WAKATI LEO TUKIAZIMISHA SIKU YA MAZINGIRA HEBU TUANGALIE IDARA YETU YA MAZINGIRA HAPA NCHINI
Umuhimu
wa mazingira kwa uchumi wa Tanzania uko katika sura nne
zifuatazo:-
¨
Mazingira yanaipatia nchi
mahitaji yote ya msingi kwa ajili ya kufanikisha masuala ya jamii
na uchumi.
¨
Mazingira ndiyo makazi ya viumbe
vyote – memea na wanyama ambao ndiyo urithi usiokuwa na badala
yake.
¨
Mazingira ni chombo cha kuweka
yale yasiyofaa.
¨
Mazingira ni msingi ambao ndiyo
itakuwa jawabu la kupunguza unyonge wa umaskini.
Kwa
hiyo ni dhahiri kwamba msukumo mkubwa wa uongozi wa mazingira ni
kulinda sehemu asili ya kuishi binadamu na kuoanisha upungufu
uliopo kwenye mazingira katika kusaidia kufikia maamuzi yanayohusu
masuala na shughuli za uchumi.
Serikali
ya Tanzania ilitambua hatari ya kupoteza rasilimali hiyo kama vile
hewa safi, mabaki ya mimea na wanyama wa kale, nyangumi, miti ya
asili na wanyama/mimea ambayo iko mbioni kutoweka.
Katika
kurekebisha hali hiyo, serikali imechukua hatua thabiti kwa
kutengeneza sera, sheria na mfumo wa taratibu ambazo zinaendana na
masuala ya jamii, uchumi na siasa.
Serikali
kwa kushirikiana na washika dau mbalimbali wameweka mkazo katika
kuendeleza kukuza na kuhamasisha ushirikishwaji wa jumuiya na watu
binafsi katika kuimarisha uhifadhi na uongozi wa mazingira.
Pamoja na hayo kulikuwa na kampeni za kutambua umuhimu wa
mazingira, elimu ya mazingira na kuendeleza ujuzi ambao ulisaidia
katika kuhifadhi na kuendesha masuala ya
mazingira. Mkazo
wa kuhifadhi na kusimamia mazingira ni kwa ajili ya kukuza uwezo
na akili za jamii na watu binafsi katika kudumisha usimamizi kwa
manufaa yao na manufaa ya vizazi vijavyo. Inatia moyo kwamba
juhudi hizo zimeamsha fahamu za watu, moyo wa kupenda na
vitendo vya kusaidia kwa sababu zaidi ya idadi 159 ya
CBO’s (Community Based Organiations) na NGO’S
(Non-Governmental Organisations) zimeundwa zikiwemo pia na sekta
binafsi na watu binafsi kujiunga katika mkumbo.
Isitoshe, Serikali kwa kushirikiana na mashirika na
mawakala kama vile CBO’s/NGO’s wanatekeleza mipango mbalimbali
katika maeneo ya mijini na vijijini.
Vyombo vya habari (radio, televisheni, magazeti)
vimefanyaka kazi nzuri katika kuhamasisha na
kutangaza vipindi mbalimbali vya elimu kuhusu masuala ya
mazingira na hivyo kutoa mafunzo kwa hadhara na watu binafsi ya
kuwa na moyo wa kupenda, kujituma na kufahamu jinsi ya kuhifadhi
na kusimamia mazingira.
Serikali
ilitumia sera za sekta zinazohusiana na misitu, madini, wanyama
pori, samaki, kilimo, mifugo na ardhi ambazo zimeweka kipaumbele
masuala ya usimamizi na hifadhi za rasilimali na mazingira, kukuza
kufahamu wa wananchi wa kuelewa uhusiano kati ya mazingira na uhai
na kuendeleza ushirikiano wa kimataifa kuhusu ajenda ya mazingira.
Ni
dhahiri kwamba uhifadhi na usimamizi wa mazingira duniani na
kitaifa una nia ya kushinda matatizo yanayotokana na umaskini,
maradhi, hali mbaya na duni ya upatikanaji wa chakula, makazi
machafu, maji yasiyo salama, upatikananji wa nishati usioridhisha
na ukosefu wa ajira.
Kuelewa
kwa wananchi na watu binafsi juu ya faida za kuhifadhi na
kusimamia mazingira ndiyo msingi wa kuendeleza rasilimali na
mazingira. Hiyo
inakwenda sambamba na utekelezaji wa mipango thabiti ya kuondoa
umaskini kwa sababu umaskini unaendana na matumizi mabaya ya
rasilimali na uharibifu wa mazingira na hivyo juhudi za kuuondoa
umaskini zinahitaji ushirikiano wa jinsia zote.
