Thursday, April 25, 2013

DALAZ CONNECTION KUTOONGEZA MSANII MWINGINE


dj sam
Mmiliki wa kampuni ya DALAZ CONNECTION DJ SAM amepiga story na SWIRATY BLOG na amefunguka kuwa kwa sasa hawatoingiza msanii yeyote yule baada ya kumsimamisha Msanii wao GITAA kutokana na kukiuka makubalianop ya mikataba

DJ SAM amefunguka hivo baada ya story zilizokuwa zimezagaa kitaa kwamba nafasi ya GITAA kwenye kampuni ya DALAZ CONNECTION ingezibwa na KIBEGA

DJ sam kwa sasa amesema wanachoangalia ni kuimarisha kampuni yna kutoa ngoma kali m=pamoja na shoo ambazo zitakuja baadae katika kulitambulisha kudni lake ambalo linasimamiwa na kampuni hiyo

PRODUZA LAMAR ANATAFUTA VIJANA WA KIUME WENYE VIPAJI VYA KUIMBA


Produza Lamar akiwa kwenye studio zake Fishcrab
Lamar kutoka studio zake za Fish Crab amesema kuwa hivi sasa anasaka wasanii wanaume wenye vipaji vya kuimba kwa kiingereza na kiswahili.
Lamar alisema kuwa anafanya hivyo kwakuwa mwaka uliopita alifanya mchakato huo huo wakutafuta vipaji kwa upande wa wasichana ambako alifanikiwa nakupata wasichana watatu ambao hivi sasa ndo wanaunda kundi la wasanii wa kike 'Shosteez'.Kwa sasa anasema anataka kutengeneza kundi la wasanii wa kiume wanaoimba kama alivyofanya kwa wasanii wa kike.
Lamar akiwa na kundi ambalo analisimamia hivi sasa 'Shosteez'
Kama wewe ni kijana wa kiume una uwezo nenda katika studio za Fishcrab zilizopo maeneo ya Kariakoo au unaweza kutuma 'demo' yako ukiwa unaimba kupitia anuani ya barua pepe ambayo ni fishcrab@gmail.com, alisema Lamar.

HAWA NDIO WALIOCHAGULIWA KUGOMBANIA TUZO ZA KILI MUSIC 2013 (KTMA)

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Comments zako kuhusu KTMA 2013 zitapitiwa na watu waandaaji baadae kidogo hivyo toa ya moyoni.

story kwa hisani kubwa ya website ya millard ayo

Wednesday, April 24, 2013

ICHEKI HAPA VIDEO YA G NAKO ft BEN POL MAMA YEYOO


OFA MAALUMU .....

Menejimenti ya SWIRATY BLOG imeetoa ofa maalumu kwa wasanii wa kusini na sehemu nyingine kutumia blog yale kwa ajili ya kutuma wimbo wako ama picha zako ili uweze kuonekana na kusikika na fanz wako kote ulimwenguni

email pekee ya kutuma mizigo na picha zako ni hii hapa idrisabandali@yahoo.com

NAKAAYA AKANA UJAUZITO WAKE KUWA WA MTU MAARUFU

Nakaaya

Hit maker wa "Mr Politician" Nakaaya Sumari, baada ya kukaa kimya kwa mda mrefu, amezungumza na Amplifaya ya Clouds Fm na kuthibitisha kuwa ana ujauzito ambao ni miezi kadhaa tu atajifungua.Alipoulizwa kuhusu baba wa mtoto huyo, Nakaya alicheka kwanza na kusema kuwa ni wa mtakatifu, na kugoma kabisa kumtaja baba wa mtoto huyo mtarajiwa, huku akisema kuwa sio wa mtu yeyote anaejulikana.

blog hii inakutakia li;a la kheri na ujifungue salama

hivi sasa pia Nakaaya ameachia wimbo mpya unaoitwa "Utu Uzima Dawa" akiwa amemshirikisha producer Dunga, ukiwa umetengenezwa chini ya producer Lamar "Fish Crab"

LINEX ATIMIZA NDOTO ZAKE

LINEX

 

Msanii Linex leo hii amekamilisha ndoto yake ya siku

nyingi kufanya kazi na msanii maarufu kutoka Kenya

"Wyre", ngoma hiyo ambayo kwa msaada wa

digitali inaelekea kukamilika, imetengenezwa beat

na producer Fundi Samweli ambae yupo Sweden

kwa hivi sasa, ambayo ilitumwa kwa Linex na kuipeleka

kwa producer Mswaki ambae pia ameongezea

maujuzi yake, na hapo ndipo linex akaingiza sauti zake.


