Monday, October 29, 2012

MILIONI 225 ZAHITAJIKA KUIPELEKA SERENGETI BOYS MOROCCO


Rais wa TFF, Tenga akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Kulia ni Sunday Kayuni, Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF na kushoto, Katibu, Angetile Osiah 


Na idrisa bandali


 RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chillah Tenga amesema kwamba timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys inahitaji zaidi ya Sh Milioni 225 kwa ajili ya kampeni yake iliyobakia ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika mwakani nchini Morocco.

Akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya TFF, Ilala, Dar es Salaam, leo Tenga alisema kwamba shirikisho lake kwa sasa halina fedha hizo, kwa sababu hiyo haina mdhamini, zaidi ya kutegemea misaada ya wadau.

Tenga alisema tayari Kamati ya Vijana ya TFF imekwishakutana kuweka mikakati ya kuiwezesha Serengti kushiriki vema kampeni hizo, ikiwemo kuunda Kamati ya kuisaidia timu hiyo.
Hata hivyo, Tenga hakuitaja Kamati iliyoundwa kwa sababu bado hawajazungumza na Wajumbe walioteuliwa.

Alisema kocha wa timu hiyo, Mdenmark Jacob Michelsen ameomba mechi za kujipima nguvu kabla ya kucheza na Kongo Brazaville kuwania tiketi ya Morocco na Kamati ya Vijana inahangaikia suala hilo kwa sasa.

Alisema tayari kuna mwaliko kutoka Botswana wa Serengeti kwenda kucheza, lakini kutokana na ukosefu wa fedha wanashindwa hadi sasa kutoa jibu.

Kikosi cha wachezaji 25 cha Serengeti Boys kipo kambini mjini Dar es Salaam tangu Oktoba 21, mwaka huu kujiandaa na mechi hiyo, ya kwanza ikichezwa nyumbani Novemba 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, wakati mechi ya marudiano itachezwa wiki mbili baadaye.

Tanzania imefuzu bila jasho hadi kufika hatua hiyo, baada ya wapinzani wake wa awali, Kenya na Misri kujitoa katika Raundi ya Kwanza na ya Pili.
Kama Tanzania itafuzu kushiriki Fainali hizo za mwakani, itapoza machungu ya mwaka 2005 walipofuzu kucheza Fainali za Vijana wa umri huo kwa kuzitoa Rwanda, Zambia na Zimbabwe, lakini baadaye kwa sababu ya ‘kufoji’ umri wa Nurdin Bakari, ikaondolewa mashindanoni.

Zaidi ya Fainali za Mataifa ya Afrika 1980 na CHAN 2009, katika soka ya wanaume, Tanzania haijashiriki fainali nyingine zozote za Afrika tangu iingie kwenye soka ya kimataifa.

Saturday, October 27, 2012

YANGA YAISHUSHA AZAM NAFASI YA PILI


Yanga SC



TIMU ya soka ya Yanga ya Dar es saslaam leo imeibuka na ushindi mwembamba wa goli 1 – 0 dhidi tim,u ngumu ya JKT OLJORO katika Mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani Mkoani Tanga
Goli pekee la Yanga hii leo limefungwa na Beki aliyezua Mtafaruku Mkubwa wakati wa Usahili wake baina ya Vilabnu viwili vikubwa hapa Nchini Simba na Yanga Mbuyu Twite
Goli hilo la leo la Mbuyu Twite linamfanay kuwa na mabao matatu aliyoyafunga tangua ajiunge na Timu hiyo yenye Maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani
Kwa Mtokeo hayo yah ii leo Timu ya Yanga sasa inakuwa imefikisha jumla ya point 20 huku Kinara wa Ligi hiyo Simba ya Dar es salaam akiwa na Jumla ya pointi 22 baada yah ii leo kitandika Timua Azam kwa goli 3- 1
Akiongea na Swiraty Blog Kocha Msaidizi wa Klabu ya Yanga Fred felix Minziro amesema kuwa Mchezo ulikuwa Mgumu tofauti na ilivotarajiwa na Ndio Maana wameshindwa kuibuka na ushindi Mnono hii leo

