WAKATI kikosi cha
timu ya Taifa 'Taifa Stars' kikiondoka alfajir ya leo kuelekea nchini Ivory
Coast, wachezaji nyota wa klabu ya Simba, beki Said Nassor 'Chollo' na
kiungo Haruna Moshi 'Boban' wameondolewa kwenye kikosi hicho.
Wachezaji hao
wameondolewa kutokana na kuwa majeruhi hivyo kufanya msafara huo kuwa na
wachezaji 21.
Awali nyota wawili wa
kikosi hicho Nurdin Bakari wa Yanga na Thomas Ulimwengu anayekipiga klabu ya TP
Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walipata majeruhi kabla ya hali zao
kuimarika.Hata hivyo nyota hao pia wameachwa ili kuendelea kujinoa taratibu na
wataungana na wenzao watakaorejea juni 5.
Stars na Ivory
Coast zitamenyana juni 2 katijka mechi ya mechi ya mchujo ya Kombe la
Dunia itakayopigwa dimba la Felix Houphouet-Boigny jijini Abijan kuanzia
saa 11 kamili kwa saa za Ivory Coast.
Mchezo huo
utachezeshwa na Mwamuzi atakuwa Slim Jedidi wakati mwamuzi msaidizi namba moja
ni Bechir Hassani, wote kutoka Tunisia. Mwamuzi msaidizi namba mbili ni Sherif
Hassan kutoka Misri. Mwamuzi wa akiba ni Youssef Essrayri pia kutoka Tunisia.
Mtathmini wa waamuzi
ni Rachid Medjiba kutoka Algeria wakati Kamishna wa pambano hilo atakuwa Saleh
Issa Mahamat kutoka Chad.
Wachezaji
waliokwenda Ivory Coast ni pamoja na Nahodha Juma Kaseja, Nahodha
msaidizi Aggrey Morris, Mwadini Ally, Deogratius Munishi, Amir Maftah, Erasto
Nyoni, Kelvin Yondani, Waziri Salum, Shomari Kapombe, Juma Nyoso, Jonas Mkude,
Mwinyi Kazimoto, Salum Abubakar, Shabani Nditi, Edward Christopher, Mrisho
Ngasa, Frank Domayo, Mbwana Samata, Ramadhan Singano, Simon Msuva na John
Bocco.