 

Hatimae leo beat na vocal za Linex zimetumwa Kenya

kwa ajili ya Wyre kuingiza sauti leo usiku na kisha

kuongezea maujuzi pia akiwa kama producer..

kuonyesha furaha ya kukamilisha asilimia kubwa

ya kazi hiyo Linex ameamua kushare na mashabiki

zake kupitia ukurasa wake wa facebook kwa kuandika status hii

Linex Sunday:

Siku ya leo imekua nzuri sana kwangu nimepiga kazi na mtu nnaemzimiaga kitambo linex ft wyre cumn soon but sita ahidi ni lini itatoka but saiz ndo kazi imeisha God is good

BANDALI NA KIBEGA WABANWA MAENEO WAKIFANYA YAO

bnadali @ mikindani
kibega akiwa na bandali

VIDEO ZILIZOKUWA NA UBORA KUTOCHEZWA KWA TV...

bandali
 

Presenter Mkali wa vipindi vya tv vya "BONGO BANG NA UNTOUCHABLE WEEKEND SHOW'  idrisa bandali ameweka wazi msimamo wake wa kutopiga video za wasanii zisizokuwa na ubora katika vipindi vyake

Presenter huyo anayekuja kwa kasi katika tasnia hiyo ameiambia Swiraty Blog kwamba lengo la kuweka wazi msimamo wake hou ni kutaka kuwafanya wasanii wenyewe pamoja na watengenezaji wa video zao kutengeneza video zenye ubora ambao hata mashabiki wao watazipenda kuziona

"Unajua napata wakati mgumu sana wa kuzicheza ngoma za hawa ndugu zangu ambao kimsinbgi nimejitolea kuwasaidia kwa sababu ubora wake ni hafifu sana na ukiangalia kwa sasa watu wanafanya video kali sana, sasa ni lazima niweke msimamo wanguo huo kwa kuwa vipindi navyofanya vimekuwa na watazamaji wengi tofautri tofauti na hii ni kuwasaidia wasanii wenyewe coz huwezi jua mtu anaeza akapenda kazi yake atakapoiona hapa then akatamani kuyfanya nae kazi ...so wajipange kwa hilo bana" alisema bandali

Mkali huyo toka Mtwara kebo Televisheni pia ametumia fulsa hiyo pia kuwataka wasanii kujitambua kwa nini wamekuwa wasanii na wana mchango gani kwa jamii

"unajua ishu ni nini?... wasanii wetu hawajuwi thamani yao ka jamnii ndio maana kial kukicha wao wanawaza kytoa ngoma tu ambazo sometimes hazina mashiko...


DALAZI CONNECTION YAMFUKUZA MSAANII WAKE "GITAA"



gitaaa
Msanii anaekuja kwa kasi katika miondoko ya muziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Flava "GITAA" amefukuzwa kutoka kwenye kundi lake la "DALAZI CONNECTIN" Swiraty blog ina mchongo wote

Akizungumza na SWIRATY BLOG Mmoja wa Viongozi wa Dalaz Connection Dj sam amesema wameamua kumpiga stop Gitaa kutokana na kwenda kinyume na mkataba wake alioingia na kampuni hiyo

inasemekana ishu kubwa iliyopelekea Gitaa kupigwa chini katika na kampuni hiyo ni kitendo chake cha kuondoka bila taarifa na kwenda kupiga shoo wilani newala hivi karibuni

dj Sam amesema kuwa taratibu za dalaz connection zimekiukwa na gitaa na hivo amesimamishwa ili iwe fundisho kwa wasanii wengine waioko katika kundi hilo

Wasanii wengine waioko katika kundi hilo ambalo pia linamilikiwa na producer mkali toka stuido za 29 Reccod ni pamoja na H moo aliyetamba na single yake ya maumivu ya mapenzi aliyom shikirikisha Pasha

Taarifa za chini ya kapeti zinasema kuwa baada ya kumtimua gitaa toka katika kundi hilo uongozi wa kundi hilo sasa una mipango ua kuziba pengo la msanii huo kwa kuchukua msanii anayetamba na ngoma ya mitikshi kwa sasa ambaye si mwingine bali ni "KIBEGA"

