MSHAMBULIAJI mpya wa Chelsea, Eden Hazard amesema ametua katika klabu hiyo kuongeza mataji,
Tayari Chelsea imetangaza katika tovuti
yake kwamba hatimaye imekubaliana na klabu ya Lille ya Ufaransa kwamba mchezaji
wa kimataifa ya Ubelgiji, Eden Hazard, atajiunga na klabu hiyo ya Stamford
Bridge msimu ujao. Mchezaji huyo, mwenye umri wa miaka 21, tayari afya yake
imekaguliwa na klabu ya Chelsea, na imeonekana hana tatizo lolote.
Walipochukua ubingwa wa ligi ya klabu bingwa, nilijiuliza,
"Kwa nini sio Chelsea?", alisema Hazard.
"Kulikuwa na mvutano kati ya Chelsea na Manchester
united, lakini binafsi naona Chelsea ndio mradi bora zaidi. Ni klabu cha
ajabu."
Inaarifiwa kwamba Chelsea wameamua kutoa pauni milioni 32
kumpata kijana huyo, na ambaye akizungumza na kituo cha redio cha nchini
Ufaransa, RMC, aliongezea: "Chelsea ni timu changa, na nitakuwa na nafasi
bora zaidi ya kucheza."
"Ikiwa nitajitahidi kucheza vyema nikiwa Chelsea,
huenda nikapata nafasi katika timu."
Hazard alikuwepo katika kikosi kilichoshinda ligi wakati
Lille ilipopata ubingwa mwaka 2010-11 na katika msimu wake wa mwisho,
alifanikiwa kufunga magoli 21 katika mechi 48.
Katika mechi yake ya mwisho dhidi ya Nancy mwezi uliopita,
alifanikiwa kupata hat-trick (magoli matatu) wakati timu yake ilipocheza dhidi
ya Nancy.
Lakini alishindwa kuvuma wakati Ubelgiji iliposhindwa na
England katika mechi ya kirafiki Jumamosi iliyopita.
Hiyo ilikuwa ni mara yake ya 28 kuichezea timu yake ya taifa
ya Ubelgiji.
Hazard sasa ni mchezaji wa pili kusajiliwa Chelsea tangu
dirisha la usajili la mwezi Januari, wa kwanza akiwa ni mchezaji wa kimataifa
wa Ujerumani, Marko Marinas.
|