Friday, August 2, 2013

Iangalie na isikilize pia Hotuba ya Mwezi Julai 2013 ya Rais kikwete


Kiiza amalizana na Yanga aweka saini Mkataba wa Miaka miwili

HATIMAYE mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Hamisi Friday Kiiza ‘Diego’ amesaini Mkataba wa miaka miwili usiku huu kuendelea kuichezea klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam.
Majemedari watatu wa Kamati ya Mashindano ya Yanga SC inayohusika pia na masuala ya usajili, Mwenyekiti Abdallah Bin Kleb na Wajumbe wake, Isaac Chanji na Mussa Katabaro wamemaliza kazi hiyo usiku huu.
Zoezi lilifanya katika eneo la bwawa la kuogelea kwenye hoteli ya Protea, Dar es Salaam na Kiiza Jumapili atavaa tena jezi ya Yanga kuichezea kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Taifa.  
Kiiza alitua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam majira ya Saa 12 jioni na moja kwa moja kwenda kumalizana na Yanga.
Hii ilikuwa mara ya tano, Kiiza anakuja Dar es Salaam kwa ajili ya suala la kusaini Mkataba na mara nne zote za awali, alishindwa kuafikiana na uongozi wa klabu hiyo akarejea Uganda, mara ya mwisho ikiwa ni wiki iliyopita.
Awali, mara tu baada ya Ligi Kuu, Yanga ilifanya mazungumzo na mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda, hawakufikika makubaliano akaondoka. Mara ya pili, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Mussa Katabaro akapanda ndege Uganda kuzungumza naye, wakafikia makubaliano akamtumia tiketi aende Dar es Salaam.
Kwa kusaini Yanga, Kiiza anakuwa mchezaji wa nne katika orodha ya wachezaji wa kigeni baada ya beki Mbuyu Twite, kiungo Haruna Niyonzima wote kutoka Rwanda na mshambuliaji Didier Kavumbangu wa Burundi, hivyo klabu itabakiza nafasi moja.
Yanga SC sasa inaendeleza mapambana yake na watani Simba SC katika kuwania saini ya Mganda mwingine, Moses Oloya ambaye anamaliza Mkataba wake na Saigon Xuan Thanh ya Vietnam mwezi huu, Agosti

(Habari hii ni mali ya Bin Zubeiry)

Kazimoto asaini dili la mwaka mmoja umangani aliko




ALIYEKUWA kiungo wa Simba Mwinyi Kazimoto jana amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu kwa ajili kuitumikia klabu ya Al Markhiya SC ya Doha, Qatar.
Habari za uhakika kutoka Qatar zinaeleza kwamba, Kazimoto amesaini mkataba baada ya kufaulu majaribio yake, sambamba na kukubaliana na uongozi ofa aliyopewa.
Imeelezwa kwamba, hatua ya Kazimoto kusaini mkataba huo imekuja baada ya uongozi wa timu hiyo kuongeza dau la kumnunua baada ya awali kugomea kwa madai kuwa halilingani na thamani waliyomnunulia.
Chanzo hicho kimeeleza kwamba, Al Markhiya iliwaangukia Simba kwa dau waliloafikiana kutokana na ukweli kwamba kwa sasa ipo katika hali mbaya ya kifedha na hasa ikizingatiwa kuwa wanahitaji kusajili wachezaji watakaoipandisdha tena daraja.
“Unajua timu imeshuka daraja hivi karibuni sasa wanajiimarisha kwa kusajili wachezaji wazuri na fedha waliyonayo haitoshelezi hivyo wameiomba Simba ipokee hicho walichonacho,”kilieleza chanzo hicho.
Juzi uongozi wa Simba kupitia kwa msemaji wake Ezekiel Kamwaga ulisema umeitupilia mbali ofa iliyotumwa na klabu hiyo kwa madai kuwa ni ya kipuuzi, huku ikidai pia Kazimoto ana maswali kwanza ya kujibu kwa Watanzania na mashabiki wa Simba kwa ujumla.
Simba pia ilidai inakusudia kuketi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya kumjadili nyota huyo kwa kitendo chake cha kutoroka nchini.