Swiraty Blog imepiga story na kibega ambaye kwa ufupi amesema hatambui hilo na kama lipo basi ataliweka wazi baada ya makubaliano yote ikiwemo swala la maslahi yake litakapowekwa wazi

Saturday, April 20, 2013

JOSE MOURINHO AMTIMIZIA NDOTO KIJANA MSAFISHA MITAA ALIYESAFIRI KUTOKA MAREKANI KWENDA SPAIN KUONA EL CLASSICO - NA KUMPA KAZI REAL MADRID

 


 
Soka ina muda mchache kwa stori za kugusa moyo siku za hivi karibuni, lakini kama kuna mtu anaweza akatengeneza stori za kugusa mioyo ya watu basi ni Jose Mourinho Special One.

Katika stori ya kusisimua, Meneja wa Real Madrid ameweza kuyabadilisha maisha ya raia mmoja wa Mexico kutoka kuwa msafisha stesheni za treni mpaka kuwa mmoja ya watu muhimu ndani ya timu yake.

Abel Rodriguez, 41, ambaye alikuwa akifanya kazi ya kusafisha stesheni za treni jijini Los Angeles, alitumia fedha zake chache anazopata kupitia kazi kusafiri mpaka ulaya na kujaribu kuangalia El Clasico dhidi Barcelona mapema mwezi wa pili mwaka huu.
Bila kuwa na tiketi, au hata sehemu ya kufikia jijini Madrid, kijana huyo wa kimexico alikuwa na tumaini kwamba angepata nafasi ya kuuona mchezo huo mkubwa duniani pamoja na kuweza kukutana na wachezaji.

Kibahati bahati, Rodriguez alifanikiwa kufika kwenye uwanja wanaofanyia mazoezi Real -Valdebebas training complex mara baada ya kufika Spain, akiwa na mpango wa kuwaona mashujaa wake wakiwa kwenye maandalizi ya mechi.

Hakuwa na namna yoyote ya kuweza kuruhusiwa kuonana nao, ingawa miezi michache zilizopita alifanya ya bila malipo kama kijana muokota mipira (ball boy) wakati Real Madrid wakiwa kwenye pre-season huko California, lakini hilo halikuwafanya walinzi wamruhusu kuwasogolea wachezaji wa Madrid.

Akiwa hana shilingi, hana pa kwenda huku matumaini ya kuwaona mashujaa wake kwenye El Clasico,Rodriguez alikuwa amejikalia pembezoni mwa barabara kwa takribani masaa matano - then miujiza ikatokea.

Rodriguez aliyezunguzishiwa duara akiwa ndani ya Old Trafford na Cristiano Ronaldo

'Ilikuwa ni miujiza nilimuona yule kijana,' Mourinhoanakumbuka kwa kuwaelezea Sports Illustrated. 'Nilimuona Abel akiwa amekaa pembezoni mwa barababa nje ya uwanja wa mazoezi.
'Nilikuwa naondoka kwenye gari la msaidizi wangu Rui Faria, na kulikuwa na watu wengi nje, lakini nikwambia Rui asimamishe gari, "Simamisha gari - ni yule kijana wa Los Angeles".'
'Amigo! fanya nini hapa?? Mourinho alimuuliza Abel akiwa ndani ya gari.
'Nimekuja kuwatembelea nyie,' Abel Rodriguez alijibu. 'Ni mara yangu ya kwanza kujs ulaya, na ndoto yangu ilikuwa kuja kuona mechi zenu. Hasa El Clasico.'
'Lakini zimeshaisha zote,' Mourinho alisema. 'Unaishi wapi sasa??'
'Sijafanya chochote kuhusu jambo hilo,' Mmexico akajibu. 'Kipaumbele changu kilikuwa ni kuwaona nyinyi halafu ningepanga mipango yangu. Kama nisingewaona - ningeenda uwanjani kujaribu kupata tiketi. Na kama hilo lisingefanikiwa basi ningerudi nyumbani.'

Then Mourinho akaamua kumpangia Rodriguez ambayo Real walikuwa wanakaa kujiandaa na mchezo dhidi ya Barcelona na akampa tiketi ya VIP.

