenyewe!!!

 
Hapa nikiwasili kwenye Studio za sporah show...with my
craizee boys from left Dumi Utamu & Right
Moses Iyobo.......WASAAFIIIII


 Picha kwa hisani ya This is Diamond

DALLAZ CONNECTION YATOA MCHONGO WA WASANII

dj sam


Dallaz Connection imetoa dili kwa wasaniui chipukizi mtwara town na sehemu nyingine wenye vipaji wa kike na kiume kujitokeza ili waweze kujoin na kundi hilo kali hapa town

C.E.O wa Dallaz Connection Dj Sam aetoboa siri kwamba lengo kubwa ni kutaka kuwasaidia wasanii haop ambao pengine wanavipaji lakini wamekosa mkwanja wa kwenda kurekodi studio

Dj sam ameiambia SWIRATY BLOG kwa yeyote aliye tayari awasiliane nae kwa namba za simu zifuatazo 0658202221

Hii ni dili nyingine ambayo wasanii chipukizi wanatakiwa kuichangamkia ili waweze kutoka kisanaa hapa town