NDANDA YAAHIDI USHINDI KESHO


Timu ya soka ya Ndanda ya Mtwara Kesho inajitupa tena uwanjani kuwania Pointi Tatu muhimu katika Mchezo wa ligi daraja la kwanza dhidi ya Timu ngumu ya Green Worius katika uwanja wa Nangwanda Mkoani Mtwara
Akizugumza na Swiraty Blog Afisa habari wa Timu ya Ndanda Idrisa bandali amesema kuwa wamejiandaa kufanya vizuri kama ilivokuwa kwa mchezo wa mwanzo dhidi ya timu ya TransitCamp baada ya kuichapa goli 5 – 2
Amesema kuwa Wachezaji wote wako katika hali nzuri isipokuwa Mchezaji Mmoja tu Faraji Kambwili ambae anasunbuliwa na Mkono baada ya kuumizwa na goli kipa wa Tranist Camp Katika Mechi iliyopita
Bandali amesema kuwa hawana sababu ya kupoteza mchezo huo kwa kuwa timu yao itakuwa inacheza katika uwanja wao wa nyumbani wa nangwanda sijaona
“tunawaomba mashabiki waje kwa wingi kuishangilia timu yao ikiibuka na ushindi kesho kwani hatuna sababu ya kupoteza tukiwa katika uwanja wetu wa nyumbani ,tutahakikisha tunaibuka na ushindi kama ilivokuwa katika mchezo wa mwanzo dhidi ya Transit Camp” alisema Bandali
Katika Mchezo uliopita Timu ya Ndanda iliibuka na ushindi wa goli 5 – 2 dhidi uya Transit Cmp na baada ya mechi hiyo ya kesho  Timu ya Ndanda iasafiri kuelekea dar es salaam kwa ajili ya kucheza mechi tatu mfululuizo wakiwa nje ya uwanja wao wa nyumbani

Friday, October 26, 2012

AZAM KUISHUSHA SIMBA KILELENI LEO?


  Azam FC

Na idrisa bandali

Azam fc wamepania kuifunga Simba SC leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ili kupanda kileleni mwa ligi hiyo.
Kocha Boris Bunjak kutoka Serbia amekuwa akiwaandaa vizuri vijana wake kwa mazoezi na kisaikolojia pia kuelekea mchezo huo, unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua.
Azam ipo kambini kwake, Chamazi ikijifua vikali na wachezaji wameweka kambi hapo, kwa ajili ya Ligi Kuu.
Kiboko ya nyavu za Simba na Yanga, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ yuko fiti kupita maelezo na kiungo bora Afrika Mashariki na Kati kwa sasa, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ aliyekuwa majeruhi mwanzoni mwa msimu sasa amepona kabisa.
Kiungo Abdulhalim Humud aliyekuwa anasumbuliwa na maumivu katika mechi tatu zilizopita kwa sasa yuko fiti kabisa na habari njema zaidi ni kwamba, kiungo mwingine  Mzanzibari Abdi Kassim ‘Babbi’ amerudi kwenye fomu na anafumua mashuti makali na ya mbali ya hatari.
Viungo washambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tcheche na Kipre Michael Balou wote wapo fiti sawa na makipa Deo Munishi ‘Dida’, Mwadini Ally, mabeki Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Mourad na Aggrey Morris.
Kwa ujumla Azam iko tayari kwa mechi hiyo ya leo ambayo wamepania kushinda ili kulipa kisasi cha kufungwa na Simba katika Kombe la BancABC Sup8R.
Simba yenyewe inaendelea vizuri na kambi yake visiwiani Zanzibar kujiandaa na mchezo huo na inatarajiwa kurejea leo  mchana na moja kwa moja kuelekea uwanjani kukipiga.   

