Monday, October 29, 2012

BAHANUZI NA YONDANI FITI KUTEJEA DIMBANI

          Bahanuzi


Na idrisa bandali
BEKI Kevin Yondan na mshambuliaji Said Bahanuzi waliokuwa nje ya Uwanja kwa zaidi ya wiki mbili kutokana na kusumbuliwa na majeruhi, leo wanatarajiwa kuanza programu rasmi ya mazoezi na wenzao baada ya kupata ahueni ya kutosha.

Wachezaji hao wamekuwa wakifanya mazoezi mepesi kwa zaidi ya wiki moja baada ya kupata ahueni kidogo na sasa wamepona kabisa na leo kocha Mholanzi, Ernie Brandts anatarajiwa kuwajumuisha kwenye programu yake kamili, Uwanja wa sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam.

Yanga imerejea kutoka Arusha, ambako Jumamosi ilivuna pointi tatu kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji JKT Oljoro, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na kupanda nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wakitimiza pointi 20 baada ya kucheza mechi 10.

Yanga sasa iko nyuma kabisa ya wapinzani wao wa jadi, Simba SC wanaoongoza Ligi Kuu kwa pointi zao 22, baada ya kucheza mechi 10 pia.

Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame sasa wanajiandaa na mchezo wao ujao wa ligi hiyo, dhidi ya Mgambo JKT Jumatano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mgambo JKT pamoja na kwamba imepanda Ligi Kuu msimu huu, lakini imeonyesha ni timu ya ushindani baada ya kutoa sare ya bila kufungana na Simba SC, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Kwa sababu hiyo, Yanga wamechukua tahadhari ya kutosha kuelekea mchezo huo na tangu jana Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb amekuwa ‘akienda mbio’ kuhakikisha timu inashinda keshokutwa.   

Kurejea kwa Yondan na Bahanuzi kunaongeza matumaini ya ushindi kwa Yanga katika mchezo huo, ingawa upande mwingine ni mtihani kwa Brandts, kwani katika kipindi ambacho wachezaji hao wako ‘wadini’, walioshika nafasi zao wamekuwa wakifanya vizuri.     

Mbuyu Twitwe aliyehamishwa kutoka beki ya kulia hadi beki ya kati tangu Yondan aumie Oktoba 3, amekuwa akifanya vizuri sawa na Jerry Tegete aliyempokea Bahanuzi Oktoba 8, alipoumia naye amekuwa akifanya vizuri pia.

Kwa kuzingatia Twite alikuwa ‘uchochoro’ alipokuwa akicheza pembeni, watu wanasubiri kuona kama Brandts atamrudisha huko huko baada ya Yondan kurejea, au ataamua mmoja kati yao na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ataanzia benchi.

Upande wa Tegete na Bahanuzi, kuna uwezekano mmoja wao atakuwa anaanzia benchi kwa sasa na mwingine kumpokea mwenzake baadaye. 


MILIONI 225 ZAHITAJIKA KUIPELEKA SERENGETI BOYS MOROCCO


Rais wa TFF, Tenga akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Kulia ni Sunday Kayuni, Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF na kushoto, Katibu, Angetile Osiah 


Na idrisa bandali


 RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chillah Tenga amesema kwamba timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys inahitaji zaidi ya Sh Milioni 225 kwa ajili ya kampeni yake iliyobakia ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika mwakani nchini Morocco.

Akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya TFF, Ilala, Dar es Salaam, leo Tenga alisema kwamba shirikisho lake kwa sasa halina fedha hizo, kwa sababu hiyo haina mdhamini, zaidi ya kutegemea misaada ya wadau.

Tenga alisema tayari Kamati ya Vijana ya TFF imekwishakutana kuweka mikakati ya kuiwezesha Serengti kushiriki vema kampeni hizo, ikiwemo kuunda Kamati ya kuisaidia timu hiyo.
Hata hivyo, Tenga hakuitaja Kamati iliyoundwa kwa sababu bado hawajazungumza na Wajumbe walioteuliwa.

Alisema kocha wa timu hiyo, Mdenmark Jacob Michelsen ameomba mechi za kujipima nguvu kabla ya kucheza na Kongo Brazaville kuwania tiketi ya Morocco na Kamati ya Vijana inahangaikia suala hilo kwa sasa.

Alisema tayari kuna mwaliko kutoka Botswana wa Serengeti kwenda kucheza, lakini kutokana na ukosefu wa fedha wanashindwa hadi sasa kutoa jibu.

