Thursday, May 31, 2012

STARS YAWAFUATA AKINA DROGBA

              
        
http://kandanda.galacha.com/wp-content/uploads/2012/05/Capture.png

WAKATI kikosi cha timu ya Taifa 'Taifa Stars' kikiondoka alfajir ya leo kuelekea nchini Ivory Coast, wachezaji nyota wa  klabu ya Simba, beki Said Nassor 'Chollo' na kiungo Haruna Moshi 'Boban' wameondolewa kwenye kikosi hicho.
Wachezaji hao wameondolewa kutokana na kuwa majeruhi hivyo kufanya msafara huo kuwa na wachezaji 21.
Awali nyota wawili wa kikosi hicho Nurdin Bakari wa Yanga na Thomas Ulimwengu anayekipiga klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walipata majeruhi kabla ya hali zao kuimarika.Hata hivyo nyota hao pia wameachwa ili kuendelea kujinoa taratibu na wataungana na wenzao watakaorejea juni 5.
Stars na  Ivory Coast zitamenyana juni 2 katijka mechi ya  mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia itakayopigwa dimba la Felix Houphouet-Boigny jijini Abijan kuanzia saa 11 kamili kwa saa za Ivory Coast.
Mchezo huo utachezeshwa na Mwamuzi atakuwa Slim Jedidi wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Bechir Hassani, wote kutoka Tunisia. Mwamuzi msaidizi namba mbili ni Sherif Hassan kutoka Misri. Mwamuzi wa akiba ni Youssef Essrayri pia kutoka Tunisia.
Mtathmini wa waamuzi ni Rachid Medjiba kutoka Algeria wakati Kamishna wa pambano hilo atakuwa Saleh Issa Mahamat kutoka Chad.

 Wachezaji waliokwenda Ivory Coast ni pamoja na  Nahodha Juma Kaseja, Nahodha msaidizi Aggrey Morris, Mwadini Ally, Deogratius Munishi, Amir Maftah, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Waziri Salum, Shomari Kapombe, Juma Nyoso, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Salum Abubakar, Shabani Nditi, Edward Christopher, Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Mbwana Samata, Ramadhan Singano, Simon Msuva na John Bocco.

OKWI KUUZWA BILIONI 2

HOFU ya kumpoteza mchezaji wake wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi, imeifanya klabu ya Simba kumweka sokoni kwa dau la sh bil. 2.

Simba itakuwa imeweka dau hilo kama wigo wa kumzuia kuondoka, kwani hakuna timu itakayoweza kutoa kiasi hicho cha fedha.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema mbali ya kiasi hicho, kuna masharti mengine kwa klabu itakayomtaka Okwi.

Kamwaga alisema sharti jingine ni kuweka bayana mshahara wa nyota huyo ili kumwepusha na dhiki ya maisha. Sharti jingine, ni muhimu kwa klabu husika kuwa na uongozi imara ili nyota huyo asipate dhiki inayoweza kusababishwa na matatizo ya kiuongozi.

“Hayo ndiyo masharti kwa timu ambayo itakuwa inamhitaji Okwi, hatutakuwa kikwazo kwa klabu itakayokidhi vigezo hivi muhimu kwa maslahi ya mchezaji,” alisema Kamwaga.

Kamwaga alisema, wameweka bayana hilo kutokana na Okwi kuwindwa na klabu nyingi za ndani na nje ya nchi, ikiwemo Austria.

Alisema, kupitia mtandao klabu moja ya huko imeonesha kumtaka Okwi, hivyo wamewapatia masharti hayo muhimu kama kweli wanamtaka.

Kamwaga alisema, kama kutakuwa na klabu itakayoridhia masharti hayo iwe ndani au nje ya nchi, wao Simba hawatakuwa kikwazo.

CHOVE KURUDI KIYOVU YA RWANDA

 Jackson Chove

ALIYEKUWA kipa namba moja wa timu ya Moro United, Jakson Chove amesema kuwa kama mambo yatakwenda vizuri yupo tayari kucheza kwenye timu yake ya zamani ya Kiyovu ya Rwanda.

Jakson Chove ambaye aliwahi kuichezea timu hiyo mwaka 2010, alisema licha ya kuwa bado hajasaini mkataba na timu hiyo, lakini timu imeonyesha inamuhitaji.

Alisema Kiyovu ni timu ambayo aliwahi kuichezea na kama watampa mkataba hawezi kuukataa kwa sababu hivi sasa hana timu baada ya timu ya Moro United kushuka daraja.

"Kuna baadhi ya jamaa zangu ambao wanachezea Kiyovu na niliwahi kucheza nao wameniambia kuwa nimetajwa miongoni mwa wachezaji watakaosajiliwa baada ya ligi ya huko kuisha hivyo nasikilizia na
nipo tayari kwa hilo," alisema Chove.

