Tuesday, September 17, 2013

Shetta achukia baada ya kukaguliwa kama jambazi uwanja wa Ndege Zanzibar

Shetta na Chege wakikaguliwa Uwanja wa Ndege wa Zanzibar
Msanii Shetta ameonekana kukerwa na kitendo cha kukaguliwa begi lake  na kutoa kila kitu kilichokuwa ndani ya begi lake kwa ajili ya kukamilisha ukaguzi huo, katika uwanja wa ndege wa Zanzibar akisafiri kuelekea Mombasa akiwa na msanii mwenzake kutoka kiumeni "Chege"
Kutokana na matukio ya watanzania wengi kujihusisha na usafirishaji wa madawa haramu ya kulevya, serikali imekuwa makini sana kwa wasafiri wanaotumia usafiri wa anga kutoka na kuingia ndani ya nchi, kuhakikisha hakuna kila anaejihusisha na kazi hiyo kufikishwa katika mikono ya sheria.

Mcheki hapa Balozi wa China akiwa na Kofia ya CCM







Matokeo ya Mechi za UEFA yako hapa

Photo: Matokeo Champions League

DKT. Kawambwa azindua Mradi wa Maji Kunywa Kerege Bagamoyo

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt Shukuru Kawambwa (wa tatu kushoto) akikata kamba kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi ya kunywa katika shule ya msingi Kerege Bagamoyo

 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt Shukuru Kawambwa(katikati) akigonganisha vikombe na wanafunzi wa shule ya msingi Kerege Bagamoyo pamoja na Raisi wa Daressalaam Rotary Club,mwenye miwani bi Nadine Atallah kama ishara ya kufurahia huduma ya maji safi katika shule hiyo. Klabu hiyo ndio imeligharamia mradi huo.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt Shukuru Kawambwa(katikati) akinywa maji mara tu baada ya kuzindua mradi wa maji safi ya kunywa katika shule ya msingi Kerege Bagamoyo, kushoto ni Raisi wa Daressalaam Rotary Club bi Nadine Atallah. Klabu hiyo ndo wadhamini wa Mradi huo. Wengine ni wanafunzi wa Shule hiyo.

Tuesday, September 3, 2013

Urban Boys yapata Dili Ubelgiji



Ni kundi ambalo hivi sasa limekuwa likishika headlines mbalimbali Afrika Mashariki si wengine bali ni The Urban Boys kutoka nchini Rwanda Kigali ambao hivi sasa wamepata bonge moja la shavu la kusafiri kuelekea nchini Ubelgiji kutumbuiza katika tukio la kumtafuta Miss and Mister Rwanda/Belgium 2013.

Ni wiki chache zilizopita kundi hilo lilitangazwa kuwa washindi wa shindano kubwa la kutafuta nyota wa muziki nchini humo la Super Star Season Three ambapo mmoja wa memba wa kundi hilo anayeitwa Safi Niyibikora, aka Safi Lee, ameelezea kufurahi sana kupata nafasi hiyo ambayo itawapa fursa ya kuweza kujitangza zaidi kimataifa.


Shindano hilo linatarajiwa kufanyika huko Brussels, Belgium tarehe tano mwezi Oktoba mwaka huu huku ikiwa ndio mara yao ya kwanza kabisa kutumbuiza nchini humo na barani Ulaya japokuwa wamekuwa wakipata mashavu kadhaa ya kutumbuiza Afrika Mashariki.

Huyu Ndiye Ktibu Mkuu Mpya wa Yanga anayechukua Nafasi ya Mwalusako

Naggi

Anayetarajiwa kuchukua nafasi Lawrence Mwalusako ni Patrick Naggi amewahi kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF).

Tayari Naggi ambaye aliwahi pia kuwa CEO wa Tusker ya  Kenya yuko nchini kumalizia mazungumzo na Yanga ili kuchukua nafasi na katibu mkuu Yanga.

Lakini taarifa zinasoma, Naggi aliwahi kufukwa kazi katika KFK kutokana na upotevu wa mipira 100.

Hata hivyo, mwenyewe aliwahi kulalamika kwamba mipira hiyo iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) haikuwa katika kiwango hicho.


Aidha, Naggi aliwahi kulalamika kwamba hakupewa nafasi ya kujieleza kutokana na kilichotokea.

Mwalusako aachia Ngazi Yanga wanachama waitisha Mkutano na Waandishi wa habari leo



Katibu Mkuu Yanga, Lawrence Mwalusako ameamua kuachia ngazi baada ya kukaimu kwa mwaka mmoja.

Mwalusako amesema amefanya hivyo kwa kuwa makubaliano yao yalilikuwa ni kukaimu nafasi hiyo kwa mwaka mmoja.

“Haya ndiyo yalikuwa makubaliano yetu na sasa muda mwafaka umefika wa kufanya hivyo,” alisema hivi punde.

Lakini uchunguzi wa Blog hii umeonyesha kuwa Yanga imeleta Mkenya kuchukua nafasi yake hiyo na tayari ameanza kazi.

Mkenya huyo anajulikana kwa jina Patrick Naggi kuchukua nafasi hyo.


Taarifa hizo zinaaleza Naggi amewahi kuwa Technical Director wa Shirikisho la Soka la Kenya (KFF) na CEO wa Tusker ya  Kenya.

