Wednesday, July 11, 2012

OKWI ATUA AUSTRIA KUFANYA MAJARIBIO

Okwi

MSHAMBULIAJI wa Simba, Emmanuel Okwi, ameikosesha klabu yake Sh. Bilioni 2 kwa kukataa kujiunga na klabu ya Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini, kwa kutimikia nchini Austria badala ya Italia kama ilivyodai ana ofa ya kufanya majaribio na klabu ya Parma.

Okwi hivi sasa yuko Austria anafanya majaribio katika klabu ambayo iko tayari kutoa Euro 600,000 akifuzu na si Italia kama ilivyoelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ wiki mbili zilizopita.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na SWIRATY BLOG umegundua Okwi aliondoka mwishoni mwa wiki Uganda kwenda Austria na hadi mwishoni mwa wiki hii tayari itajulikana kama amefuzu au la.

Awali Olando Pirates ya Afrika Kusini ilimuomba Okwi akafanye majaribio huko kama angefuzu wangemsajili dau la dola 550,000 kabla ya kuibuka kwa taarifa za kutakiwa Italia na klabu ya Parma.

Hata hivyo, Simba SC ilisema imeshindwa kumshawishi Okwi kwenda kucheza Afrika Kusini kwa kuwa mwenyewe anataka kucheza Ulaya tu. Wakala aliyeiunganisha Simba na Pirates akawasilisha ofa nyingine kutoka Mamelodi, ambayo ni Euro 600,000 na kupanda hadi Sh. Bilioni 2, lakini bado mabingwa hao wa Tanzania, walishindwa kumshawishi Okwi kwenda Ligi Kuu ya Afika Kusini (PSL).

Akiwa Austria, bado Sundown wanamfuatilia Okwi na leo ndio wameambiwa Okwi yupo nchi hiyo ya Ulaya.

Wasiwasi uliopo ni kwamba Okwi anaweza kukwama Austria na kuigeukia ofa ya Mamelodi wakati dirisha la usajili limefungwa, au Mamelodi tayari imepata mchezaji mwingine wa aina yake na kufunga milango. 

NAFTALI DAVID AKIWA MOMBASA

Beki wa Bandari ya Mombasa, David Naftali akiwa amejipumzisha nyumbani kwake mjini Mombasa, baada ya mazoezi ya asubuhi ya jana. Picha kwa hisani ya Naftali mwenyewe.

SAINTEF AANZA KWA NEEMA YANGA SC, MASHABIKI WAPIGWA CHANGA LA MACHO

KOCHA mpya wa klabu ya Yanga Tom Sentief ameanza vema na klabu hiyo baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Ruvu.
Timu hizo zilikuwa zikuikwaana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki ambapo mabao ya Yanga yalipachinkwa na Nadir Haroub 'Cannavaro' na Hamis Kiiza.
Kutokana na matokeo hayo, Saintef amewapongeza wachezaji wake na kusema kasoro ndogo alizoziona atazifanyia marekebisho kabla ya kuanza kwa michuano ya Kagame ambapo timu yake inashiriki kama bingwa Mtetezi.
Aidha, Mbelgiji huyo pia amekimwagia sifa kikosi cha JKT Ruvu na kusema kwamba pamoja na kufungwa kilionyesha kandanda safi. 
Katika hatua nyingine, mashabiki wa Yanga wamepigwa na butwaa baada ya kutoonekana mkwa wachezaji wapya wa kimataifa kama ilivyotangazwa jana na msemaji wa Yanga Louis Sendeu.
Sendeu aliwaambia waandishi wa habari kwamba katika mchezo wa leo Yanga ingetambulisha rasmi nyota wake waili wa kimataifa ambao wangeziba pengo la Mghana Kenneth Asamoah na Mzambia Davies Mwape ambao walitupiwa virago.

MISS LINDI 2012 APATIKANA

MISS Lindi 2012  irene veda,katika picha ya pamoja na washinmdi wengine watakaowakilisha mkoa huo katika Kanda ya Nyanda za juu Kusini, kutoka kulia ni mshindi wa pili Stela Baltazar, Dorena Athuma aliyeshika nafasi ya tatu na Stela Ngala aliyekuwa wa nne. 