Zaidi ya hayo, serikali imeamua kushughulikia hifadhi na
usimamizi wa mazingira pamoja na kuondoa umaskini ukishirikiana
kikamilifu na watu binafsi, CBO’s, NGO’s na wafadhili.
Sera
Madhumuni
ya Sera ya Taifa ya Mazingira ya 1997 ni yafuatayo:-
¨
Kuhakikisha udumishaji, usalama
na matumizi sawa ya rasilimali kwa mahitaji ya msingi ya sasa
na ya vizazi vijavyo bila kuharibu mazingira au kuhatarisha afya
na usalama.
¨
Kuzuia na kudhibiti uharibifu wa
ardhi, maji, mimea na hewa ambayo ndiyo husaidia mfumo wa uhai
wetu.
¨
Kuhifadhi na kuendeleza urithi
wetu na ule unaotengenezwa na binadamu, ikiwa ni pamoja na maisha
ya viumbe wa aina mbalimbali na vya pekee nchini Tanzania.
¨
Kurekebisha hali na uzalishaji wa
maeneo yaliyoharibiwa pamoja na makazi ya watu mijini na vijijini
ili watanzania wote waweze kuishi katika hali ya usalama, kiafya,
kuzalisha bidhaa pamoja na kuishi katika mazingira mazuri yenye
kuvutia.
¨
Kung’amua na kufahamu mahusiano
muhimu kati ya mazingira na maendeleo na kuhimiza ushirikiano wa
mtu binafsi na jamii katika kuhifadhi mazingira.
¨
Kuendeleza ushirikiano kimataifa
kuhusu ajenda ya mazingira na kupanua ushiriki na mchango wetu kwa
pande zote zinazohusika ikiwa zinahusu nchi jirani na mashirika na
mipango ya ulimwengu pamoja na utekelezaji wa mikataba.
Taratibu za sheria
Sera
ya Taifa ya mazingira ya 1997 inasisitiza umuhimu wa kutunga
sheria za mazingira na sheria za Sekta hiyo kitu ambacho ni cha
lazima katika kusimamia ipasavyo na kwa manufaa kwa mazingira na
kustawisha uhai. Sheria
za mazingira zinazofaa na zenye maana ni lazima zieleweke sawa
sawa na kuthaminiwa na jumuiya na watu wanaolengwa.
Sheria zitaweka bayana viwango na taratibu, kazi na mipaka,
kubuni masharti kwa ajili ya washikadau wote, ambayo yatakwenda
sambamba na shughuli za binadamu na usimamizi thabiti wa
rasilimali. Serikali
iko mbioni kutayarisha sheria hiyo. Sheria nyingi zinazohusu Sekta ya mazingira zimetungwa na
kurekebishwa ambazo zinahusu yafuatayo:
Misitu, wanyamapori, uvuvi, madini, nishati, maji, ardhi na
mamlaka za mitaa na mijini,
Serikali
imeweka saini mikataba kadhaa ya mazingira na kuridhia makubaliano
na nchi za kimatifa na nchi za jirani kama ifuatayo:
·
Mapatano
juu ya “Biological Diversity” yaliyo idhinishwa tarehe 8 Machi
1996.
·
Mapatano
kwa ajili ya hifadhi, usimamizi na maendeleo ya mazingira ya
bahari na mwambao wa Afrika Mashariki pamoja na itifaki
zinazohusika na mapato hayo yaliyofikiwa tarehe 1 Machi 1996.
·
Mkataba
wa umoja wa Mataifa wa kupambanua na jangwa ulisainiwa Aprili
1997.
·
Mkataba
wa umoja wa Mataifa unaohusu mfumo wa mabadiliko ya Hali ya Hewa
ulisainiwa Aprili, 1996.
·
Makubaliano
ya vienna ya kuhifadhi tabaka la ozoni (ozone layer) na
makubaliano ya Montreal juu ya vitu vinavyoharibu tabaka la ozoni
yaliyosainiwa Aprili 7, 1993 na Aprili 16, 1993.
·
Mkataba
wa Basley wa kudhibiti kusafirisha nje ya mipaka madawa yenye
hatari na jinsi ya kuyateketeza uliowekwa saini tarehe 7 Aprili
1993, na
·
Makubaliano
ya Bamako juu ya kuzuia kuingiza Afrika na kudhibiti kusafirisha
nje ya mipaka madawa yenye hatari katika Afrika yaliyofikiwa
Aprili 7, 1995.
Jukumi
la Sekta ya Umma na Sekta Binafsi
Inakubalika
kote kwamba jukumu la kusimamia mazingira ni wajibu wa kila mtu.
Majukumu ya mashirika ya Serikali ni kuzisaidia jumuiya
pale zilipo kuelewa hali zao kuzisaidia kuwajibika kuendesha
maisha yao. Kitu cha
muhimu ni kutayarisha Sera, kutunga sheria na mifumo ya kusimamia,
pamoja na kuimarisha mipango ya elimu.
