Sunday, June 3, 2012

MAZUU,MATONYA NA ABDU KIBA WAKO MTWARA TANGU JANA NA WAPIGA SHOE MOJA KITERE NJE KIDOGO YA MTWARA MJINI

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh3x2Z8v0QJ26IKCSzWlZlf83dWad82qyGIzxMVAmBCifNmXTd7EW9qbTQWM7ivYrbbUupCTg7Pp9JgS_n3Acb0uTsYMhuFY3mrZ-wHWUqAAsC5BbVxqyakBWKIi-lRFp9dERmyNou6ys7W/s1600/matonya01bc.jpeg 
http://video.greatlakesmix.com/uploads/thumbs/2toxddmhagwh4ytt.jpg









WASHINDI WA KILI MUSIC WAFANYA KUFURU VIWANJA VYA POSTA KIJITONYAMA DAR(PICHA KWA HISANI YA BLOG YA DJ CHOKA}

KITOKOLOLO kwa steji

 Isha Mashauzi aka Jike la Simba kwa steji

 Malkia wa Taarabu Khadija Kopa kwa steji

 DJ Mafuvu kutoka EA Radio/TV

 AT msanii kutoka ZNZ akilitawala steji

 Ben Pol kwa steji

 Queen Darling kwa steji

 Suma Lee kwa steji...

Saturday, June 2, 2012

stars iko nyuma kwa goli moja kwa bila dk ya 30




kila la heri taifa stars


     

Leo timu yetu ya Taifa Taifa stars inakipiga na ivory coast katika kuwania nafasi ya kucheza kombe la dunia mwaka 2014 huko brazil

Kwa kufahamu maana ya uzalendo na umuhimu wa mchezo huo wa leo Mwenyekiti wenu naitumia nafasi hii kuitakia kila la heri ili iweze kuipeperusha vema bendera ya Taifa la Tanzania

                                         "mungu ibariki tanzania"         

                                          "mungu ibariki taifa stars"

TFF YAWAASA MASHABIKI WA YANGA KUFUATA KANUNI NA TARATIBU ZA KUCHUKUA FOMU ZA UCHAGUZI



WAKATI zoezi la uchukuaji fomu za kuwania uongozi katika klabu ya Yanga likianza leo, kamati ya  uchaguzi ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limewataka wanachama wake kufuata kanuni za uchaguzi zilizowekwa na shirikisho hilo. 

Hatua hiyo inafuatia baadhi ya wanachama wa klabu ya Yanga kukiuka kanuni hizo kwa kutoa taarifa potofu kuhusiana na uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi za zilizowazi utakaofanyika Julai 15mwaka huu. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF Deogratius Lyatto alisema jana kwamba uchaguzi huo ni kwa ajili ya kuziba nafasi za viongozi ili kutimiza akidi na si kwa ajili ya kuchagua upya viongozi kama inavyoenezwa. 

“Kuna upotoshwaji unafanywa na baadhi ya wanachama kuhusiana na uchaguzi huu, napenda ieleweke kuwa, uchaguzi huo utajaza nafasi za viongozi waliojiuzulu na ile ya mjumbe mmoja aliyefariki dunia, hivyo wanachama wa Yanga wafahamu hilo na kuzingatia,”alisema. 

Mbali na hilo, Mwenyekiti huyoa lisema kwamba viongozi watakaochaguliwa watakaa madarakani kwa muda uliosalia kama katiba inavyoelekeza na kwa mantiki hiyo hiyo viongozi hao watamaliza muda wao wa miaka minne mwaka 2014. 

“TFF inaamini kuwa wajumbe wa kamati ya uchaguzi wa Yanaga wqatatekeleza wajibu na majukumu yao ya kikatiba na kikanuni kuhakikisha kwamba klabu hiyo inajaza nafasi zilizowazi  katika mkutanio mu wa uchaguzi kwa kipindi kilichobaki cha mamlaka ya kamati ya utendaji (ibara ya 29 ya Katiba ya Yanga),”alisema. 

