|
Okwi |
MSHAMBULIAJI wa Simba, Emmanuel Okwi, ameikosesha klabu yake
Sh. Bilioni 2 kwa kukataa kujiunga na klabu ya Mamelodi Sundown ya Afrika
Kusini, kwa kutimikia nchini Austria badala ya Italia kama ilivyodai ana ofa ya
kufanya majaribio na klabu ya Parma.
Okwi hivi sasa yuko Austria anafanya majaribio katika klabu
ambayo iko tayari kutoa Euro 600,000 akifuzu na si Italia kama ilivyoelezwa na
Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ wiki mbili zilizopita.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na SWIRATY BLOG umegundua Okwi
aliondoka mwishoni mwa wiki Uganda kwenda Austria na hadi mwishoni mwa wiki hii
tayari itajulikana kama amefuzu au la.
Awali Olando Pirates ya Afrika Kusini ilimuomba Okwi akafanye
majaribio huko kama angefuzu wangemsajili dau la dola 550,000 kabla ya kuibuka
kwa taarifa za kutakiwa Italia na klabu ya Parma.
Hata hivyo, Simba SC ilisema imeshindwa kumshawishi Okwi
kwenda kucheza Afrika Kusini kwa kuwa mwenyewe anataka kucheza Ulaya tu. Wakala
aliyeiunganisha Simba na Pirates akawasilisha ofa nyingine kutoka Mamelodi,
ambayo ni Euro 600,000 na kupanda hadi Sh. Bilioni 2, lakini bado mabingwa hao
wa Tanzania, walishindwa kumshawishi Okwi kwenda Ligi Kuu ya Afika Kusini (PSL).
Akiwa Austria, bado Sundown wanamfuatilia Okwi na leo ndio
wameambiwa Okwi yupo nchi hiyo ya Ulaya.
Wasiwasi uliopo ni kwamba Okwi anaweza kukwama Austria na
kuigeukia ofa ya Mamelodi wakati dirisha la usajili limefungwa, au Mamelodi
tayari imepata mchezaji mwingine wa aina yake na kufunga milango.