Huyu Ndio Diamond my number one iangalie hapa


Tazama hapa Picha za Matuki ya Kumbukumbu ya Mwaka Mmoja ya Mrehemu Daudi Mwangosi kwa waandshi wa Mtwara

picha ni kwa hisani ya eliamigongo.blogspot.com

ASKOFU LUCAS MBEDULE






Mwenyekiti wa Mtwara Press club, HASSAN SIMBA, wwakati akitoa neno la shukurani.








Tuesday, August 20, 2013

Picha 3 Tofauti zilizomvutia Swiraty Asubuhi ya Leo

idrisa bandali

Saida Mussa

mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari Mkoani Mtwara Hassani Simba
Nawe unaweza kutuma picha zako zilizotolezea ili uwepo katika shwangwe na swiraty Blog

Mtangazaji wa Kipindi cha Ukurasa Upya Info radio atoa Ngoma yake "MY BUU"

Aloycea Ngunyali
Mwanadada mwenye uwezo wa kuvutia wasikilizaji akiwa kwenye Kipindi Chake cha Ukurasa Mpya kupitia Info Radio ALOYCEA NGUNYALI ametoa Single nyingine inayokwenda kwa jina la MY BUU safari hii Single hiyo imepikwa kwa Produza Sully wa 29 Record ya Mtwara

Swiraty Bloy ilipopiga Story na mwana dada huyo mahili ktika tasnia ya utangazaji Mkoani Mtwara amesema ameamua kuto wimbo huo kwa kuwa yeye anapenda sanaa tangu mda mrefu na imekuwa ni muendelezo wa kile anachokipenda 

Itakumbukwa pia kuna filamu amewahi kucheza madad huyo akiwa chuoni na nyimbo hii imekuwa ya pili kwae kuitoa 

'Naomba wadau wangu waipokee ngoma yangu ili wajue n upande wa pili ninauwezo gani wa kufanya kama ilivyo katika kazi yangu ya utangazaji" alisema Aloycea

Diamond Akanusha kuwa ni mmoja kati ya walioko kwenye mtandao wa madawa ya kulevya

Licha ya kutajwa kuwa ni mmoja kati ya wauza unga Nchi Msanii huyo ambae anasifika kwa kutoa ngoma kali zinazofanya puwa katika radio na Tv Station ameakanusha taarifa hizo na kueleza kuwa yeye ni kweli anapesa nyingi za kusihi maisha anayoyataka lakini pesa hizo zinatokana na kazi anayoifanya ya sanaa na siku zote mchumia juani hulia kivulini alisema diamond

Wednesday, August 14, 2013

Angalia hapa Picha za Fezza katika mapokezi yake Dar jana

Vanesa Mdee alikuwepo kumpokea Feza

Fezza akiwa amembeba mwanae wa kiume....
Baada ya kufanya yake ndani ya jumba la Big Brother the chase 2013,muda wake ullifikia tamati jumapili ya juzi baada ya kutolewa kwenye  jumba ilo nchini South Africa....


Familia ya Fezza ikimsubiri kijana wao
Baada ya Tamati hiyo kufika mdada huyo mwenye mvuto huyo kutoka nchini Tanzania siku ya jana amewasili nchini majira ya saa 1 jioni na kulakiwa na ndugu,jamaa na marafiki nzuri zaidi hata mtoto wake na mama yake mzazi  walifika uwanja wa ndege wa kimataifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kumpokea  sambamba wakiwa na kiongozi toka Multi choice Tanzania,Barbra.

Picha kwa hisani ya Millad ayo.com


Iangalie hapa list ya Wasanii watakaotoa Burudani Mwanza Jumamosi Agosti 17 Kili Music Tour 3013


Roma 
Kampuni ya bia ya Tanzania Breweries Limited (TBL) kupitia  bia yake ya Kilimanjaro  Premium  Lager, inang'oa nanga katika awamu ya pili ya tamasha lake kali za muziki la ‘Kili Music Tour 2013’ wikiendi hii Jijini Mwanza.


Tamasha hili  kubwa litafanyika jumamosi ya tarehe 17 Agosti, 2013 mjini Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba na litajumuisha wasaniii 11 ambao ni Diamond, Snura Mushi, Professor J, Lady Jay Dee, Roma, Dabo, Bob Junior, Ben Pol, Kala Jeremiah, Fid Q na AT.



Lady Jay Deee

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Meneja wa bia ya Kilimanjaro George Kavishe, matamasha ya Kili Music Tour 2013 yalikuwa yamepumzika kwa muda wa mwezi mmoja sasa, yanaendelea tena kwa kishindo kwenye mikoa mitano iliyobakia.


Bw. Kavishe ameeleza kuwa “Bia ya Kilimanjaro Premium Lager inaendelea kutoa bonge la kiburudisho kwa watanzania kwa kuhakikisha kuwa kila mkoa unapelekewa wasanii mahiri kabisa wa muziki wa Bongofleva hivyo mashabiki wa muziki wakae mkao wa burudani.

Tuesday, August 13, 2013

Haijawahi tokea angalia waumini wakiwa katika foleni kwenda kumuona shehe Ponda


                             Waumini wakisubiri kumuona Shehe Ponda Muhimbili alipolazwa