KWA HABARI ZILIZO HARIRIWA NA KUHAKIKIWA NA WACHAMBUZI MAKINI USIKOSE KUTEMBELEA HAPA KILA SIKU
Saturday, June 2, 2012
TAIFA STARS KUIVAA IVORY COASTY USIKU WA LEO HUKU KIM POULSEN AKITAJA KIKOSI MAPEMA
Wachezaji
wa timu ya Soka ya Taifa ‘Taifa Stars’ wakijifua kwenye Uwanja wa wa
kituo cha Michezo mjini Abidjan kujiandaa na mechi ya mchujo ya
Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast inayotarajiwa kufayika leo kwenye
uwanja wa Felix Houphouet-Boigny.
Kocha
Kim Poulsen ametaja kikosi cha Taifa Stars ambacho leo (Juni 2 mwaka huu)
kitakuwa uwanjani kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan kuivaa
Ivory Coast katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia.
Amefanya
mabadiliko katika nafasi mbili kwenye kikosi ambacho Mei 26 mwaka huu kilicheza
mechi ya kujipima nguvu na Malawi (The Flames) iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam na kumalizika kwa suluhu.
Amir
Maftah atacheza beki wa kushoto badala ya Waziri Salum wakati Mrisho Ngasa
atakuwa mmoja kati ya washambuliaji wa mwisho. Ngasa atacheza nafasi ya Haruna
Moshi ambaye hayuko na Stars hapa baada ya kuumia mazoezini siku moja kabla ya
safari.
Kikosi
kamili cha Taifa Stars ambayo itatumia mfumo wa 4-4-2 ni kima ifuatavyo;
Kipa; Juma Kaseja
Mabeki; Shomari
Kapombe, Amir Maftah, Aggrey Morris na Kevin Yondani
Viungo; Shabani Nditi,
Salum Abubakari, Frank Domayo na Mwinyi Kazimoto
Washambuliaji; Mbwana Samata
na Mrisho Ngasa
Wachezaji
wa akiba; Mwadini
Ali, Waziri Salum, Juma Nyoso, Erasto Nyoni, John Bocco, Simon Msuva, Jonas
Mkude, Christopher Edward na Ramadhan Singano.
Kim
amesema kikosi chake kimejiandaa vizuri kwa ajili ya mechi hiyo, na kilichobaki
ni kwa wachezaji kudhibitisha maandalizi hayo kwenye dakika 90 za mchezo huo
utakaoanza saa 11 kamili jioni (nyumbani itakuwa saa 2 kamili usiku).
Mechi
hiyo itaoneshwa moja kwa moja (live) kupitia televisheni ya RTI ambapo
itaonekana katika nchi 58 duniani.