Zaidi ya hayo, serilai itawajibika kutoa msaada wakati
unaofaa na kutoa taarifa sahihi zinazohusu usimamizi wa mazingira.
Kama ilivyoelezwa katika Sera ya Taifa ya mazingira ya
1997, na kufafanuliwa katika Dira ya Maendleo 2025 jumuiya na
vikundi vya wafanyabiashara vina wajibu wa kupanga, kutekeleza
mipango/miradi inayohusu mahitaji yao na kuchochea matumizi
yanayofaa ya rasilimali pamoja na kutumia tena, kurudisha katika
mzunguko wa kutumika na kunguza uchafu.
Zaidi ya hayo Sekta binafsi ina wajibu wa kushiriki katika
mabaraza mbalimbali yakiwemo ya kutayarisha Sera na kushiriki
katika masuala ya kutunga sheria zinazohusu usimamizi wa
mazingira.
Jumuiya
ya wahisani
Usimamizi
wa mazingira umepokea misaada mingi kutoka kwa jumuiya ya wahisani
kuliko Sekta nyinine yoyote nchini Tanzania kwa sababu ya umuhimu
wake katika uchumi wa nchi. Wahisani
wanaochangia kwa hali na mali ni DFID, ICUN, GEF, FAO, WB, USAID,
UNDP, UNEP, CARE pamoja na Serikali za Finland, Norway, Denmark,
Uholanzi na Sweden.
Idara
ya mazingira
·
Idara
ya mazingira ina majukumu makuu yafuatayo:
·
Kuandaa
Sera ya mazingira
·
Kuunganisha
na kusimamia shughuli za mazingira
·
Kushughulikia
mipango ya mazingira
·
Kufanya
utafiti juu ya Sera zinazohusiana na mazingira
Mbinu
na mipango ya Idara
·
Mpango
wa Taifa wa vitendo wa mazingira wa 1994.
·
Mpango
wa Taifa kwa Agenda 21 ya 1993.
·
Mpango
wa Taifa wa kupambana na Jangwa wa 1999.
·
Mpango
wa kuhifadhi uhai wa mwambao wa 1995.
·
Mpango
wa Nchi wa kuondoa viti vinavyoharibu tabaka la ozoni wa 1996.
·
Mpango
wa Taifa juu ya mabadiliko ya tabia ya dunia wa 1997.
Anwani:
Ofisi
ya Makamu wa Rais
S.L.P.
5380
Dar
es salaam
TANZANIA
Simu:
+255(022)-2113983, 2113926
Fax:
+255(022)-2112997, 2113082
Wakala
zilizo chini ya idara
Baraza
la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) liko chini ya Ofisi ya
Makamu wa Rais. Jukumu
kuu la NEMC ni kutoa ushauri kwa Ofisi ya Makamu wa Rais juu ya
masuala yanayohusu usimamizi na hifadhi ya mazingira.
Baraza
la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) lilianzishwa na sheria
ya Bunge namba 19 ya 1983 kutoa ushauri kwa Serikali juu ya
masuala yote yanayohusu usimamizi wa mazingira.
Katika kutekeleza jukumu lake, NEMC ina mamlaka ya kukuza,
kuchochea, kusimamia na kuunganisha masuala yote yanayohusika na
mazingira.
Dira
ya NEMC
Kutoa
uongozi wa kiutaalam katika kushuhulikia kwa vitendo jinsi ya
kudumisha maendeleo ya mazingira.
Maelezo
ya ujumbe wa NEMC
Maisha
ya Watanzania yanahusiana kwa karibu sana na mazingira, uhai wao
na uhai wa vizazi vijavyo unategemea kuwepo kwa uhusiano wa amani
kati ya watanzania na rasilimali ya ulimwengu.
Kwa bahati mbaya, kutokana na kuongezeka haraka kwa idadi
ya watu, kukimbilia kwa watu kwenda mijini, umaskini na ujinga,
utaratibu mbaya za kilimo, uharibifu wa misitu, kupungua kwa
rasilimali za majini na uchafuzi wa hewa na hivyo kuleta matatizo
ya uwiano kati ya rasilmali za mazingira yaliyopo, watu wanatakiwa
sasa kutambua kuwa matatizo hayo yanayotokana na uharibifu wa
mazingira, na kuwafanya kutambua umuhimu wa kuchochea usimamizi wa
mazingira na ili Watanzania wote washiriki katika jitihada za
kuchukua hatua za kurekebisha hali hiyo mbaya ya sasa inaoelekea
kuyadhalisha mazingira.
