KWA HABARI ZILIZO HARIRIWA NA KUHAKIKIWA NA WACHAMBUZI MAKINI USIKOSE KUTEMBELEA HAPA KILA SIKU
Tuesday, May 7, 2013
TID Ashangaa Maamuzi Haya Ya KILI MUSIC AWARDS ... "Hii Maana Yake Nini ... "
Mwanamuziki maarufu TANZANIA, TID anaemiliki bendi yake inayofahamika kama TOP BAND ambayo hutumbuiza kila weekend ameonekana akilalamikia Tuzo za KILI AWARDS zilizoingia kwenye upigaji wa kura sasa ...
LAURYN HILL KWENDA JELA MIEZI MITATU
Ingawa Lauryn amelipa dola 900,000 wikiendi liyopita lakini bado anaenda jela kwa miezi mitatu.
Amelipa karibia dola milioni moja kutokana na kodi za nyuma alizokuwa akidaiwa lakini bado mwanadada anakwenda jela limeripoti Associate Press.
Msanii huyo 1st lady wa kundi la zamani la Fugees amehukumwa kwenda jela miezi mitatu hii leo katika mahakama iliyopo anapoishi Newwark New Jersey Marekani.
Lauryn Hill alikuwa afungwe miaka mitatu jela lakini hukumu yake imepunguzwa hadi kufikia miezi mitatu, Baada ya kukutwa na kosa hilo la kukwepa kodi kati ya 2005 - 2007.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Lauryn Hill kuingia jela na pia anaweza akatoka mapema baada ya mwezi.
DIAMOND ATIA AIBU UINGEREZA

Mtanzania ambaye kwa sasa ni raia wa Uingereza na anayechezea klabu ya Chelsea, Adam Nditi ameiponda show ya Diamond mjini Reading nchini humo na kudai ilikuwa ni aibu tupu.
“Diamond jana manyago aibu tupu waswahili lazima tubadilike it’s embarrassing,” ametweet.
“Hajafanya jambo lolote ila shoo ilikuwa very unprofessional kwenye tangazo walisema inaanza saa 3 usiku jamaa amefika saa 1 asubuhi.”
“Jukwaa lilikuwa ovyo kama vile watu hawajalipa kumuuona mmoja Wa wasani wanaotamba bongo nyimbo zilikuwa zinapigwa redioni alikuwa haimbi.”
Kwa sasa Diamond yupo ziarani nchini Uingereza.
Sunday, May 5, 2013
Saturday, May 4, 2013
"HAKUNA ZAWADI KUBWA NILIYOPEWA NA MUNGU ZAIDI YAKO DIAMOND...NAKUPENDA SANA"......PENNY

Pengine utundu wa Diamond ndo kitu pekee kinachowafanya akina dada wamgombanie..Leo ni birthday ya Penniel Mungilwa na mpenzi wake Diamond Platnumz, amemwandikia maneno matamu.“Sometimes I wish you could know how much you mean to me…its a lot’..fu***n a lot, I can’t even explain it.. It’s even more than money… sometimes I don’t even know how to col u, a wife, friend,sister,bedmate, partner.. Ooh God! I don’t know coz you are more than dat,”
“Siku zote umekuwa mwema, mkarimu,mpole,nidhamu na mwenye mapenzi tele juu yangu…. You always should keep this in your mind “I LOVE YOU SO MUCH”… Happy birthday Darling.”ameandika Diamond
Kwa maneno haya, hakuna msichana anayeweza kujizuia kulia kama akiambiwa na mpenzi wake.
Baada ya kuona ujumbe huo ulioandikwa na Diamond kwenye Instagram, Penny amejibu:
“Baby u just made me cry!! Oh God Naseeb I luv u so much hubby…wallahi sina hata cha kujibu to make u understand How I appreciate ur sweet luv,God has given me so many things but bringing u in my life is the best gift I have received…U just made my day,years,a lifetym…I wont forget this…thank u hubby.”
HAPPY BIRTHDAY PENNY.
ISOME HAPA KAULI YA SHILOLE KUHUSU KUTUMIA KONDOM
Mwigizaji na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Zena Mohamed, maarufu kwa jina la shilole amedai kuwa anaweza kufanya ujinga wowote humu duniani lakini linapokuja suala la mapenzi kamwe hawezi kwenda pekupeku ( bila condom ) ....
Akiongea kwa kujiamini ,Shilole alisema kuwa hata mtu awe vipi, au awe wa dini gani au awe na pesa kiasi gani kamwe hawezi kumvulia nguo kama hana kondom mkononi.....
Msanii huyo alienda mbali zaidi na kuzilaani kauli za baadhi ya watu zinazosema eti ukitumia "CONDOM" ladha ya mapenzi inapungua.Yeye anadai kuwa ni mdau wa "GEMU" hilo na huwa anatumia NDOM kama kawa na hufurahia kama kawaida...
" Hata niwe nimelewa kiasi gani huwa nipo makini sana maana najua vijana wengi wa mjini wananimezea mate....Waje tu , lakini bila KINGA wataambulia PATUPU!!” Alisisitiza Shilole
WOLPER AIJUTIA HISTORIA YAKE YA MAPENZI
DIVA wa kiwango cha juu cha filamu hapa Bongo, Jacqueline Wolper, ameonekana kujutia historia yake ya kimapenzi baada ya kufungukia kitendo cha yeye kumuanika kila aliyekuwa akimpenda kwamba kimemtibulia na sasa amejifunza kutokana na makosa.
