Wednesday, November 13, 2013

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari kutoka kwa Kamanda Polisi Mkoa wa Mbeya

MAJAMBAZI 8
“PRESS RELEASE” TAREHE 13.11. 2013.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA SARE ZA JESHI.
MNAMO TAREHE 12.11.2013  MAJIRA YA  SAA 17:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KAMFICHENI, KIJIJI NA KATA YA   MKWAJUNI, TARAFA YA  KWIMBA, WILAYA YA  CHUNYA MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA  TRAIPHONE S/O MWANG’ONDA, MIAKA 24 ,KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA VWAWA WILAYA YA  MBOZI AKIWA NA SARE ZA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA [JWTZ] AMBAZO NI SURUALI MOJA, KOFIA MBILI NA FILIMBI MOJA. MBINU NI KUTUMIA SARE HIZO KATIKA MATUKIO YA  KIHALIFU. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA   JAMII KUACHA TABIA YA  KUMILIKI/KUTUMIA SARE ZA MAJESHI YA  ULINZI NA USALAMA  BILA  UTARATIBU KWANI NI KINYUME CHA SHERIA ZA NCHI NA ATAKAYEBAINIKA HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAKE ZITACHUKULIWA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MTU/WATU/KIKUNDI KINACHOMILIKI SARE ZA MAJESHI YA  ULINZI NA USALAMA IKIWA NI PAMOJA NA SILAHA KWA NIA YA  KUFANYA UHALIFU AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO TAREHE 12.11.2013  MAJIRA YA  SAA 14:30HRS HUKO KATIKA ENEO LA STENDI KUU, KATA YA   MBALIZI ROAD,TARAFA YA  SISIMBA, JIJI NA  MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA  ANYELWISYE S/O JOHN, MIAKA 22, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA MTAA WA MAJENGO  AKIWA NA BHANGI KETE MOJA SAWA NA UZITO WA GRAM 5. MBINU NI KUFICHA BHANGI KWENYE MFUKO WA SURUALI. MTUHUMIWA NI MVUTAJI WA BHANGI.  TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA   JAMII KUACHA TABIA YA  KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI- ACP]
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.