Thursday, June 14, 2012

MBUNGE wa jimbo la Iramba magharibi (CCM) mkoani Singida, Mwigulu Nchemba, anakusudia kuwasilisha hoja binafsi katika  bunge la bajeti linaloendelea juu ya kuanzishwa kwa baraza maalum litakaloshughulikia makosa ya uhujumu uchumi na vitendo vya rushwa.
Amesema amefikia uamuzi huo ambao amedai utasadia kwa kiasi kikubwa wananchi kuendelea kuiamini serikali yao , baada ya kubaini kuwa kesi zinazohusu vitendo hivyo, huchukua muda mrefu, mno kumalizika na kitendo hicho,huchangia watuhumiwa wengi kuachiliwa huru.
Akifafanua zaidi, amedai kuwa kuchelewa kumalizika kwa kesi hizo, hutoa mwanya kwa watuhumiwa kutoa rushwa ili sheria iweze kupinduliwa kwa manufaa yao .
Mwigulu ambaye pia ni Katibu wa fedha na uchumi wa CCM taifa, amesema kuachiwa kwa watuhumiwa wa makosa ya rushwa na uhujumu uchumi, kunachangia kuporomoka kwa maadili ya viongozi na wakati huo huo, wananchi kuichukia serikali yao.
Amesema mazingira ya usikilizaji wa kesi hizo yalivyo hivi sasa katika mahakama za kawaida, yanachangia kupunguza ufanisi wakati wa kuzishughulikia, kutokana na msongamano wa kesi katika mahakama hizo za kawaida.
Mwigulu amesema upo umuhimu mkubwa wa kuongeza adhabu ya makosa hayo ambayo itakuwa fundisho la kweli kwa wakosaji na kuwaogopa viongozi/wananchi wanaotarajia kutoa rushwa ua kuhujumu uchumi.

DOGO JANJA; UONEVU DHULUMA NA MATESO NDIO VILIVONIONDOA DAR ES SALAAM

WAZIRI WA FEDHA DK. WILLIAM MGIMWA AWASIL;ISHA BAJETI YA 2012/2013 MCHANA HUU BUNGENI


Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa akisoma bajeti ya Serikali  ya 2012/13, Bungeni Mjini Dodoma Juni 14, 2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa  akionyesha mkoba wenye Bajeti ya Serikali ya  2012/13 Bungeni Mjini Dodoma Juni 14, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Fedha Dk William Mgimwa akionyesha mkoba wenye bajeti huku akiwa ameongozana na Naibu Waziri Janet Mbene
Waziri wa Fedha,Dkt.William Mgimwa akiongozwa na Mpambe wa Bunge kuingia Bungeni kusoma Bajeti ya Serikali ya Mwaka  2012/13, Mjini Dodoma Juni 14, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wapiga picha wakigombea  picha  ya Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa  wakati aliponyanyua mkoaba wa Bajeti ya Serikali ya 2012/13, Bungeni Mjini Dodoma Juni 14, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Mabalozi wa Nchi mbalimbali  waliohudhuria Bungeni kusikiliza Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2012/13 iliyosomwa na Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa, Bungeni Mjini Dodoma Juni 14,2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda (kulia) akimsikiliza kwa makini Waziri ujenzi Dkt Jojn Pombe Magufuli(kushoto)(leo) wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwenye kikao cha tatu cha mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoendelea mjini Dodoma.PICHA NA VICENT TIGANYA WA MAELEZO
Naibu Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu , Tawala za mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI)  Aggrey Mwanri  akijibu maswali mbalimbali yaliulizwa na Wabunge katika kipindi cha maswali na majibu  (leo) mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA na Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mh. Freeman Mbowe akimuuliza Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda maswali ya papo kwa papo  (leo) mjini Dodoma katika kikao cha tatu cha mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano unaoendelea mjini Dodoma.
Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu ) Stephen Wasira  akiwasilisha Bungeni   (leo) mjini Dodoma taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2011 na mwelekeo wa mpango wa maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2012/13.
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim  Lipumba  akisikiliza kwa makini taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2011 na mwelekeo wa mpango wa maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2012/13 iliwasilishwa jana (leo)  Bungeni  mjini Dodoma na Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais   (Mahusiano na Uratibu) Stephen Wasira.

