Ni siku nyingine tena napenda kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema zake kwa sisi wanadamu...... sote kwa ujumla,wewe unaesoma ujumbe huu na ata ambae yupo miangaikoni mungu amfanyie wepesi......Binafsi Mi mzima kabisa wa afya tele pamoja na Familia yangu nzima kwa ujumla.....Namshukuru sana Mungu kwa Pumzi yake ya bure kwetu na kuzidi kunibariki na kunifungulia milango ya Baraka kwenye kazi yangu ya Muziki ....Si kama sisi tuliopo hapa wazima ni wema sana machoni pakee lakini kwa kudra zake mwenyezi Mungu Tu angali wazima wa Afya....!! Nachukua nafasi hii kuwashukuru Mashabiki zangu kote Nchini na hata nje ya nchi na Dunia nzima kwa support yenu kwangu na mapenzi yenu kwangu ya dhati.....!! Hakuna Nyota Bila Shabiki Bila Nyinyi mi si chochote.....!! Binafsi Nafurahi sana kuwa karibu na nyie japokuwa sio wote ntakaowaridhisha kwa ujumla kwa kuwa ni mashabiki wengi sana kila kona na pembe ya Dunia..... Lakini Mda huu mdogo naopata nafurahi kuwajulia hali kwa pamoja.....
Cha Msingi napenda kuwatakia mafanikio na baraka tele juu yenu iwe kwenye masomo,Biashara,kazi hata kwa wale wagonjwa,wasiojiweza na vilema Mkono wa Mungu ukawe Juu yenu kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mwingi wa baraka na daima utuwazia Mema Juu yetu hata kwa mabaya mengi tumkoseayo...!! Upendo na Amani daima utawale kati yenu katika Maendeleo ya kujenga taifa letu kwa nguvu na umoja kama Nguzo ya Muunganiko na umoja kati yetu.....Dini wala ukabila usiruhusu vitawale kati yenu na kujenga chuki mioyoni mwenu kutokana na tamaa za baadhi ya watu kusababisha mtafaruku kati yetu viumbe wa Mungu....!! Mshukuru Mungu kwa hapo ulipo.....Hakuna kitu kibaya kama kutokuamini wewe si chochote wala si lolote..... Amini ya kwamba upo dunia kwa makusudi ya mwenyezi mungu na Mungu anakusudi na wewe hapo ulipo......!!! .....Ni Hayo Tu kwa Leo....NAWAPENDA SANA......................................!!!!!!!
|