Lakini Mourinho hakuishia hapo.
Duties: Rodriguez helped lay out the Real Madrid strip before their Champions League tie at Old Trafford
Rodriguez aliwasaidia Real Madrid kuvaa jezi hizi kwenye mechi ya mtoano ya Champions League pale Old Trafford

Wakati wa chakula cha usiku kuamkia siku ya Clasico, Mourinho akampa ofa rafiki yake mpya Rodriguez ya kuwa mmoja ya wafanyakazi wa Real - kama mtunza vifaa wa muda wa Los Blancos - wakati zikiwa zimebaki siku mbili kupambana na Manchester United.

Mourinho alisema: 'Nilimwambia hakuna namna angerudi nyumbani kwao, nikamwambia nitaenda nae jijini Manchester akafanye kazi kama mtunza vifaa vyetu. Nilimwambia atusadie kwa mechi hiyo na atapata nafasi ya kushuhudia mechi kubwa ya ligi ya mabingwa wa ulaya ndani ya Old Trafford.'
Rodriguez alirudi chumbani kwake na kuchukua passport yake ili maandalizi ya kazi yake mpya yaanze kufanyika. Kwa kufurahishwa na kilichotokea akaanza kulia katika meza ya chakula waliyokaa wachezaji wa Madrid.

Siku chache baadae, alikuwa ndani ya Old Trafford, akiwa amevaa sare rasmi ya Real na akiwapangia jezi wachezaji ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo.

Celebration time: Rodriguez also saw his beloved Real Madrid beat Barcelona in the Clasico at the Bernabeu
Rodriguez alipata nafasi ya kuiona timu yake ya Madrid ikishinda dhidi ya Barcelona kwenye el clasico ndani ya uwanja wa Bernabeu

Baada ya ushindi uliozua utata ndani ya Old Trafford, Rodriguez akijikuta ndani ya chumba cha Manchester United akikusanya jezi za wachezaji wa United zilizosainiwa na wachezaji wenyewe na akafanya hivyo pia kwa upande wa wachezaji wa Madrid.
Pia aliagizwa na Sir Alex Ferguson akamwite Mourinho kwa ajili ya utamaduni wao wa kunywa mvinyo kila baada ya mchezo unaowakutanisha.

Rodriguez alirudi nyumbani kwao LA na jezi zilizovaliwa na wachezaji kama Javier Hernandez, Mesut Ozil, Kaka na Michael Essien, na mmoja wa mpira uliochezewa siku hiyo.

Akikumbuka wakati akimuaga mkewe aitwaye Olga na watoto wake watatu wa kike huko LA wakati akija ulaya kujaribu kuiona timu yake aipendayo, Rodriguez alisema: 'Nilikuwa na mashaka sana juu ya kwenda ulaya, lakini ushawishi mkubwa ulikuja kutoka kwa mke wangu, ambaye aliniambia, 'Inabidi uende. Imekuwa ndoto yako kwa muda mrefu.'

KIBEGA SASA ATEMBEA NA BAUNSA WAWILI

KIBEGA

Msanii wa muziki wa kizazi kipya toka mtwara Rahim a.k.a Kibega (dume la shida) jana ameshindwa kufanya shoo alipotakiwa kupafom kwenye tamsha la Pepsi baada ya cd ya ngoma yake kushindwa kucheza kwenye mashine ya dj

Baada ya cd hiyo kugoma kucheza kwenye mashine hiyo ndipo alipotakiwa kuimba kwa kutumia beat ya nyimbo nyingine ya nje ambapo kibega alikataa kwa madai kuwa atakuwa anaendelea kuwatukuza wanamuziki wakubwa mpaka lini wakati yeye ana ngoma zake na zinafamnya poa kwenye radio na tv station

Ishu nyingine klwa kibega ni pale alipopata wakati mgumu licha ya kutokuimba ila baada ya kushuka jukwaani ndipo alipofuatwa na mashabiki wake wakitaka awaachie namba za simu kitu ambacho ilimlazimu kibega awe chini ya mabaunsa wawili kuhofia kuporwa vitu vyake na mashabiki wake hao

Swiraty blog ilipiga story na kibega kuhusu tukio hilo ambapo kibega alisema kuwa hali hiyo imetokana na kupendwa kwake na mashabiki wake hao ambao hawajamuona mda mrefu akifanya shoo