HOTUBA YA BAJETI MWAKA 2012/2013 ILIYOSOMWA NA WAZIRI WA FEDHA DK. WILLIAM MGIMWA BUNGENI LEO

1.         Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu liweze kujadili na kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2012/2013.  Pamoja na hotuba hii, nimewasilisha vitabu vinne vya Bajeti vinavyoelezea takwimu mbalimbali za Bajeti. Kitabu cha Kwanza kinaelezea makisio ya mapato.   Kitabu cha Pili kinaelezea makisio ya matumizi ya kawaida kwa Wizara, Idara zinazojitegemea; Taasisi na Wakala wa Serikali; cha Tatu kinahusu makisio ya matumizi ya kawaida kwa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na cha Nne kinaelezea makadirio ya matumizi ya maendeleo kwa Wizara, Idara zinazojitegemea, Taasisi na Wakala za Serikali; Mikoa na
Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha, upo Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2012 ambao ni sehemu ya Bajeti hii.

2.  Mheshimiwa Spika, awali ya yote, naomba nitumie fursa hii kumshukuru kwa dhati Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa imani kubwa aliyonayo kwangu kwa kuniteua kuwa Waziri wa Fedha. Naahidi kutekeleza majukumu niliyokabidhiwa kwa umakini na uaminifu mkubwa.
3.         Mheshimiwa Spika, napenda kuwapongeza wafuatao kwa kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa mawaziri kama ifuatavyo: Mhe. Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo (Mb); Mhe. Mhandisi Christopher Kajoro Chiza (Mb); Mhe. Dkt. Harrison George Mwakyembe (Mb); Mhe. Dkt. Fenella Ephraim Mukangara (Mb); Mhe. Balozi Khamis Sued Kagasheki (Mb); Mhe. Dkt. Abdallah Omari Kigoda (Mb). Aidha, napenda kuwapongeza wafuatao kwa kuteuliwa kuwa naibu mawaziri katika Wizara mbalimbali, Mhe. Janet Zebedayo Mbene (Mb); Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb); Mhe. Dkt. Seif Suleiman Rashid (Mb.); Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb.); Mhe.  January Yusuf Makamba (Mb.); Mhe. Dkt. Charles John Tizeba (Mb.); Mhe. Amos Gabriel Makalla (Mb.); Mhe. Angela Jasmine Kairuki (Mb.); Mhe. Stephen Julius Maselle (Mb.); na Mhe. Mhandisi Dkt. Binilith Satano Mahenge (Mb). Kadhalika, nampongeza Mhe. James Mbatia (Mb) kwa kuteuliwa na Mhe. Rais kuwa Mbunge.



4.         Mheshimiwa Spika, nawapongeza pia, Mhe. Alhaji Adam Kimbisa (Mb.); Mhe. Shy Rose Banji (Mb.); Mhe. Abdulah Alli Hassan Mwinyi (Mb); Mhe. Charles Makongoro Nyerere (Mb); Mhe. Dkt Twaha Issa Taslima (Mb); Mhe. Nderkindo Perpetua Kessy (Mb); Mhe. Bernard Musomi Murunyana (Mb); Mhe. Anjela Charles Kizigha (Mb.); Mhe. Maryam Ussi Yahaya (Mb.), ambao wamechaguliwa kutuwakilisha kwenye Bunge la Afrika Mashariki. Ni matumaini yangu watatuwakilisha vyema kwa maslahi na manufaa ya Taifa letu.