Kazimoto ambaye alisajiliwa na Simba mwaka juzi kutokea JKT Ruvu, alitoroka nchini akiwa na timu timu ya Taifa iliyokuwa ikijiandaa na mechi yake ya kufuzu fainali za Afrika zinazoshirikisha nyota wanaocheza ligi za ndani (CHAN) dhidi ya Uganda ‘The Cranes’

Kesi ya jinai inayomkabili muigizaji Wema Sepetu, ya tuhuma za kumpiga vibao vitano meneja wa hoteli ya Mediterano , pamoja na kuharibu mali za hoteli hiyo, imeahirishwa leo hii pia mpaka tarehe 20 mwezi wa nane.

sakata hilo lilitokea siku ya tarehe 4 mwezi wa 4, kesi yake ya kwanza ilisomwa siku ya tarehe 17, na kuahirishwa mpaka leo hii, na baada ya kufika mahakamani leo hii na Wema kukataa mashtaka hayo, kesi imeahirishwa tena mpaka tarehe 20 mwezi wa 8.


"Siku ya kwanza ya keshi hiyo wanaume walikuwa wengi, lakini leo hii imekuwa tofauti, wasichana walikuwa wengi yaani marafiki zake wakiongozwa na Kajala, walifika majira ya saa mbili na robo na waliitwa sehem maalum (chemba) kwa ajili ya kusikilizwa kesi hiyo, na keshi hiyo ilisomwa ila ilihairishwa mpaka tarehe 20/08/2013" amesema Mwahija (mwandishi wa habari wa kujitegemea).

Dimpoz kukamua bujumbura......




Ommy Dimpoz, mkali ambaye anafanya poa sana katika tasnia ya Bongofleva Afrika Mashariki, anatarajia kuweka historia huko nchini Burundi katika sikukuu ya Eid El Fitri katika shoo kubwa ambayo inasubiriwa kwa hamu na wapenzi wa burudani nchini humo.

Ommy Dimpoz pamoja na timu nzima ya Poz Kwa Poz, katika onyesho hili watakuwa pia na sapoti ya wasanii wa nchi hiyo , Mkombozi, Happy Famba, Rally Joe, Mac Dady, Bengo Star na wengineo.

Msanii huyu pia siku ya leo imekuwa ni ya kipekee kwake baada ya ngoma yake mpya aliyoifanya na J Martins kutoka Nigeria kutoka leo rasmi na kuanza kupendwa na watu

Wednesday, July 31, 2013

Iangalie hapa Speech ya Mwl Nyerer ya mwaka 1995


Ngoma azipendazo Swiraty kuzitizama


Joh na Niki kupimana



Baada ya kuwa na ubishi wa muda mrefu kati ya marapa wawili ambao ni ndugu Joh Makini pamoja na Niki wa Pili juu ya nani ni mkali zaidi kati yao, wakali hawa sasa wameamua kumaliza ubishi kwa kutengeneza kazi ya pamoja ambayo mwisho wa siku utaleta majibu kuwa ni nani anaweza zaidi.

Hii itakuwa ni kupitia albam ya pamoja ambayo itatoka hivi karibuni ambayo Niki na Joh watakuwa wakijipimia uwezo ndani yake na kuwapatia mashabiki nafasi ya kuamua mshindi wenyewe, ambapo hivi sasa tayari wametanguliza zawadi ya ngoma mpya ya pamoja inayokwenda kwa jina Bei ya Mkaa.

Albam hii ambayo tayari imekwishaanza kushughulikiwa, ni moja ya kazi ambayo mashabiki wa wasanii hawa kwa sasa watakuwa katika hamu kubwa kutaka kuisikia, na inatarajia kuweka historia mpya katika gemu ya burudani na itakuwa imekamilika baada ya miezi miwili kutoka hivi sasa.

Albam hii kwa mujibu wa Niki wa Pili, Itazinduliwa kwa Tour kubwa na kuwasilishwa moja kwa moja kwa mashabiki ili kupima wenyewe ni nani mkali hasa kati ya yeye na Joh.

Zisome hapa Tweets 4 za Mbunge wa kawe Halima Mdee akizikemea dawa ya kulevya


Mbunge wa Kawe kupitia Chama cha Demokrasia Chadema ameonekana kuzidi kufedheheshwa na uingizwaji wa madawa ya kulevya na biashara hiyo kuzidi kushamili 
nchini kwa kasi sana....


Aidha hivi karibuni binafsi wenyewe tumeweza kusikia na kushuudia watanzania wakikamatwa ughaibuni na hata wengine kufa kutokana na kumeza kete hizo na wengine kufungwa....

