Mziki
unakuwa kila kukicha na wasanii wanaongezeka sio tu kwa dar es salaam ila kwa
kila mkoa, wilaya na hata kata na vijiji
Wadadisi wa Mambo ya Burudani walishawahi kusema kuwa kila
ukipita nyumba 3 lazima ukutane na familia moja yenye msanii
Kuongezeka kwa wasanii hawa inatokana na maslahi
yaliyokuwepo kwa sasa kwa wasanii wenyewe ambapo kwa sasa kama unatoa nyimbo
inayokubalika kwa jamii tegemea kipato chako sio chini ya milioni 2 kwa kila
ukipata jukwaani
Mkoa wa Mtwara ni moja kati aya mikoa ambayo inahazina
kubwa ya wasanii hususani wale kwa kizazi kipya (bongo fleva)
Miongoni mwao wanautangaza mkoa huu wa Mtwara katika ngazi
za kitaifa mfano Pasha, Kigwema Das Lameck na wengineo
Uwepo wa wasanii hao na wengine wanaochipukia wakiwemo
Gitaa, Young Stable, Kibega,Pg,Young Chibo na wengineo unaufanya mkoa huo wa
Mtwara kuwa na hazina kubwa ya wasanii endapo watatambua kazi zao ni nini hasa
kwa jamii
Licha ya uwepo wa Production Nzuri ikiwemo 29 Reccods,
Pisha Reccod na mama land pia bado wasanii hao wamekuwa wanashindwa
kuzitumia vizuri kupata mafaniko makubwa kutokana na kazi zao
Mafaniko ninayoyazungumzia hapa sio ya kutoa nyimbo tu bali
pia kupata mialiko mbalimbali kutokana na ubora wa kazi zao na hii inategemea
na wasanii wenyewe walivyojirahisisha kwa mashabiki wao
Tatizo kubwa ninaloliona hapa ni wasanii wa Mtwara kwa sasa
kuwa na shida ya kusikika tu Radio nyimbo zao zikipigwa na sio harakati za
kufanya hata shoo kadhaa kutokana na kazi zao
Nimefanya utafiti wa kutosha juu ya hili ambapo nimegundua
hilo kwa wasanii waliokuwa wengi waliopo mtwara kwa sasa hawana mipango mingine
baada ya nyimbo zao kupigwa radio kitu ambacho kinapelekea hata mashabiki wao
nao kutokuwa na jipya kutoka kwa wasanii wao pale wanapo waona zaidi ya kusema
'nakukubali sana mwanangu kaza buti utatoka tu'
Utoaji wa nyimbo kwa kila baada ya mwezi au hata wengine
baada ya wiki mbili nalo limekuwa tatizo la wasanii hawa maana wanashindwa
kujua kama nyimbo iliyotolewa mwanzo kama imefanya vizuri ama la na hii inatokana
na pia studio ama produza nao kujirahisisha kwa wasanii wao kitu kinachopelekea
msanii kila siku atoe nyimbo
Mfano kama produza anatengeneza nyimbo kwa shilingi 150000
atakaetoa pesa hizo kati ya kumi ni mmoja kwa mujibu wa Sully Produza kutoka 29
Rekodi kitu ambacho hata utengenezaji wa kazi zao nao hautakuwa na ubora mkubwa
kutokana na kutolipa kiasi kinachotakiwa
|
pasha |
Nilibahatika kuongea na Sully na kumpa changamoto hii ya
kuwalemaza wasanii wa Mtwara kwa kutowalipisha gharama zinazostahili katika
utengenezaji na kazi zao kitu kinachopelekea wasanii hao kuwa hatarini kupotea
endapo tu mfumo wa ulipaji wa pesa inayostahili utakapoanzishwa moja kwa moja
na maproduza hao maana walishazoea sana kuslaidi kama msemo wa ndugu yangu pg
anavyosema
Sully alinihakikishia kwa sasa ameanza utaratibu huo wa
kuwataka wasanii sasa walipe pesa zote za kurekodi nyimbo vinginevyo atakuwa
tayari kufanya kazi na wasanii waliokuwa lebo kwake ama wenye uwezo wa kupia
kiasi anachokitaka
|
sully |
Tunataka kuona sasa mabadiliko katika sanaa ya kizazi kipya
Mtwara kwa kuona harakati nyingine zaidi baada ya nyimbo kutolewa na kusikika
radio, mfano shoo nyingi na sio tu kutegemea upigiwe simu kuambia kuna shoo na
utalipwa shilingi ngapi , bali hata kutengeneza ukaribu na watu wenye kumbi na
vyombo vya mziki katika kuandaa shoo za pamoja ili kuendelea kuwafanya
mashabiki wako kuona unaharakati za kuwafanya wawe karibu yako zaidi kutokana
na kazi zako na harakati zako
Sio kusubiri kuambiwa kuna shoo kitu ambacho unaweza kukaa
hata mwaka mzima haujafanya shoo yeyote ile kwa mazingira ya Mtwara
Zipo kumbi nyingi za bududani kwa sasa Mtwara ikiwemo masiha
Club na makonde royal night club kumbi ambazo hujaza mashabiki nykati za
wikiendi na hata wanapokuja wasanii kutoka dar es salaam wamekuwa wanajaza
mashabiki wengi kitu ambacho hata wasanii wa kusini wanaweza kufanya endapo tu
wanatakuwa karibu na wamiliki wa kumbi hizo kwa kuandaa hata shoo ya wasanii wa
kusini kila jumamosi ya mwisho wa mwezi na kadhalika
Uwezo wa kuwafanya mashabiki waokulipa kiingilio cha elfu
tano kwenda kuwaona wasanii wa kusini upo endapo watajitambua tu
Hii ni changamoto kwenu wasanii wa kusini sasa kuamka na
kuchangamkia fursa zilizopo kwa sasa mkoani mtwara
NB; Huu ni mtaamo wa
mmiliki wa blog hii na isichukuliwe kama wasanii hawa wamedharauliwa na
hawawezi mziki ila tunataka kuona matokeo chanya ya kazi zao kwa jamii