NATURE AKATISHWA INTERVIEW YA TELEVISHENI KISA KAVAA NDALA

JUMA NATURE

Msanii mkongwe na maarufu nchini, Juma Kassin Kiroboto, aka Nature, ameonyesha kukerwa na kile kilichoendelea jana usiku katika kipindi cha burudani cha televishen inayotizamwa africa ya mashariki alipokuwa akifanya nao interview. Nature alionekana akiwa amevaa kawosh na ndala na mara baada ya mahojiano mafupi ya mwanzo ambapo mtangazaji alisema watarejea baada ya mapumziko mafupi Nature hakuonekana tena. Kilichotokea kwa mujibu wa Nature mwenyewe, ni wakati wa mapumziko hayo, mtangazaji wa kipindi hicho alimfata na kumuambia kuwa hataendelea na interview tena kwasababu ya mavazi aliyokuwa kavaa ambayo ni ndala na kawosh. kuonyesha kukerwa kwake na ishu hiyo Nature aliamua kuandika kupitia ukurasa wake wa facebook....

Juma Natur Kibla
hivi kwa mfano angekuwepo mzungu pale na kavaa ndala wangesitisha mahojiano na kuvaa kaoshi ni tatizo,kunywa nimekunywa bt kuna baya nimeliongea na hivi kama kweri we nimuandishi wa habari unaruhusiwa kuvaa vile kisheria kama yule mtangazaji nimeboreka kinoma na ikiwezekana nasitisha kuanzia ssa kupeleka ngoma zangu pale siitaji interview

Wednesday, February 20, 2013

YANGA YAENDELEA KUANDAA DOZI YA AZAM

.
yanga wakiwa mazoezini(picha na maktaba)
 
kikosicha Young Africans leo asubuhi kimeendelea na mazoezi katika uwanja wa Mbegani nje kidogo ya mji wa Bagamoyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wake dhidi ya timu ya Azam Fc siku ya jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Young Africans ambayo imeweka kambi katika hoteli ya Kiromo - Bagamoyo tangu jana mchana kujiandaa na mchezo huo, leo asubuhi imefanya mazoezi chini ya kocha mkuu Brandts, kocha msaidizi Fred Felix 'Minziro' na kocha wa makipa Razaki Siwa huku wachezaji wote wakiwa katika hali nzuri kiafya na kiakili kuelekea katika mchezo wa jumamosi.

Kikosi cha mholanzi Ernest Brandts kinaonekana kuwa kwenye hali nzuri na wachezaji wote wanaoekana kuwa kwenye ari ya mchezo huo wa jumamosi kwani mechi hiyo ndio itakayotoa taswira ya msimamo wa Ligi Kuu kuelekea katika mbio za kutwaa Ubingwa.


Young Africans ambayo katika mchezo wake wa mwisho iliibuka na ushindi wa jumla ya mabao 4-0 dhidi ya timu ya African Lyon huku safu ya ushambuliaji wa timu ya Yanga ikionekana kuwa na uchu wa kucheka na nyavu katika kila mchezo.

Akiongea na www.youngafricans.co.tz Brandts amesema kikosi chake kipo katika hali nzuri, mazingira ya kambi ni mazuri, wachezaji wanapata fursa ya kukaa pamoja na kushiriki mazoezi kwa pamoja katika hali ya utulivu hali inayongeza umakini katika kuelewa maelekezo yake
 
Najua macho na masikio ya wapenzi wa soka nchini yansubiri kuona nini kitatokea siku ya jumamosi, ukweli ni kwamba huo ni mchezo muhimu sana kwetu ili kujijweka katika hali nzuri ya kuendelea kuongoza ligi , hivyo nachoweza kusema ni kwamba nimekiandaa kikosi changu ili kiweze kuibuka na ushindi katika mcheo huo siku ya jumamosi 'alisema Brandst'

Aidha Brandts alisema anafarijika kuwa na wachezaji wake wote 26 kambini kujiandaa na mchezo huo wa jumamosi, wachezaji wote wapo safi kiafya, kiakili na morali ya kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo huo, hivyo nashukuru kuwa fit kwa kikosi changu chote nitapata fursa ya kumtumia yoyote kati yao

Young Africans inaongoza msimamo wa VPL kwa kuwa na pointi 36 huku ikiwa imecheza michezo 16, imeshinda jumla ya michezo 11, imetoka sare michezo mitatu (3) na kupoteza michezo miwili (2) huku ikiwa imefunga jumla ya mabao 33 na kufungwa mabao 12 tu.