Hali hii naona ndio inayomchosha na kumuumiza Mbunge Halima Mdee na hizi ndizo
Tweets zake kupitia mtandao wake wa Tweeter  alizotupia kufunguka Live kuhusiana na Madawa hayo na kukemea vikali

Soma kilichomkuta Madee alipotua Zanzibar

1

Kwa takribani yapata wikii mbili sasa tokea tuhuma za  madawa ya kulevya kushamili
nchini hususani watanzania wanojishugulisha na maswala hayo....



Karibuni kulizuka tuhuma ambazo za kweli kwa watanzania kukamatwa na madawa
ya kulevya nchini Afrika ya kusini na hii inaleta mtafaruku ya ushirikiano wa baina ya
nchi na nchi...

Msanii Madee kutoka Tip Top cinnection jana aliwasili nchi Afrika ya kusini na alivyowasili anasema alivyojulikana anatoka Tanzania  aliwekwa pembeni kwa takribani zaidi ya saa 1 na kusachiwa kuojiwa sana baada ya hapo kuruhusiwa kuondoka
uwanjani hapo...

Anasema baaada ya kutaja anatokea Tanzania walikuwepo  askari waliovalia sare walimuamuru kuvua tshirt na kubakia na nguo nyepesi ya  ndani hadi kumkagua mabegi yake huku abiria aliokuwa amesafiri nao ndege moja walipita bila matatizo yoyote...

Sehemu yenyewe ambayo alivuliwa nguo sio kwenye  chumba maalumu ilikuwa pale pale  kwenye mstari,lakini baada ya ukaguzi  walimomba msamaha na kumruhusu kuendelea na safari yake....!!

Monday, June 17, 2013

kinachoendeleela wakati wa kuaga mwili wa Langa

Baba yake Langa

kaka yake Langa


langa
Yanayoendeleela kwenye kwenye Msiba wa Langa wakati huu wa kuaga kwa hisani ya Salehejembe.blogsport.com

Wednesday, May 22, 2013

Sajna arudi tena

Sajna

Baada ya kutamba na ngoma kali kama Iveta,Sitaki tena kuumizwa na Mganga,msanii kutoka pande za mwanza Rock city Sajna anakuja na Ningekuwa Single.

Kwa muda fulani Sajna amekuwa kimya katika Tasnia ya Bongo fleva na kuwaacha wakali wengine kutoka pande za Mwanza kuwakilisha vilivyo akiwamo C-Sir Madini kwa wasanii wanaoimba huku wakali wengine kutoka pande hizo katika Hip Hop waliendelea kuwakilisha Jiji la Mwanza akiwamo Young Killer mzee wa Dear Gambe.

Sajna ameamua kudondosha wimbo huo mwanzoni wa mwezi wa Sita aliowashirikisha wakali wa R&B Ben Paul pamoja na C-Sir Madini, kwa mujibu wa Sajna amekili kutowaangusha Fans wake kabsaa katika ngoma hiyo iliyounganisha vichwa vitatu vya R$B.

“Zimebaki siku chache naachia wimbo wangu mpya itakuwa mwezi wa 6 ni wimbo wa mapenzi ambao nimewashirikisha BEN POL na jembe langu C-SIR MADINI...Sisemi mengi mtakuja kujaji wenyewe ila nachoweza kusema sijawaangusha,Niamini mimi sijawaangusha!”

Man Water ajipanga kwa ushindani

walter

Kutokana na hatua ya watayarishaji wengi wa muziki wa Bongo ambao wamekuwa kwenye gemu kwa muda mrefu kufikia kipindi na kukaa kando, jambo linalowasababisha watu kufikiri kuwa wanakimbia ushindani na vitu kama hivyo, eNewz imeongea na Hit Maker Prpdyuza Man Water

kuhusiana na mtazamo kwa hali hii na iwapo yeye nae ana mpango wa kustaafu kutengeneza muziki.

Mkali huyu ambaye amekiri kuwa hatua hii haikwepeki, na amesema kuwa hataachia ngazi kwenye kutengeneza muziki kirahisi na sasa tayari ameshaanza kuwatengeneza watayarishaji chipukizi wa muziki ambao watakuja kuendeleza kazi yake katika studio ya Combination Sound

Vilevile Producer huyu ambaye ngoma aliyotengeneza ya Joto Hasira yakwake Lady Jay Dee fy Prof Jay inafanya poa sana kwa sasa amesema kuwa, ni kweli katika music production Tanzania kwa sasa, kuna vipaji vingi na watayarishaji wengi chipukizi, lakini kwa maoni yake ni wachache sana anaowaelewa na wamekuja na kitu cha tofauti.