Kikosi cha wachezaji 25 cha Serengeti Boys kipo kambini mjini Dar es Salaam tangu Oktoba 21, mwaka huu kujiandaa na mechi hiyo, ya kwanza ikichezwa nyumbani Novemba 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, wakati mechi ya marudiano itachezwa wiki mbili baadaye.

Tanzania imefuzu bila jasho hadi kufika hatua hiyo, baada ya wapinzani wake wa awali, Kenya na Misri kujitoa katika Raundi ya Kwanza na ya Pili.
Kama Tanzania itafuzu kushiriki Fainali hizo za mwakani, itapoza machungu ya mwaka 2005 walipofuzu kucheza Fainali za Vijana wa umri huo kwa kuzitoa Rwanda, Zambia na Zimbabwe, lakini baadaye kwa sababu ya ‘kufoji’ umri wa Nurdin Bakari, ikaondolewa mashindanoni.

Zaidi ya Fainali za Mataifa ya Afrika 1980 na CHAN 2009, katika soka ya wanaume, Tanzania haijashiriki fainali nyingine zozote za Afrika tangu iingie kwenye soka ya kimataifa.

Saturday, October 27, 2012

YANGA YAISHUSHA AZAM NAFASI YA PILI


Yanga SC



TIMU ya soka ya Yanga ya Dar es saslaam leo imeibuka na ushindi mwembamba wa goli 1 – 0 dhidi tim,u ngumu ya JKT OLJORO katika Mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani Mkoani Tanga
Goli pekee la Yanga hii leo limefungwa na Beki aliyezua Mtafaruku Mkubwa wakati wa Usahili wake baina ya Vilabnu viwili vikubwa hapa Nchini Simba na Yanga Mbuyu Twite
Goli hilo la leo la Mbuyu Twite linamfanay kuwa na mabao matatu aliyoyafunga tangua ajiunge na Timu hiyo yenye Maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani
Kwa Mtokeo hayo yah ii leo Timu ya Yanga sasa inakuwa imefikisha jumla ya point 20 huku Kinara wa Ligi hiyo Simba ya Dar es salaam akiwa na Jumla ya pointi 22 baada yah ii leo kitandika Timua Azam kwa goli 3- 1
Akiongea na Swiraty Blog Kocha Msaidizi wa Klabu ya Yanga Fred felix Minziro amesema kuwa Mchezo ulikuwa Mgumu tofauti na ilivotarajiwa na Ndio Maana wameshindwa kuibuka na ushindi Mnono hii leo

NDANDA YAAHIDI USHINDI KESHO


Timu ya soka ya Ndanda ya Mtwara Kesho inajitupa tena uwanjani kuwania Pointi Tatu muhimu katika Mchezo wa ligi daraja la kwanza dhidi ya Timu ngumu ya Green Worius katika uwanja wa Nangwanda Mkoani Mtwara
Akizugumza na Swiraty Blog Afisa habari wa Timu ya Ndanda Idrisa bandali amesema kuwa wamejiandaa kufanya vizuri kama ilivokuwa kwa mchezo wa mwanzo dhidi ya timu ya TransitCamp baada ya kuichapa goli 5 – 2
Amesema kuwa Wachezaji wote wako katika hali nzuri isipokuwa Mchezaji Mmoja tu Faraji Kambwili ambae anasunbuliwa na Mkono baada ya kuumizwa na goli kipa wa Tranist Camp Katika Mechi iliyopita
Bandali amesema kuwa hawana sababu ya kupoteza mchezo huo kwa kuwa timu yao itakuwa inacheza katika uwanja wao wa nyumbani wa nangwanda sijaona
“tunawaomba mashabiki waje kwa wingi kuishangilia timu yao ikiibuka na ushindi kesho kwani hatuna sababu ya kupoteza tukiwa katika uwanja wetu wa nyumbani ,tutahakikisha tunaibuka na ushindi kama ilivokuwa katika mchezo wa mwanzo dhidi ya Transit Camp” alisema Bandali
Katika Mchezo uliopita Timu ya Ndanda iliibuka na ushindi wa goli 5 – 2 dhidi uya Transit Cmp na baada ya mechi hiyo ya kesho  Timu ya Ndanda iasafiri kuelekea dar es salaam kwa ajili ya kucheza mechi tatu mfululuizo wakiwa nje ya uwanja wao wa nyumbani