Jacqueline Wolper.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Wolper alisema kuwa, kwenye maisha yake ya huko nyuma ameshajianika akiwa na wapenzi tofauti lakini sasa atakayempa nafasi kwenye moyo wake hatamuanika ila hilo litakuja baadaye sana kwani sasa hivi kaweka pembeni kwanza mambo ya mapenzi.
“Sitaki yajirudie yaliyotokea katika maisha yangu ya huko nyuma, hata hivyo sasa hivi niko bize sana na kazi, mambo ya wanaume nimeamua kuyaweka pembeni kwanza,” alisema Wolper na kuongeza:
“Sitaki itokee kama ilivyokuwa kwa Dallas ambapo kila mtu alijua alikuwa ni mtu wangu, kwa sasa nimeamua kutulia kwanza na hata nikimpata mwingine watu hawatamjua hadi wakati wa ndoa
Friday, May 3, 2013
PICHA 3 ZINAZOONESHA MUONEKANO MPYA WA VIDEO QUEEN AGNES
![]() |
![]() |
MSIKIE DIAMOND HAPA AKIZUNGUMZA NA FANS WAKE BILA KUMSAHAU MUUMBA WAKE
GUCCI MANE ATOKA JELA
Rapper Gucci Mane ameachiwa kutoka jela Geogia baada ya kukaa kwa takribani wiki tatu jela.Kama nilivyoripoti siku ya tarehe 13 april kwa kukiuka masharti,tangu siku hiyo aliwekwa ndani.
Mwanasheria wa Gucci Drew Findling, amesema, ukiukaji muda wa majaribio na Gucci ulisababishwa na tukio lilitokea march 25 katika club ya usiku ya Atlanta....wakati Gucci anadaiwa kumpiga na chupa kichwani mmoja wa watu waliokuwepo ndani ya Club hiyo, na kusababisha tafash kubwa
RIPOTI YA POLISI KUHUSU KILICHOSABABISHA KIFO CHA MSANII CHRIS KELLY
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ , Ripoti ya Polisi kuhusu kilichobababisha kifo cha msanii Chris Kelly ambaye alikuwa member wa kundi la Kriss Kross inasema , marehemu alitumia mchanganyiko wa madawa ya kulevya aina ya 'Cocaine' na 'Heroine'.
"Chris Kelly had been using a combination of cocaine and heroin the night before his death, this according to the police report obtained by TMZ.
According to the report, cops responded to Kelly's home Wednesday afternoon and found the 34-year-old lying on the living room couch. Both paramedics who arrived to the scene said Kelly was unresponsive and had "no life signs." They attempted to revive Kelly, to no avail. Cops then spoke with Kelly's friend, Donna, who told officers ... the night before Kelly's medical emergency, he had taken a mixture of heroin and cocaine. The friend also told police that Kelly had done"
LIST YA WASANII WATAKAOSHIRIKI KWENYE SHOO YA MIAKA 13 YA LADY JAYDEE
List ya wasanii ambao watamshindikiza Lady Jaydee aka Komando aka Anaconda kwenye sherehe za miaka 13 na uzinduzi wa Album yake mpya ya 6 'Nothing but the Truth'.Kwa mujibu wa ukurasa wa facebook wa Lady Jaydee wasanii ambao wataperform ni TID, Hamza Kalala, Barnaba, Grace Matata,Linah,Profesa Jay na Matonya
Itakuwa ni tarehe 31 May kama unavyoona kwenye Posters pande za Nyumbani Lounge.Tickets za show ya miaka 13 ya LADY JAYDEE za VIP, 50,000/= zitaanza kuuzwa tarehe 10 May 2013.
Katika ticket hii utapata Dinner, Wine zitakuwepo mezani pamoja na free CD Album mpya.
Meza ziko 50 tu zenye viti 10@. Wahi nafasi yako mapema.
Ticket zingine za 20,000/= zitauzwa mlangoni siku ya show ambayo ni tarehe 31 May 2013
Na utapata CD Album ya Nothing But The Truth Bureeeee.
#Anacondastyle itahusika
Kila la Kheriiii Lady Jadee aka Komando aka Anaconda.
WYCLEF AZUNGUKA MITAA YA NYC NA GITAA LENYE UMBO LA SILAHA AINA YA AK-47
Wyclef Jean anasema yeye anataka kubadili silaha kuwa muziki ... hivyo ametengeneza gitaa lenye umbo kama AK-47 ASSAULT RIFLE ... na kuzunguka nayo katika mitaa ya NYC.
idea inaonekana kuwa nzuri, lakini kuzurura na kuinyesha kwa watu kitu kinachofanana na Silaha katikati ya mitaa ???
hoja inaonekana kuwa ya sio kabisa... hasa kwa kuzingatia utekelezaji wa sheria katika miji iko juu sana kwa tagadhari tangu maafisa kugundua wale ndugu wa kigaidi walikuwa wakiwalenga New York
Subscribe to:
Posts (Atom)