Kwa mujibu wa Katibu wa kamati ya uchaguzi ya Yanga Francis Kaswahili,  zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu litamalizika Juni 6, huku Juni 7 hadi 13 kamati itapitia  majina ya walioomba kugombea na kutangaza majina yao, wakati juni 14 hadi 18 itakuwa ni kipindi cha kupokea pingamizi. 

Aidha, Juni 19 hadi 23 utafanyika usaili na kutangaza matokeo, wakati juni 24 hadi 26 itakuwa ni kipindi cha kukata rufaa, juni 27 hadi julao mosi kamati ya uchaguzi TFF itasikiliza rufaa kama zipo, huku Julai 2 yatatabgazwa majina na kampeni kuanza hadi julai 14. 

Uchaguzi huo unafuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti Lloyd Nchunga  baada ya kushinikizwa na baadhi ya wanachama wakiongozwa na baraza la wazee wa klabu hiyo kutokana na kushindwa kuiletea mafanikio klabu hiyo chini ya uongozi wake. 

Pia nafasi ya Makamu mwenyekiti iliyokuwa inashikiliwa na Davis Mosha ambaye alijitoa miezi michache baada ya kuchaguliwa kutokana na kutoelewana na Nchunga, huku mjumbe Theonest Rutashoborwa akitangulia mbele ya haki.  
Uchaguzi huo pia utajaza nafasi za Wajumbe  walioachia ngazi ambao ni pamoja na Mzee Yusuf, Charles Mgondo na Ally Mayay. 

Kwa sasa Yanga imebaki na wajumbe wanne, Mohammed Bhinda, Sarah Ramadhan, Tito Osoro na Salum Rupia ambao baada ya uchaguzi wataungana na viongozi wapya na  kuteua wajumbe wengine watatu kwa mujibu wa katiba, hiyo inatokana na wajumbe hao wa kuteuliwa Seif Ahmed, Mbaraka Igangula na Pascal Kihanga kujiuzulu.


TAIFA STARS KUIVAA IVORY COASTY USIKU WA LEO HUKU KIM POULSEN AKITAJA KIKOSI MAPEMA

Wachezaji wa timu ya Soka ya Taifa ‘Taifa Stars’ wakijifua kwenye Uwanja wa wa kituo cha Michezo mjini Abidjan  kujiandaa na mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast inayotarajiwa kufayika leo kwenye uwanja wa Felix Houphouet-Boigny.

Kocha Kim Poulsen ametaja kikosi cha Taifa Stars ambacho leo (Juni 2 mwaka huu) kitakuwa uwanjani kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan kuivaa Ivory Coast katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia. 

Amefanya mabadiliko katika nafasi mbili kwenye kikosi ambacho Mei 26 mwaka huu kilicheza mechi ya kujipima nguvu na Malawi (The Flames) iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa suluhu. 

Amir Maftah atacheza beki wa kushoto badala ya Waziri Salum wakati Mrisho Ngasa atakuwa mmoja kati ya washambuliaji wa mwisho. Ngasa atacheza nafasi ya Haruna Moshi ambaye hayuko na Stars hapa baada ya kuumia mazoezini siku moja kabla ya safari.

Kikosi kamili cha Taifa Stars ambayo itatumia mfumo wa 4-4-2 ni kima ifuatavyo;

Kipa; Juma Kaseja

Mabeki; Shomari Kapombe, Amir Maftah, Aggrey Morris na Kevin Yondani

Viungo; Shabani Nditi, Salum Abubakari, Frank Domayo na Mwinyi Kazimoto

Washambuliaji; Mbwana Samata na Mrisho Ngasa

Wachezaji wa akiba; Mwadini Ali, Waziri Salum, Juma Nyoso, Erasto Nyoni, John Bocco, Simon Msuva, Jonas Mkude, Christopher Edward na Ramadhan Singano.

Kim amesema kikosi chake kimejiandaa vizuri kwa ajili ya mechi hiyo, na kilichobaki ni kwa wachezaji kudhibitisha maandalizi hayo kwenye dakika 90 za mchezo huo utakaoanza saa 11 kamili jioni (nyumbani itakuwa saa 2 kamili usiku).

