WAKATI zoezi la uchukuaji fomu za
kuwania uongozi katika klabu ya Yanga likianza leo, kamati ya uchaguzi ya
Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limewataka wanachama wake kufuata kanuni za
uchaguzi zilizowekwa na shirikisho hilo.
Hatua hiyo inafuatia baadhi ya
wanachama wa klabu ya Yanga kukiuka kanuni hizo kwa kutoa taarifa potofu
kuhusiana na uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi za zilizowazi utakaofanyika Julai
15mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya
TFF Deogratius Lyatto alisema jana kwamba uchaguzi huo ni kwa ajili ya kuziba
nafasi za viongozi ili kutimiza akidi na si kwa ajili ya kuchagua upya viongozi
kama inavyoenezwa.
“Kuna upotoshwaji unafanywa na
baadhi ya wanachama kuhusiana na uchaguzi huu, napenda ieleweke kuwa, uchaguzi
huo utajaza nafasi za viongozi waliojiuzulu na ile ya mjumbe mmoja aliyefariki
dunia, hivyo wanachama wa Yanga wafahamu hilo na kuzingatia,”alisema.
Mbali na hilo, Mwenyekiti huyoa
lisema kwamba viongozi watakaochaguliwa watakaa madarakani kwa muda uliosalia
kama katiba inavyoelekeza na kwa mantiki hiyo hiyo viongozi hao watamaliza muda
wao wa miaka minne mwaka 2014.
“TFF inaamini kuwa wajumbe wa kamati
ya uchaguzi wa Yanaga wqatatekeleza wajibu na majukumu yao ya kikatiba na
kikanuni kuhakikisha kwamba klabu hiyo inajaza nafasi zilizowazi katika
mkutanio mu wa uchaguzi kwa kipindi kilichobaki cha mamlaka ya kamati ya
utendaji (ibara ya 29 ya Katiba ya Yanga),”alisema.
Kwa mujibu wa Katibu wa kamati ya
uchaguzi ya Yanga Francis Kaswahili, zoezi la uchukuaji na urejeshaji
fomu litamalizika Juni 6, huku Juni 7 hadi 13 kamati itapitia majina ya
walioomba kugombea na kutangaza majina yao, wakati juni 14 hadi 18 itakuwa ni
kipindi cha kupokea pingamizi.
Aidha, Juni 19 hadi 23 utafanyika
usaili na kutangaza matokeo, wakati juni 24 hadi 26 itakuwa ni kipindi cha
kukata rufaa, juni 27 hadi julao mosi kamati ya uchaguzi TFF itasikiliza rufaa
kama zipo, huku Julai 2 yatatabgazwa majina na kampeni kuanza hadi julai
14.
Uchaguzi huo unafuatia kujiuzulu kwa
aliyekuwa Mwenyekiti Lloyd Nchunga baada ya kushinikizwa na baadhi ya
wanachama wakiongozwa na baraza la wazee wa klabu hiyo kutokana na kushindwa
kuiletea mafanikio klabu hiyo chini ya uongozi wake.
Pia nafasi ya Makamu mwenyekiti
iliyokuwa inashikiliwa na Davis Mosha ambaye alijitoa miezi michache baada ya
kuchaguliwa kutokana na kutoelewana na Nchunga, huku mjumbe Theonest
Rutashoborwa akitangulia mbele ya haki.
Uchaguzi huo pia utajaza nafasi za
Wajumbe walioachia ngazi ambao ni pamoja na Mzee Yusuf, Charles Mgondo na
Ally Mayay.
Kwa sasa Yanga imebaki na wajumbe
wanne, Mohammed Bhinda, Sarah Ramadhan, Tito Osoro na Salum Rupia ambao baada
ya uchaguzi wataungana na viongozi wapya na kuteua wajumbe wengine watatu
kwa mujibu wa katiba, hiyo inatokana na wajumbe hao wa kuteuliwa Seif Ahmed,
Mbaraka Igangula na Pascal Kihanga kujiuzulu.