Kikosi kilichofanya mauaji leo
Erasto Nyoni mfungaji wa bao la ushindi
Shomary Kapombe aliyesawazisha
Boban akisaidia ulinzi
Boban kabla ya kuingia kulia akiwa na Nurdin Bakari benchi
Boban kulia, Nurdin katikati na Shaabn Nditi
Dk Mwankemwa akimtibu jeraha Ngassa
Kaseja akiokoa moja ya hatari langoni Stars
Mwinyi Kazimoto akiwaongoza wenzake kutoka uwanjani baada ya mechi
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeibuka na
ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Gambia jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam, katika mechi ya pili ya Kundi C, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za
Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Stars ilitoka nyuma kwa 1-0 kipindi cha kwanza na kuibuka na
ushindi huo- kwa mabao ya kipindi cha pili ya Shomari Kapombe dakika ya 60 na
Erasto Nyoni dakika ya 87 kwa penalti, baada ya beki mmoja wa Gambia kuunawa mpira
kwenye eneo la hatari.
Stars ambayo mechi ya kwanza ilifungwa 2-0 na wenyeji Ivory
Coast mjini Abidjan Jumamosi iliyopita, kipindi cha kwanza ilicheza ovyo kidogo,
lakini kuingia kwa Haruna Moshi ‘Boban’ aliyechukua nafasi John Bocco ‘Adebayor’
kipindi cha pili, kuliifanya Tanzania icheze kwa uhai na kulitia misukosuko
lango la Gambia hatimaye kupata mabao hayo mawili.
Gambia walitangulia kupata bao lililofungwa na Mamadou
Ceesay dakika ya nne.
Stars sasa imejinasua mkiani mwa kundi C na kupanda nafasi
ya pili badaaye Morocco kutoa sare ya 2-2 jana na Ivory
Coast inayoongoza kwa pointi zake nne.
Kwa Stars huu ni ushindi wa kwanza nyumbani tangu waifunge
Jamhuri ya Afrika ya Kati Machi 26, mwaka jana
|