.Ni onyesho maalum la familia
MKALI
wa filamu nchini Nigeria na Afrika, Omotola Jalade atazindua filamu ya
Wema Sepetu Jumapili hii katika Ukumbi wa Hoteli ya Girafee Ocean View,
iliyopo Mbezi Beach.
Filamu
hiyo iitwayo Super Star imechezwa na Wema, ikionyesha maisha ya mtu
maarufu na changamoto anazozipata ikiwemo kuandikwa mambo mbalimbali
ikiwemo taarifa za vyombo vya habari.
Katika
uzinduzi huo, bendi kutoka Tanzania House Of Talent (THT) watatoa
burudani, kabla ya mashabiki kupata nafasi ya kupiga picha na msanii
huyo.
Omotola,
ambaye ni mke wa rubani Kapteni Matthew Ekeinde, ambao walifunga ndoa
yao angani kwenye ndege atatoa nafasi ya kupiga picha na watu kadhaa.
Katika
uzinduzi huo, pamoja na burudani ya muziki, mashabiki watakaofika hapo,
watapata pia fursa ya kuiona filamu ya Super Star katika viwanja hivyo
vya hoteli hiyo iliyoko ufukweni.
Omotola ambaye yuko kwenye ndoa kwa miaka 16 akiwa na watoto wanne, ana jumla ya albamu mbili za muziki.
Msanii
huyo ambaye mwaka jana alitangaza kuachana na kucheza filamu kutokana
na kuandikwa vibaya, anatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kwenye uzinduzi
huo ambao kiingilio kitakuwa Sh 30, 000 kwa wakubwa na watoto 10,000.