afisa
ushirika wa halmashauri ya wilaya ya mtwara mohamed mpenye amewataka viongozi
wa vyama vya msingi vya ushirika kuhakikisha wanakaguliwa vitabu vyao mara
baada ya msimuwa korosho kumalizika.
ameyasema
hayo hii leo wakatika akifunga warsha ya viongozi hao, ya siku mbili
iliyofanyika katika chuo cha ushirika mjini hapa .
mpenye
amesema kuwa sikuzote chama kisicho taka matatizo huwa kina utaratibu wa
kufunga hesabu zao na kukaguliwa na maafisa ushirika ilikuepusha migogoro na
wanachama wao.
aidha
imeelezwa kuwa, ni wajibu wa viongozi kuwakumbusha wanachamasa wao kulipia ada na
kuongeza wanachama katika vyama vyao kwani mtaji wa vyama ni wanachama kuwa wengi
ndani ya chama cha msingi.
kwa
upande wake afisa mwandamizi wa ushirika wilaya, ndugu mohamed amewataka viongozi
hao kuhakikisha msimu huu wanaangalia pia mazao mengine na kuyaingiza katika
mfumo wa stakabadhi ghalani ili kumwezesha mkulima kulithaminisha zao lake kwa
kupata bei nzuri ya serikali na kuachana na bei za walanguzi.