TAIFA STARS KWENDA ABDIJAN KESHO ALFAJIRI
Kikosi
cha wachezaji 23 na viongozi tisa kinatarajia kuondoka kesho (Mei 31
mwaka huu) saa 11.10 alfajiri kwa ndege ya Kenya Airways kwenda Abidjan,
Ivory Coast kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia
itakayochezwa Juni 2 mwaka huu.
Wachezaji
wanaoondoka ni nahodha Juma Kaseja, nahodha msaidizi Aggrey Morris,
Mwadini Ally, Deogratius Munishi, Nassor Masoud Cholo, Amir Maftah,
Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Waziri Salum, Shomari Kapombe na Juma
Nyoso.
Wengine
ni Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Salum Abubakar, Shabani Nditi, Edward
Christopher, Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Mbwana Samata, Ramadhan
Singano, Simon Msuva, Haruna Moshi na John Bocco.
Wachezaji
waliobaki kutokana na kuwa majeruhi ni mshambuliaji Thomas Ulimwengu
anayecheza timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na
kiungo wa Yanga, Nurdin Bakari.
Viongozi
wanaofuatana na timu hiyo ni Kocha Mkuu Kim Poulsen, Sylvester Marsh
(Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Mukebezi
(Meneja wa timu), Juma Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda
(Physiotherapist) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
Msafara
huo unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) Crescentius Magori wakati naibu kiongozi wa
msafara ni Makamu wa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA)
Haji Ameir Haji.
Timu
hiyo inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeagwa leo (Mei 30
mwaka huu) na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos
Makala ambaye aliwataka wachezaji hao kwenda kuiwakilisha vizuri
Tanzania kwenye mechi hiyo.
Hafla
hiyo ya kukabidhi Bendera ya Taifa pia ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa
Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi, Rais wa TFF, Leodegar
Tenga na Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe.
Mechi itachezwa kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abijan kuanzia saa 11 kamili kwa saa za Ivory Coast.
Mwamuzi
atakuwa Slim Jedidi wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Bechir
Hassani, wote kutoka Tunisia. Mwamuzi msaidizi namba mbili ni Sherif
Hassan kutoka Misri. Mwamuzi wa akiba ni Youssef Essrayri pia kutoka
Tunisia.
Mtathmini wa waamuzi ni Rachid Medjiba kutoka Algeria wakati Kamishna wa pambano hilo atakuwa Saleh Issa Mahamat kutoka Chad.
Stars
itarajea nyumbani Juni 5 mwaka huu saa 1.40 asubuhi na kuingia moja kwa
moja kambini kujiandaa kwa mechi dhidi ya Gambia itakayofanyika Juni 10
mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.