Sunday, June 10, 2012

shaibu ndeja a.k.a mzee wa ndege ndani ya info radio mtwara

AFARAA SULEIMAN AKIWA NA BANDALI A.K.A SWIRATY INFO RADIO MTWARA

NDANDA YAWEKA MATUMAINI KUCHEZA LIGI DARAJA LA KWANZA

TIMU ya Soka ya Ndanda leo imeweza kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi y mkamba Rangers ya Morogoro katika Mechi za ligi ya Taifa ngazi ya Taifa kituo cha Mtwara

 

Timu hizo zilikwenda mapumziko huku zikiwa hazijafungana huku Timu ya Ndanda ikiwa imekosa nafasi nyingi za wazi kuweza kufunga bao katika kipindi hicho cha kwanza

Kipindi cha pili kilianza kwa Timu ya Ndanda kuliandama Lango la Timu ya Mkamba Rangers na kufanikiwa kufunga bao la kwanza kunako dk ya 52 kwa kichwa na Gallas baada ya kuunganisha kona \safi iliyopigwa toka upande wa kushoto 

 

Wakiwa wanatafakari kuingia klwa goli hilo Mkamba Rangers walijikuta wanafungwa goli la pili kunako dk 60 na kupelekea mpira huo kumalizika kwa Timu ya Ndanda kuibuka na ushindi wa goli 2-0

 

Kwa Matokeo hayo ya leo Timu ya Ndanda imefikisha Point 10 nyuma ya vinara Kurugenzi ya Iringa yenye point 13 na mechi ya mwisho kwa Ndanda inakuwa hapo taeh 13 kwa kucheza na jirani zao Lindi mechi ambayo inatarajiwa kuwa ngumu na huku ikisubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka mkoani hapa

STARS KIMEELEWEKA LEO TAIFA

Kikosi kilichofanya mauaji leo
 Erasto Nyoni mfungaji wa bao la ushindi
Shomary Kapombe aliyesawazisha
 Boban akisaidia ulinzi
 Boban kabla ya kuingia kulia akiwa na Nurdin Bakari benchi
 Boban kulia, Nurdin katikati na Shaabn Nditi

 Dk Mwankemwa akimtibu jeraha Ngassa
Kaseja akiokoa moja ya hatari langoni Stars
Mwinyi Kazimoto akiwaongoza wenzake kutoka uwanjani baada ya mechi
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Gambia jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, katika mechi ya pili ya Kundi C, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Stars ilitoka nyuma kwa 1-0 kipindi cha kwanza na kuibuka na ushindi huo- kwa mabao ya kipindi cha pili ya Shomari Kapombe dakika ya 60 na Erasto Nyoni dakika ya 87 kwa penalti, baada ya beki mmoja wa Gambia kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Stars ambayo mechi ya kwanza ilifungwa 2-0 na wenyeji Ivory Coast mjini Abidjan Jumamosi iliyopita, kipindi cha kwanza ilicheza ovyo kidogo, lakini kuingia kwa Haruna Moshi ‘Boban’ aliyechukua nafasi John Bocco ‘Adebayor’ kipindi cha pili, kuliifanya Tanzania icheze kwa uhai na kulitia misukosuko lango la Gambia hatimaye kupata mabao hayo mawili.
Gambia walitangulia kupata bao lililofungwa na Mamadou Ceesay dakika ya nne.
Stars sasa imejinasua mkiani mwa kundi C na kupanda nafasi ya pili badaaye Morocco kutoa sare ya 2-2 jana na Ivory Coast inayoongoza kwa pointi zake nne.
Kwa Stars huu ni ushindi wa kwanza nyumbani tangu waifunge Jamhuri ya Afrika ya Kati Machi 26, mwaka jana
Vikosi vya Tanzania kushoto na Gambia kulia
Mfungaji wa bao la Gambia dakika ya nane, Mamadou Cesay akishangilia