Aidha Chove alisisitiza kuwa pamoja na kusikilizia kutoka katika timu hiyo haina maana kuwa timu inayomuhitaji hapa nyumbani hataingia nao mkataba ili mradi uwe ni ndani ya makubaliano.

VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA MKOANI MTWARA WATAKIWA KUKAGULIWA BAADA YA MSIMU WA KOROSHO KUMALIZIKA


afisa ushirika wa halmashauri ya wilaya ya mtwara mohamed mpenye amewataka viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika kuhakikisha wanakaguliwa vitabu vyao mara baada ya msimuwa korosho  kumalizika.
ameyasema hayo hii leo wakatika akifunga warsha ya viongozi hao, ya siku mbili iliyofanyika katika chuo cha ushirika mjini hapa .
mpenye amesema kuwa sikuzote chama kisicho taka matatizo huwa kina utaratibu wa kufunga hesabu zao na kukaguliwa na maafisa ushirika ilikuepusha migogoro na wanachama wao.
aidha imeelezwa kuwa, ni wajibu wa viongozi kuwakumbusha wanachamasa wao kulipia ada na kuongeza wanachama katika vyama vyao kwani mtaji wa vyama ni wanachama kuwa wengi ndani ya chama cha msingi.
kwa upande wake afisa mwandamizi wa ushirika wilaya, ndugu mohamed amewataka viongozi hao kuhakikisha msimu huu wanaangalia pia mazao mengine na kuyaingiza katika mfumo wa stakabadhi ghalani ili kumwezesha mkulima kulithaminisha zao lake kwa kupata bei nzuri ya serikali na kuachana na bei za walanguzi.

WAANDISHI WA HABARI MTWARA KUKIPIGA NA RAS MTWARA JUMAMOSI HII





kikosi cha waandishib wa habari mkoa wa mtwara



TIMU ya waandishi wa habari moani mtwara jumamosi hii inaingia dimbani kukipiga na timu ya soka ya Ras mkoa wa mtwara

Akizungumzia mchezo huo nahodha wa timu ya waandishi wa habari Emanuel msingwa amesema kuwa wamejiandaa vya kutosha kuweza kuibuka na ushindi katika mchezo huo siku ya jumamosi

Kwa upande wake Katibu msaidizi wa Timu ya Ras mkoa wa mtwara Ismail Makumbuli amesema kuwa timu yao iko katika hali nzuri na inaendelea na mazoezi tayari kuikabili timu ya waandishi wa habari siku ya jumamosi katika kiwanja cha chuo cha ualimu TTTC

Ikumbukwe hapo awali timu hii ya Ras iliinyuka Timu ya Waandishi wa habari goli 3-1 na Mchezo wa jumamosi hii unatarajiwa kuwa mkali kwa timu zote 2
Kwa upande wao mashabiki wa soka Mkoani Mtwara wamesema kuwa wanasubiri kwa hamu mtanange huo ambao umekuwa gumzo sasa mitaani mkoani hapa

WAZIRI KUU KUMUWAKILISHA RAIS KIKWETE MKUTANO WA SADC





WAZIRI MKUU Mizengo Pinda anatarajia kuhudhuria kikao cha Wakuu wa Nchi za
Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) nchini Angola.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, Waziri Mkuu Pinda anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Rais
Jakaya Kikwete ambaye anahudhuria mkutano wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB) jijini Arusha.
Waziri Mkuu atahudhuria kikao cha TROIKA
ambacho kinajumuisha Wakuu wa Nchi kitakachofanyika Ikulu ya nchi hiyo na
usiku atashiriki hafla maalum iliyoandaliwa kwa viongozi wakuu wa nchi za
SADC.

TANZANIA YASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO YA PAMOJA NA IRAN

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Makamu wa Rais wa Kwanza wa Iran, Mhe. Mohammad Reza Rahimi, wakisainiana mkataba wa makubaliano ya pamoja ya masuala mbalimbali yanayohusu uhusiano wa nchi hizo mbili,  wakati wa hafla hiyo fupi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam jana Mei 30, 2012. Picha na Amour Nassor-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Makamu wa Rais wa Kwanza wa Iran, Mhe. Mohammad Reza Rahimi, wakibadilishana mkataba baada ya kusainiana mkataba huo wa makubaliano ya pamoja ya masuala mbalimbali yanayohusu uhusiano wa nchi hizo mbili,  wakati wa hafla hiyo fupi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam jana Mei 30, 2012. Picha na Amour Nassor-OMR