Nafasi ya pili inashikiliwa na timu ya Azam FC yenye pointi 33 ikiwa na mabao 27 ya kufunga na ikiwa imefungwa mabao 14 ambayo leo inashuka dimba la chamanzi kucheza na timu ya JKT Ruvu katika muendelezo wa michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom.

MALKIA WA NYUKI AMALIZANA NA MILLOVAN

Rahma Al Kharoos

Na idrisa bandali
MFADHILI wa Simba SC, Bi Rahma Al Kharoos, amejitolea kulipa malimbikizo ya mishahara ya miezi mitatu ya aliyekuwa kocha wa klabu hiyo, Mserbia, Profesa Milovan Cirkovick, dola za Kimarekani 24,000 (kiaisi cha Sh Milioni 40,000).
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mchana katika hoteli ya Movenpick, Dar es Salaam, Rahma maarufu kama Malkia wa Nyuko, amesema kwamba amejitolea kumlipa kocha huyo kwa mapenzi yake kwenye klabu hiyo na kwa kuwa pia aliitumikia klabu, hivyo anadai haki yake.
“Sasa hivi kuna matatizo mengi, kwa hiyo timu haifanyi vizuri, wanachama hawajui waangalie nini, waaangalie matatizo ya kocha aliyetoka anadai fedha zake, au waaangalie timu kwa nini haifanyi vizuri,”alisema.
Alisema umefika wakati Simba lazima waondokane na hali hiyo na katka hilo, amesema hakuna haja ya kuoneana haya wala kuogopana.
“Nafikiri watu wengi wanasema kama mimi naweza kuburuzwa, mimi siburuziki, mimi nasema ukweli, kama tatizo lipo litatuliwe,”alisema.
Mama huyo ameshauri matatizo ndani ya Simba yaanze kutatuliwa kuanzia ndani ya uongozi, akiwashauri wakae chini na kutafuta suluhisho la muda mrefu.
“Siyo mambo ya kuzima zima moto, au mambo ya kuweka weka viraka, kama hili tatizo la kocha, ni la kukaa tu na kocha mwenyewe na kulitatua. Lakini mtu wao wenyewe wamemuita, amefika hapa wanamkwepa, akianza kusema sema maneno, kosa litakuwa la nani, kosa litakuwa la uongozi dhahiri.
Mimi nasema, nitalitatua hili tatizo, nitampa kocha fedha zake kwa sababu ni haki yake. Mtu katoka kwao kule, amekwishawafanyieni kazi, mpeni haki yake, ya nini mnamzungusha? “alihoji Malkia wa Nyuki.
Aidha, Malkia wa Nyuki amekana dhana kwamba yeye anaburuzwa ndani ya Simba, akisema; “Kwa hiyo mimi nasema, nawaambia watu wa Simba, hamna mtu anayeniburuza hapa, wala siogopi mtu, kitu kinachotakiwa tuanze kujisafisha,”alisema.
Amelaani kitendo anachofanyiwa Milovan, akisema inawezekana klabu hiyo ikamuhitaji tena baadaye, hivyo halitakuwa jambo zuri kuharibu uhusiano naye.
“Kwa hiyo ninamuomba msamaha kocha kwa matatizo yote, amenipa data zake za benki, nasafiri leo, nataka acheki akaunti yake Jumatano atapata fedha zake,” alisema.
Pamoja na hayo, Mama huyo amesema hakuridhishwa na kiwango cha timu, ambayo sasa iko chini ya kocha Mfaransa, Patrikc Liewig katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Recreativo de Libolo ya Angola, siku ambayo Wekundu hao wa Msimbazi walilala 1-0 nyumbani.
Simba ambayo ina makocha wasaidizi watatu, wazalendo Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na James Kisana na Mganda, Moses Basena sasa inatakiwa kushinda 2-0 ugenini wiki ijayo ili kusonga mbele kwenye michuano hiyo.
Milovan alitimuliwa Simba SC baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Novemba mwaka jana timu hiyo ikishika nafasi ya tatu nyuma ya Yanga, inayoongoza hadi sasa na Azam inayoshika nafasi ya pili hadi ya sasa.