Mwanza
imekata tiketi ya kucheza nusu fainali ya michuano ya Copa Coca-Cola
baada ya leo (Julai 11 mwaka huu) kuitoa Kinondoni kwa penalti 3-1
katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Hadi
dakika 90 za mechi hiyo ya robo fainali zinamalizika timu hizo zilikuwa
hazijafunga, hivyo kulazimika kuingia kwenye mikwaju ya penalti ili
kupata mshindi ambaye atacheza nusu fainali keshokutwa (Julai 13 mwaka
huu) dhidi ya Temeke.
Walioifungia
Mwanza katika penalti ni Christopher Maghinwa, Steven Lubela na Juma
Masunga. Penalti ya Kinondoni ilitiwa wavuni na Shabani Nyenje.
Waliokosa kwa Kinondoni ni Miza Abdallah, John Komba na Juma Masunga.
Nusu
fainali ya pili itakuwa kati ya Morogoro na mshindi wa mechi ya robo
fainali kati ya Dodoma na Tanga itakayochezwa leo jioni (Julai 11 mwaka
huu) kwenye uwanja huo huo