Serikali Ya Mapinduzi Zanzibar Kutumia Billioni 648 Bajeti Ya 2012-13

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Zanzibar anayeshughulikia Fedha Uchumi Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee (pichani) akiwasilisha mwelekeo wa Bajeti ya Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013 ambapo makadirio ya mapato na matumizi ni Sh.bilioni 648.9.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Zanzibar anayeshughulikia Fedha, Uchumi , Mipango na Maendeleo, Omar Yussuf Mzee (kulia) akitoa taarifa ya mwelekeo wa Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mwaka 2012/2013 kwa wandishi wa habari kwenye ukumbi wa ofisi yake Vuga mjini Zanzibar jana

IPI MUHIMU: 'VUA GWANDA VAA GAMBA' YA CHADEMA NA 'CHANA GAMBA NA GWANDA VAA UZALENDO' YA CCM

Mfuasi wa Chadema akiwa na fulanaz yenye ujumbe 'VUA GWANDA VAA GWANDA' na wa CCM akiwa na fulanaz yenye umumbe 'CHANA GWANDA NA GAMBA, VAA UZALENDO', Je nani zaidi?

HIVI NDIVO CCM ILIVOSHABULIA VIWANJA VYA JANGWANI

 Waziri wa Ujenzi Mh.John Pombe Magufuli akihutubia katika mkutano wa wachama wa CCM Jangwani leo jijini Dar es salaam ikiwa ni moja ya mikakati ya chama kusikiliza kero za wananchi pamoja na mfumuko wa bei na upandaji holela wa nauli na kuelezea miradi mbalimbali inayoendelea nchini

Waziri wa uchukuzi Mh.Harrison Mwakyembe akihutubia katika mkutano wa wachama wa CCM jangwa leo jijini Dar es salaam ikiwa ni mikakati ya chama  kusikiliza kero za wananchi pamoja na mfumuko ya bei na upandaji holela wa nauli na kuelezea wananchi miradi mbalimbali inayoendelea
 Katika picha kutoka kushoto ni mawaziri Prof Anna Tibaijuka, John Magufuli na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam John Guninita.
 Abdulrahman Kinana (kulia) akipeana  mkono na waziri John Magufuli kushoto.

 Wanachama wa CCM wakichambua baadhi ya kadi ya vyama pinzani zilizorudishwa na wanachama wao kama zinavyoonekana katika picha
 Waziri wa nyumba na maendeleo na makazi Profesa Anna Tibaijuka akifafanua jambo katika mkutano huo
Viongozi wa CCM pamoja na mawaziri wakiimba katika mkutano huo uliofanyika Jangwani jijini Dar es salaam leo

Tuesday, June 5, 2012

UPDATES: Tukio kamili la ajali iliyo tokea eneo la Ntangano Ijombe Mbeya , kuanzia Ajali ilivyo tokea, uokoaji hadi Maiti na Majeruhi kufikishwa Hospitalini.


 Watu Mbali mbali wakisaidia shughuri za uokoaji katika eneo hilo 
 Umati Mkubwa wa watu uliofika Eneo la Ajali kushuhudia pamoja na kusaidia kazi ya uokoaji 
Baadhi ya watu wakiwa wameitanda Coaster hiyo kwa ajili ya kusaidia uokoaji 

 Baadhi ya ya maiti kama zinavyo onekana zikiwa chini wakati wanangojea shughuri nzima ya uokoaji 




 Gari Kubwa la Mizigo ambalo nalo Lilipinduka Mara baada ya ajali kutokea 
 Watu walio Fika katika hospitali ya Rufaa kutazama miili ya Marehemu
 Miili ya Marehemu ikiwa tayari imewasili katika Hospitali ya Rufaa Mbeya
 Polisi na watu mbali mbali pamoja na wauguzi wakiwa wamefika kusaidia kazi ya kushusha maiti hizo 
 Wafanyakazi wakiwa wanakimbiza majeruhi kupata huduma ya kwanza pamoja na Kupeleka Marehemu katika chumba cha Kuhifadhia Maiti.