Miss Lindi 2012, Irene Veda

FID Q APAGAWISHA WAJANJA WA VODACO MTWARAS VODACOM WAJANJA MUSIC TOUR IN MTWARA


Hundreds of Wajanja Music Tour fans in Mtwara were thrilled on Sunday evening by music star  Farid Kubanda, popularly referred to as Fid Q, forcing him to stay on stage even after his performance had ended.
The exited fans screamed and cheered Ngosha!Ngosha!Ngosha!as Fid Q took to the stage a few minutes after fellow star, Diamond, finished his show, and gave security guards managing the event a hard time managing the fans who later pushed his car in excitement not wanting him to leave.
Other artists present during the Mtwara music tour include Shetaa,Joh Makini, Ney wa Mitego and Mabeste.
While addressing the media, Matina Nkurlu, Vodacom Tanzania Public Relations Manager, said that the Wajanja Tour proceeds to Tanga this coming Sunday, at Mkwakwani stadium.
“Wajanja tour is set for “waja leo waondoka leo” in Tanga. The show really rocked Mtwara, so fans in Tanga better get ready for great entertainment from the various artists this Sunday,” said Nkurlu.

Wahariri Katika Mafunzo Ya Sensa Mjini Dodoma




Meza kuu- Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Amos Makala(wa pili kushoto) , Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr. Albina Chuwa (wa pili kulia) , Mkuu wa Chuo cha Mipango Dodoma Constantine Lifurilo(kushoto) na Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi Moris Uyuke(kulia) wakifuatia zoezi la ufunguaji wa semina ya siku tatu kwa wahariri na waandishi waandamizi kuhusu sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 inayotarajia kufanyika usiku wa kuamkia tarehe 26 mwezi Okotba nchini kote. Mafunzo hayo yalifunguliwa jana (leo) katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere kwenye Chuo cha Mipango _Dodoma


 wahariri na waandishi wa habari--Wahariri na waandishi waandamizi wakifuatilia mafunzo wakati wa semina ya siku tatu kwa wahariri na waandishi waandamizi kuhusu sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 inayotarajia kufanyika usiku wa kuamkia tarehe 26 mwezi Okotba nchini kote. Mafunzo hayo yalifunguliwa jana (leo) katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere kwenye Chuo cha Mipango _Dodoma na Naibu Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Amos Makala(hayupo pichani)




 Pamoja - Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Amos Makala(mwenye tai kwa walio kaa) akiwa katika picha ya pamoja na wahariri na waandishi waandamizi mara ya kumalizi kwa zoezi la ufunguzi wa semina ya siku tatu kwa wahariri na waandishi waandamizi kuhusu sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 inayotarajia kufanyika usiku wa kuamkia tarehe 26 mwezi Okotba nchini kote. Mafunzo hayo yalifunguliwa jana (leo) katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere kwenye Chuo cha Mipango _Dodoma

              Picha na Tiganya vincent- MAELEZO_ DOPDOMA.

MWANZA YAING’OA KINONDONI COPA COCA-COLA 2012

 

Mwanza imekata tiketi ya kucheza nusu fainali ya michuano ya Copa Coca-Cola baada ya leo (Julai 11 mwaka huu) kuitoa Kinondoni kwa penalti 3-1 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.

Hadi dakika 90 za mechi hiyo ya robo fainali zinamalizika timu hizo zilikuwa hazijafunga, hivyo kulazimika kuingia kwenye mikwaju ya penalti ili kupata mshindi ambaye atacheza nusu fainali keshokutwa (Julai 13 mwaka huu) dhidi ya Temeke.

Walioifungia Mwanza katika penalti ni Christopher Maghinwa, Steven Lubela na Juma Masunga. Penalti ya Kinondoni ilitiwa wavuni na Shabani Nyenje. Waliokosa kwa Kinondoni ni Miza Abdallah, John Komba na Juma Masunga.

Nusu fainali ya pili itakuwa kati ya Morogoro na mshindi wa mechi ya robo fainali kati ya Dodoma na Tanga itakayochezwa leo jioni (Julai 11 mwaka huu) kwenye uwanja huo huo

WAAMUZI KAGAME KUNOLEWA JULAI 12


Mtihani wa timamu wa mwili (fitness test) kwa waamuzi walioteuliwa kuchezesha michuano ya Kombe la Kagame inayoanza Jumamosi (Julai 14 mwaka huu) utafanyika kesho (Julai 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Waamuzi 15 walioteuliwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuchezesha michuano hiyo. Waamuzi hao wanawasili leo jijini Dar es Salaam. 

Kwa upande wa waamuzi wa kati (centre referees) ni Anthony Ogwayo (Kenya), Dennis Batte (Uganda), Israel Mujuni (Tanzania Bara), Issa Kagabo (Rwanda), Thierry Nkurunziza (Burundi), Farah Aden Ali (Djibouti) na Waziri Sheha (Zanzibar).

Waamuzi wasaidizi (assistant referees) ni Elias Kuloba (Kenya), Peter Sabatia (Kenya), Musa Balikoowa (Uganda), Hamis Changwalu (Tanzania Bara), Jesse Erasmo (Tanzania Bara), Simba Honore (Rwanda), Abdulahi Mahamoud (Djibouti) na Josephat Bulali (Zanzibar)