NCCR MAGEUZI YAPATA WANACHAMA WAPYA MTWARA






Katika ziara inayoendelea mkoani Mtwara, hadi sasa wanachama wapya 2,517 wamejiunga na chama katika Jimbo la Mtwara Mjini.
Takwimu hizi ni kwa mujibu wa Mjumbe wa Halmashauri ya chama Ndg. Danda Juju, ambaye alizitoa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Mtwara.
Alisema kuwa, idadi hiyo imepatikana kutokana na jitihada za uhamasishaji ambazo zimekuwa zikifanywa na viongozi wa kitaifa na wa jimbo hilo.
“Chama kinazidi kushika kasi, tumekuwa tukipata wanachama wapya kila kunapokucha kwa sababu wananchi wametambua kuwa NCCR-Mageuzi ndicho chama makini kitakachoweza kuwakomboa.
Tumepata wanachama wengi na tunaamini idadi itazidi kuongezeka kwa sababu wananchi wa Mtwara wameshaamka, na wanataka mageuzi hasa kutokana na kukichoka chama tawala,”
Kwa mujibu wa Juju ambaye pia ni Msaidizi Mkuu wa Mwenyekiti wa chama hicho Bw. James Mbatia;  baadhi ya wanachama wanaojiunga na chama wanatoka vyama vingine vya siasa.


Wakati huohuoChama cha Nccr Mageuzi kinatarajia kufanya mkutano wa hadhara leio katika uwanja wa lindi mgahawa mtwara mjini
Akizungumza na Swiraty blog mwenyekiti wa chama cha Nccr Mageuzi jimbo la Mtwara ndugu Uledi Hasani amesema kuwa baada ya kuzunguka katika ziara kubwa iliyohusisha wilaya za mtwara leo wanamalizia ziara hiyo kwa mkutano huo mkubwa hadhara.
Amesema kuwa katika mkutano huo ambao utahudhuliwa pia na mjumbe wa halmshauri kuu taifa wa chama hicho Ndugu Msabaha ambaye ndie anatarajiwa kuwa mgeni rasmi hii leo
Mkutano huo unatarajia kuanza saa nane mchana hadi saa kumi na mbili jioni na imeelezwa kuwa miongoni mwa mambo yanayotarajiwa kuzungumzwa hii leo katika mkutano huo ni pamoja na halia ya umaskini wa mtwara na vitega uchumi vilivyopo

CHADEMA YAENDELEA KUTEKA MTWARA






chama cha demokrasia na maendeleo chadema kimevuna jumala ya wanachama 200 katika kijiji cha tangazo katika halmashauri ya wilaya mtwara vijijini
Chadema na viongozi wake wakuu wa nchi wapo katika mkoa wa mtwara kwa ziara ya siku 17 ambapo wanatazunguka katika wilaya zote za mtwara na hatimaye kuingia mkoani lindi kwa ziara ya kichama kama hii
Chadema imekuwa ikipata mapokezi makubwa tangu ilipowasili katika mkoa wa mtwara wiki iliyopita na kuhutubia wananchi wa mtwara katika uwanja wa mashujaa mkoani hapa
Baada ya ziara hiyo ya wilaya ya mtwara vijijini jana ambapo wamezunguka jumla ya kata 20 leo uongozi wa chama hico utaingia wilayani tandahimba tayari kwa ziara ya kichama wilayani humo

Wednesday, May 30, 2012

DIAMOND KUTUMBUIZA KATIKA SHINDANO LA MISS CHANG'OMBE

DIAMOND KUTUMBUIZA KATIKA SHINDANO LA MISS CHANG'OMBE

Baada ya  kufanya  show ya Big Brother  Afrika Kusini MSANII Abdul Naasib ‘Diamond’ni mmoja wa wasanii watakaotoa burudani kamambe kulipamba  shindano la Redd’s Miss Chang’ombe 2012 shindano litakalofanyika Juni 9 mwaka huu  katika ukumbi wa Quality Centre barabara ya Nyerere Jijini Dar es Slaam.
Wengine watakaopamba shindano hilo la aina yake ni  kundi la Original Commedy akina Joti na bendi ya mapacha watatu ambayo kwa sasa imekuwa moja ya bendi zinayokonga  nyoyo za mashabiki wengi wa muziki hapa nchini.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam msemaji wa Kampuni ya King Promoters  ambao ndiyo waandaaji wa shindano hilo Martin Mauya ameaema kuwa kwa sasa warembo hao wameendelea kufanya mazoezi katika viwanja vya klabu ya TCC Chang’ombe Jijini Dar es Salaam.
Shindano hilo linatarajia kushirikisha warembo bomba 14 watakaopanda jukwaani kuchuana vikali kumpata mrembo wa mkoa huo wa kimashindano wa Chang’ombe huku baadhi ya wadau wa fani hiyo ya urembo nchini wakitabiri kuwa mrembo wa Tanzania mara hii atatokea katika mkoa huo wa kimashindano.
Mauya  amewataja warembo wanaotarajia kupanda jukwaani ni Elizabeth Mushi, Restituta Faustine, Miriam Ntakisivya, Flora Kazungu, Flora Robert,  Like Abraham, Clara Diu, Margareth Gerald, Jesca Haule, Deborah Nyakisinda, Suzan Paul, Wensley Matius, Zulfa Bundara na Catherine Masumbigana.
‘Kwa sasa warembo hao wanafanya mazoezi na kurudi nyumbani lakini Juni 3 warembo hao wataingia rasmi kambini katika Hoteli moja kubwa Jijini kabla ya kuapnda hiyo Juni 9’ alisema Mauya.
Shindano hilo limedhaminiwa na REDD’S ORIGINAL, NEXUS CONSULTING AGENCY, DODOMA WINE, CXC AFRIKA, PAPAZII INTERTAINMENT, KITWE GENERAL TRADERS,CHERISH, BEN EXPEDITION, SCREEN MASTERS, ARDHI PLAN LIMITED.