Mechi hiyo itaoneshwa moja kwa moja (live) kupitia televisheni ya RTI ambapo itaonekana katika nchi 58 duniani.

Mwamuzi; Slim Jedidi (Tunisia)

Mwamuzi msaidizi namba 1; Bechir Hassani (Tunisia)

Mwamuzi msaidizi namba mbili; Sherif Hassan (Misri)

Mwamuzi wa akiba; Youssef Essrayri (Tunisia)

Mtathmini wa waamuzi; Rachid Medjiba (Algeria)

Kamishna wa mchezo; Saleh Issa Mahamat (Chad)

 

Friday, June 1, 2012

swiraty akiwa na Rahma moja kati ya waimbaji wa Jahazi Morden Taarabu baada ya mahojiano leo Info Radio mtwara

Mzee yusuph akiwa na mafanzi wake

mzee yusuph akiwa na Mfaume Pastory na Robi James toka info radio

Shaibu ndeja a.k.a spear one maarufu mzee wa ndege toka Afro Tingisha ya Info Radio


jahazi taarabu
Jahazi morden taarabu wakiwa ndani ya studio za info radio mchana wa leo

JAHAZI KUWASHA MOTO BLANTAYA MTWARA USIKU WA LEO

Mzee yusuph akiwa katika studio za Info Radio Mtwara

JAHAZI MORDEN TAARABU KUWASHA MOTO LEO MTWARAC KATIKA UKUMBI WA BLANTAYA KWA UCHAKAVU WA BUKU KUMI TU


Baadhi ya tim,u jhazi itakayowasha moto leo hapa mtwara  blantaya hall

JUMAMOSI HII KUMJUA MREMBO ATAKAYEWAKILISHA MTWARA PALE MAKONDE BEACH CLAB

                  
Warembo watakaopanda jukwani kushiriki katika shindano la  kumtafuta Miss Mtwara 2012 siku ya jumamosi juni 2 katika ukumbi wa Makonde Beach mjini Mtwara, ambapo wamekuwa wakiendelea na mazoezi katika ukumbi huo kujiweka tayari kwa ajili ya shindano hilo.
Warembo watakaopanda jukwani kumtafuta Miss Mtwara 2012 Wakimsikiliza mkufunzi wao Isabela mpada (MISS RUVUMA 2006) siku ya jumamosi Juni2 katika ukumbi wa makonde beach
Warembo watakaopanda jukwani kumtafuta Miss Mtwara 2012 Wakimsikiliza mkufunzi wao Isabela mpada (MISS RUVUMA 2006),Pamoja na muandaaji wa shindano Rajab Mchatta. siku ya jumamosi Juni 2 katika ukumbi wa makonde beach

WABISOCO MKOANI MTWARA KUFANYA MKUTANO WA MWAKA KESHO

Chama cha ushirika wa wafanya biashara mkoani mtwara (WABISOCO) Kinatarajia kufanya mkutano wake mkuu wa mwaka wa chama hicho jumamosi hii katika ukumbi wa ushirika uliopo katika manispaa ya mtwara mkoani hapa

Akizungumza na Waaandishi wa ofisini kwake mapema leo Katibu wa Chama hicho Ndugu Hamza Licheta alisema kuwa katika mkutano huo utaambatana na kuchagua viongozi wapya watakaoongoza Chama hicho hapo baadae

Licheta ametoa wito pi kwa wafanya biashara waliowasnachama wa chama hicho kuhakikisha wanalipa ada ya uanachama wao ili waweze kushiriki katika mkutano huo vinginevyo mwanachama ambae hatolipa ada ya uanacahama wake hatoruhusiwa kuhudhurioa mkutano huo

Aidha ameongeza kuwaomba wananchama wa wabisoco mkoani mtwara kuhakikisha wanahudhutri kwa wingi ili kuweza kufanikisha mkunao huo kufanyika hapo kesho

Kufanyika kwa mkutano huo wa mwaka wa wabisoco kunakuja baada ya wanachama wa wabisoco kudai kufanyika kwa mkutano mkuu ambapo ulikuwa haujaitishwa kwa muda mrefu