Ujumbe
Baraza
la Taifa la kusimamia mazingira (NEMC) ni wakala wa kuongoza kutoa
ushauri wa kiutaalam, kuunganisha na kuratibu jukumu la kulinda
mazingira na matumizi mazuri ya rasilimali katika Tanzania, NEMC
ina wajibu wa kutoa ushauri, kushiriki kwa kupanga na vyombo
vingine vinavyohusika na masuala ya mazingira na watu wote kwa
jumla pamoja na kusaidia na kuendeleza hatua zinazofaa za kusaidia
kufanikisha hali nzuri ya maisha katika Tanzania.
Kazi
·
Kushauri
Serikali juu ya masuala yote ya kitaalam ili kufanikisha usimamizi
thabiti wa mazingira.
·
Kuunganisha
shughuli za utaalam za vyombo vyote vinavyoshugulika na masuala ya
mazingira.
·
Kutia
mkazo utekelezaji wa sheria za mazingira (kanuni, viwango,
miongozo na taratibu).
·
Kuchunguza,
kusimamia na kutathmini vitendo vyote ambayo vina migogoro na
mazingira.
·
Kustawisha
na kusaidia upatikanaji wa taarifa, mawasiliano na uwezo kwa ajili
ya mazingira.
·
Kutafuta
taarifa za kisayansi zinazohusu sababu za kimsingi zinazosababisha
mabadiliko katika mazingira na kuhamasisha maendeleo ya mazingira
kwa kutumia teknolojia iliyo sahihi.
Anwani:
Baraza
la Taifa la Kusimamia Mazingira
S.L.P.
63154
Dar
es salaam
TANZANIA
Simu:
+255-(022)-2134603
0741-608930/232310
fax:
+255-(022)-2134603
Mashirika
Chuo
Kikuu cha Kilimo cha Sokoine
Anwani:
Kituo
cha Misitu
Morogoro
TANZANIA
Simu:
+255-023-263511
Taasisi
ya Uchunguzi wa Misitu Tanzania(TAFORI)
Anwani:
S.L.P.
1854
Morogoro
TANZANIA
Simu:
255-023-2263725
Mpango
wa Mbegu za Miti Taifa wa (NTSP)
Anwani:
S.L.P.
373
Morogoro
TANZANIA
Simu:
255-023-25632192
Fax:
255-023-2563275
Taasisi
ya Mafunzo ya Misitu Olmotonyi
Anwani:
S.L.P.
943
Arusha
TANZANIA
Simu:
255-027-50441
Taasisi
ya Mafunzo ya Uvuvi Kunduchi
Anwani:
S.L.P.
60091
Dar
es salaam
TANZANIA
Simu:
255-022-2650011
Kutuo
cha Maendeleo ya Uvuvi Mbegani
Anwani:
S.L.P.
83
Bagamoyo
TANZANIA
Taasisi
ya Mafunzo ya Uvuvi Nyegezi
Anwani:
S.L.P.
1213
Mwanza
TANZANIA
Mbuga
za Taifa za Tanzania (TANAPA)
Anwani:
S.L.P.
3134
Arusha
TANZANIA
Simu:
255-027-2508040
Fax:
255-027-2508216
Mamlaka
ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro
Anwani:
S.L.P.
1
Morogoro
TANZANIA
Simu:
255-027-2504619
Fax:
255-027-2503339
Taasisi
ya Utafiti wa Wanyama Pori Tanzania (TAWIRI)
Anwani:
S.L.P. 661
Arusha
TANZANIA
Chuo
cha Afrika cha Usimamizi wa Wanyama Pori
Anwani:
S.L.P.
3231
Moshi
TANZANIA
Fax:
255-027-2551113
Sekta
ya Utalii
Bodi
ya Tanzania ya Utalii
Anwani:
S.L.P.
2485
Dar
es salaam
TANZANIA
Simu:
255-022-2110908, 2111244/5, 2136105
Fax:
255-022-2116420
Taasisi
ya Mafunzo ya Hoteli na Utalii
Anwani:
S.L.P.
9181
Dar
es salaam
TANZANIA
Simu:
255-022-2112223
Viko
vyama vyingi vya Jumuiya (CBOs) na visivyo vya Serikali (NGO’s)
vinavyojishughulisha na masuala ya mazingira ambayo ni pamoja na
Chama cha Hifadhi Wanyama Pori Tanzania (TWCS) Dar es salaam,
Klabu ya Malihai Tanzania (MCT) Arusha, Timu ya Wanasheria wa
Mazingira (LEAT) Dare es salaam. Chama cha Mazingira Tanzania
(TESO) Dar es salaam, Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira
Tanzania (JET) Dar es salaam na Kituo cha Nishati, Mazingira,
Sayansi na Teknolojia (CEEST) Dar es salaam.