Sunday, June 3, 2012

FAHAMU KWA UFUPI HISTORIA FUPI YA MKOA WA MTWARA

Mtwara ni mji nchini Tanzania ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Mtwara. Kulingana na sensa ya mwaka 2002 idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 92,602 [1] .
Mtwara ni mji wa bandari kando la Bahari Hindi karibu na mpaka wa Tanzania na Msumbiji. Kiutawala Mtwara ni wilaya ya Mtwara mjini umeunganishwa pamoja na mji wa kihistoria wa Mikindani katika halmashauri ya manisipaa ya Mtwara-Mikindani.

Mtwara ni mji mpya ulioanzishwa tangu 1947 mahali ambako palikuwa na kijiji kidogo cha wavuwi tu. Waingereza waliotawala Tanganyika wakati ule walipanga mradi mkubwa wa kilimo katika Tanganyika ya Kusini wakahitaji bandari kwa ajili ya kubeba mazao yake. Mji ulipangwa kitaalamu kwa ajili ya wakazi 200,000 na mahali palichaguliwa kwa sababu ya badari asilia iliyofaa hata kwa meli kubwa.
Bandari ilijengwa na mji mpya ulianzsihwa lakini tangu 1950 ilionekana ya kwamba mradi wa kilimo kilishindikana. 1953 mji ulikuwa na wakazi 36,999 pekee. Mji haukuendelea ukarudi nyuma hasa kwa sababu pwani la Kusini ilikosa barabara na njia za mawasiliano. Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Msumbiji ilizuia biashara ya mpakani.
Tangu miaka ya 1990 uchumi ulianza kusogea mbele polepole. Barabara ya lami inaendelea kutengenezwa kutoka Daressalaam kuelekea Mtwara. Tangu kukamilishwa kwa daraja la mto Rufiji mawasiliano kwa barabara yameboreshwa hata wakati wa mvua. Vilevile feri inayovuka mto Ruvuma imeongeza biashara ya mpakani na Msumbiji.
Kuna pia mipango ya kujenga barabara imara kutoka Mtwara kwenda Songea na Ziwa NyasaMalawi. itakayowezesha badari kuhudumia kusini yote ya Tanzania pamoja na

Mtwara ni kitovu cha usafiri katika kusini-mashariki ya Tanzania. Mabasi kadhaa hufika kila siku kutoka Daressalaam. Meli hufika mara kwa mara. Uwanja wa ndege hufikiwa na Air Tanzania mara tano kila wiki. Barabara ya lami imefikia Lindi na Masasi. Feri ya mto Rovuma inabeba magari na mizigo karibu kila siku. Daraja kwenda Msumbiji unapangwa.
Kuna pia mipango ya kujenga barabara ya lami kutoka Mtwara kwenda Songea na Ziwa NyasaMalawi. itakayowezesha bandari ya mji kuhudumia kusini ya Tanzania pamoja na

ZIPATE KUFAHAMU KATA ZA MTWARA MJINI NA WILAYA ZAKE ZILIZOPO MKOA WA MTWA
Chikongola | Chuno | Jangwani (Mtwara Mjini) | Kisungure | Likombe | Magengeni | Majengo (Mtwara Mjini) | Mitengo | Mtonya | Railway (Mtwara Mjini) | Shangani | Ufukoni (Mtwara Mjini) | Vigaeni