SIMBA KAMILI KUIVAA AZAM LEO TAIFA



Kikosi cha Simba
 Na idrisa bandali

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC wanatarajiwa kurejea Leo Dar es Salaam wakitokea Zanzibar ambako waliweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo wa wa leo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Taifa.
Pamoja na Juma Nyosso na Haruna Moshi kusimamishwa, lakini wachezaji waliobaki wana morali ya hali ya juu na wamepania kushinda mechi ya kwanza kati ya nne, baada ya sare nne mfululizo.  
Kwa kawaida Simba SC huenda Zanzibar katikati ya Ligi Kuu kuweka kambi linapokaribia pambano dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga SC lakini kwa kitendo cha kwenda kujichimbia huko kwa ajili ya Azam, maana yake wanaipa uzito huo mechi hiyo.
Simba ilienda Zanzibar Jumanne, siku moja baada ya kurejea kutoka Tanga, ambako ililazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji Mgambo JKT Jumapili katika mfululizo wa ligi hiyo.
Matokeo hayo, yaliifanya Simba ifikishe pointi 19, baada ya kucheza mechi tisa na kuendelea kuongoza Ligi Kuu.
Awali ya hapo, Simba ilitoka 2-2 na Kagera Sugar Uwanja wa Taifa na 0-0 na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani.
Baada ya sare ya Jumapili, Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage amewataka wanachama na wapenzi wa klabu hiyo kuwa watulivu na wasikatishwe na tamaa na sare tatu mfululizo za timu hiyo katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kwani safari bado ni ndefu.
Rage amesema kwamba, hadi sasa timu yao haijafungwa katika Ligi Kuu kuashiria kwamba bado ni timu bora na matokeo ya sare hizo tatu mfululizo pia ni kutokana na uimara wa timu yao.

Thursday, October 25, 2012

THE MOST CLASSIC COMBINATION KUANZA KUINGIZA SAUTI KATIKA NYIMBO YAO MPYA LEO

the most classic combinatinon leo watakuwa wanaanza kuingiza sauti katika nyimbo yao mpya ambayo bado haijapewa jina na mara hii inafanyika tena kwa produza mkali Jof Masta
Nyimbo hiyo imekaa kimahadhi ya klabu hivi na ni mfululizo wa ngoma mpya toka kwa the most classic combination ambayo iko chini ya mkurugenzi D Bravu
Baada ya voko hiyo leo ngoma hiyo itatambulishwa jumatatu katika vituo vyote vya radio hapa mtwara na nchini kote ambapo mafanzi wetu wako kibao huko kwa hiyo watu wakae mkao wa kula tayari kwa ngoma kali ktoka the most classic combination

PICHA MBILI ZA WATANGAZI WA INFO RADIO WAKITANGAZA MECHI KATI YA NDANDA NA TRANSIT CAMP KATIKA UWANJA WA NANGWANDA


Idrisa bandali wa info radio aliyevaa headphone akiwa na mzee hamisi mvulla kutoka info radio pia wakirusha matangazo hayo yam mpira

NDANDA YAWAPA FARAJA WAKAZI WA MTWARA

mtangazaji wa Info Radio akitangaza mechi hiyo moja kwa moja kutoka katika uwanja wa nangwanda akiwa sambamba na mwandishi mkongwe mzee hamisi Mvullla

Timu ya soka ya Ndanda ya Mtwara jana imeanza vema ligi Draja la kwanza katika kwa kuichapa timu ya soka ya Transit Camp baada ya kuichapa goli 5 - 2

Katika Mchezo huo ulikuwa mkali na wakusisimua ulianza kwa Timu ya Ndanda kuandika bao la mapema kunako dk ya 15 tu ya Mchezo liliwekwa kimani na Gaspol Pancholi bbaada ya kupiga adhabu iliyoweknda moja kwa moja katika wavu wa Transit Camp na kumuacha Golikipa Razak makene akiwa hana la kufanya
Kuingia kwa goli hilo kuliwafanya Ndanda kuongeza Ari ya Mchezo na kufanikiwa kuandika bao la pili lililowekwa kimani na Eliasi Ndokezi Kunako dk 35 ya Mchezo akimalizia kazi Nzuri ya Salumu Minel

Katika Mchezo huo wachezaji wawili wa TransitCamp waliineshwa kadi nyekundu kufuatia mchezo mchafu waliouonesha .wachezaji hao ni Golikipa Razak Makene na huseni Pandu
magoli ya Transit Camp yaliwekwa kimani kipindi cha kwanza na Prosper Mkwama na baadae Said salumu akaipatia timu hiyo y wanajehi goli la pili

Kipindi cha pili kila timu ilifanya mabadiliko ambayo yanlionekana kuisandia zaidi ndanda ambapo walifanikiwa kuandika mabao matatu yaliyowekwa kimani na Salumu Makongolo na elesi Ndiokezi
hadi mwamuzi Endru Shamba anapuliza kipenga cha mwisho Ndanda 5 na Transit Camp 2

Jumamosi Ndanda watatemka Tena katika uwanja huo wa Nangwanda kumenyana na Green worious katika mfululizo wa ligi daraja la kwanza