TAIFA STARS KWENDA ABDIJAN KESHO ALFAJIRI

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjXJQXFpwNX9rx4iCmmAWFoJ_woi9YnkQgPCpEHReDfjzbsG9ecjBmCNObUKnFXxegL-FCh1Ld8jufCtj0Jog1UYEIHKLQx7eV7NKy3DPSmtU8NRQfA2r-x3YSwfnyogfvRoyoNozJGsizn/s400/STARS.JPG

                      TAIFA STARS KWENDA ABDIJAN KESHO ALFAJIRI

Kikosi cha wachezaji 23 na viongozi tisa kinatarajia kuondoka kesho (Mei 31 mwaka huu) saa 11.10 alfajiri kwa ndege ya Kenya Airways kwenda Abidjan, Ivory Coast kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia itakayochezwa Juni 2 mwaka huu.
Wachezaji wanaoondoka ni nahodha Juma Kaseja, nahodha msaidizi Aggrey Morris, Mwadini Ally, Deogratius Munishi, Nassor Masoud Cholo, Amir Maftah, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Waziri Salum, Shomari Kapombe na Juma Nyoso.
Wengine ni Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Salum Abubakar, Shabani Nditi, Edward Christopher, Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Mbwana Samata, Ramadhan Singano, Simon Msuva, Haruna Moshi na John Bocco.
Wachezaji waliobaki kutokana na kuwa majeruhi ni mshambuliaji Thomas Ulimwengu anayecheza timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na kiungo wa Yanga, Nurdin Bakari.
Viongozi wanaofuatana na timu hiyo ni Kocha Mkuu Kim Poulsen, Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Mukebezi (Meneja wa timu), Juma Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Physiotherapist) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
Msafara huo unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Crescentius Magori wakati naibu kiongozi wa msafara ni Makamu wa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) Haji Ameir Haji.
Timu hiyo inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeagwa leo (Mei 30 mwaka huu) na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala ambaye aliwataka wachezaji hao kwenda kuiwakilisha vizuri Tanzania kwenye mechi hiyo.
Hafla hiyo ya kukabidhi Bendera ya Taifa pia ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi, Rais wa TFF, Leodegar Tenga na Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe.
Mechi itachezwa kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abijan kuanzia saa 11 kamili kwa saa za Ivory Coast.
Mwamuzi atakuwa Slim Jedidi wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Bechir Hassani, wote kutoka Tunisia. Mwamuzi msaidizi namba mbili ni Sherif Hassan kutoka Misri. Mwamuzi wa akiba ni Youssef Essrayri pia kutoka Tunisia.
Mtathmini wa waamuzi ni Rachid Medjiba kutoka Algeria wakati Kamishna wa pambano hilo atakuwa Saleh Issa Mahamat kutoka Chad.
Stars itarajea nyumbani Juni 5 mwaka huu saa 1.40 asubuhi na kuingia moja kwa moja kambini kujiandaa kwa mechi dhidi ya Gambia itakayofanyika Juni 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

NEW VIDEO (SHETTA FT DIAMOND--NIDANGANYE)


MTOTO MWENYE MIGUU SITA

MTOTO ALIYEZALIWA NA MIGUU SITA



MTOTO mmoja amezaliwa jijini Karachi nchini Pakistan akiwa na miguu sita na amefanyiwa upasuaji kuondoa iliyozidi.
Jopo la madaktari waliomfanyia upasuaji huo Alhamisili iliyopita kwenye taasisi iitwayo National Institute of Child Heath (NICH), jijini Karachi wamesema upasuaji ulikwenda vizuri kama walivyopanga.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Dk. Jamal Raza ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa NICH, alisema miguu mingine iliondolewa kwa operesheni na hali hiyo hutokea mara chache sana.