Rais wa TFF, Tenga akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Kulia ni Sunday Kayuni, Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF na kushoto, Katibu, Angetile Osiah |
Na idrisa bandali
Akizungumza na Waandishi wa Habari
makao makuu ya TFF, Ilala, Dar es Salaam, leo Tenga alisema kwamba shirikisho
lake kwa sasa halina fedha hizo, kwa sababu hiyo haina mdhamini, zaidi ya
kutegemea misaada ya wadau.
Tenga alisema tayari Kamati ya
Vijana ya TFF imekwishakutana kuweka mikakati ya kuiwezesha Serengti kushiriki
vema kampeni hizo, ikiwemo kuunda Kamati ya kuisaidia timu hiyo.
Hata hivyo, Tenga hakuitaja Kamati
iliyoundwa kwa sababu bado hawajazungumza na Wajumbe walioteuliwa.
Alisema kocha wa timu hiyo, Mdenmark
Jacob Michelsen ameomba mechi za kujipima nguvu kabla ya kucheza na Kongo
Brazaville kuwania tiketi ya Morocco na Kamati ya Vijana inahangaikia suala
hilo kwa sasa.
Alisema tayari kuna mwaliko kutoka
Botswana wa Serengeti kwenda kucheza, lakini kutokana na ukosefu wa fedha
wanashindwa hadi sasa kutoa jibu.
Kikosi cha wachezaji 25 cha
Serengeti Boys kipo kambini mjini Dar es Salaam tangu Oktoba 21, mwaka huu
kujiandaa na mechi hiyo, ya kwanza ikichezwa nyumbani Novemba 17, mwaka huu
kwenye Uwanja wa Taifa, wakati mechi ya marudiano itachezwa wiki mbili baadaye.
Tanzania imefuzu bila jasho hadi
kufika hatua hiyo, baada ya wapinzani wake wa awali, Kenya na Misri kujitoa
katika Raundi ya Kwanza na ya Pili.
Kama Tanzania itafuzu kushiriki
Fainali hizo za mwakani, itapoza machungu ya mwaka 2005 walipofuzu kucheza
Fainali za Vijana wa umri huo kwa kuzitoa Rwanda, Zambia na Zimbabwe, lakini
baadaye kwa sababu ya ‘kufoji’ umri wa Nurdin Bakari, ikaondolewa mashindanoni.
Zaidi ya Fainali za Mataifa ya
Afrika 1980 na CHAN 2009, katika soka ya wanaume, Tanzania haijashiriki fainali
nyingine zozote za Afrika tangu iingie kwenye soka ya kimataifa.