Wednesday, November 13, 2013

Kongamano la wadau wa Mfuko wa Bima wa Afya Mkoa wa Mtwara lafanyika leo katika ukumbi wa Makonde beach

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia kwenye Ukumbia Makonde Beach Tayari kufungua Kongamano la wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya
Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Mtwara Bi Joyce Mwenda akitambulisha wadau walioalikwa kwenye Kongamano hilo
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Joseph Simbakalia akihutubia wadau waliofika katika Kongamano hilo
Wakuu wa wilaya za Mkoa wa Mtwara wakiwa katika kongamano hilo la wadau wa mfuko wa bima ya afya
Wadau wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea kwenye kongamano hilo ndani ya ukumbi wa makonde beach mkoani Mtwara




Mkapa Atimiza Miaka 75


 mkapa+px


Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akipongezwa na Mhadhama Polycarp Kardinali Pengo jana wakati misa ya jubilei ya miaka 75 ya kuzaliwa kwake. Picha na Fidelis Felix.  

Dar es Salaam.Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa jana aliadhimisha miaka 75 ya kuzaliwa kwake kwa kufanya Ibada ya Misa iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo.

Katika ibada hiyo ya shukrani iliyofanyika Kanisa Katoliki la Maria Imakulata, Upanga jijini Dar es Salaam, Mkapa aliwataka Watanzania kumshukuru Mungu kwa kila jambo.

“Tunamshukuru Mungu kwa majaliwa aliyoipatia nchi yetu ya Tanzania na tunamwomba azidi kuijalia umoja katika yote tunayofanya na tunayokusudia kuyafanya,” alisema Mkapa.

Mkapa pia aliwashukuru waumini wenzake katika kanisa hilo, huku akifichua siri kwamba, Kadinali Pengo alimtaka ahamie Kanisa la Mtakatifu Joseph wakati alipokuwa rais, lakini hakukubali.
Kwa upande wake, Kardinali Pengo aliwataka Watanzania kuwa na tabia ya kumshukuru Mungu kwa kila jambo.

“Alichofanya Rais Mstaafu Mkapa ni cha kuigwa. Tunatakiwa kutambua kuwa hatuishi kwa nguvu zetu bali kwa uwezo wa Mungu hivyo ni lazima tumshukuru kama alivyofanya mwenzetu,” alisema Kardinali Pengo.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria ibada hiyo ni pamoja na Mawaziri Wakuu Wastaafu, Edward Lowassa na Cleopa Msuya, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Wengine ni waziri wa zamani, Profesa Philemon Sarungi, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa pamoja wakuu wa zamani wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Majenerali, Robert Mboma na George Waitara

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari kutoka kwa Kamanda Polisi Mkoa wa Mbeya

MAJAMBAZI 8
“PRESS RELEASE” TAREHE 13.11. 2013.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA SARE ZA JESHI.
MNAMO TAREHE 12.11.2013  MAJIRA YA  SAA 17:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KAMFICHENI, KIJIJI NA KATA YA   MKWAJUNI, TARAFA YA  KWIMBA, WILAYA YA  CHUNYA MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA  TRAIPHONE S/O MWANG’ONDA, MIAKA 24 ,KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA VWAWA WILAYA YA  MBOZI AKIWA NA SARE ZA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA [JWTZ] AMBAZO NI SURUALI MOJA, KOFIA MBILI NA FILIMBI MOJA. MBINU NI KUTUMIA SARE HIZO KATIKA MATUKIO YA  KIHALIFU. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA   JAMII KUACHA TABIA YA  KUMILIKI/KUTUMIA SARE ZA MAJESHI YA  ULINZI NA USALAMA  BILA  UTARATIBU KWANI NI KINYUME CHA SHERIA ZA NCHI NA ATAKAYEBAINIKA HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAKE ZITACHUKULIWA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MTU/WATU/KIKUNDI KINACHOMILIKI SARE ZA MAJESHI YA  ULINZI NA USALAMA IKIWA NI PAMOJA NA SILAHA KWA NIA YA  KUFANYA UHALIFU AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO TAREHE 12.11.2013  MAJIRA YA  SAA 14:30HRS HUKO KATIKA ENEO LA STENDI KUU, KATA YA   MBALIZI ROAD,TARAFA YA  SISIMBA, JIJI NA  MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA  ANYELWISYE S/O JOHN, MIAKA 22, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA MTAA WA MAJENGO  AKIWA NA BHANGI KETE MOJA SAWA NA UZITO WA GRAM 5. MBINU NI KUFICHA BHANGI KWENYE MFUKO WA SURUALI. MTUHUMIWA NI MVUTAJI WA BHANGI.  TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA   JAMII KUACHA TABIA YA  KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI- ACP]
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Wednesday, October 30, 2013

Kigwangalla kusaka saini za kutokuwa na imani na Spika wa Bunge Anna Makinda

Mbunge wa Nzega, Dk Khamis Kigwangalla, (CCM), leo anatarajiwa kuanza kukusanya saini za wabunge akitafuta kuungwa mkono katika hoja ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge, Anne Makinda kwa madai kwamba amekuwa akikiuka kanuni za Bunge.
Dk Kigwangalla aliibua hoja ya kutokuwa na imani na Spika katika kikao cha wabunge wote cha kuelezea shughuli zitakazofanywa na Bunge katika mkutano wa 13, kilichofanyika juzi jioni kwenye ukumbi wa Pius Msekwa.
Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, jana alithibitisha kuwapo kwa mjadala huo katika kikao cha wabunge, lakini hakuwa tayari kueleza kwa undani na badala yake alisema kwamba leo ataanza kukusanya saini za wabunge kwa ajili ya kukamilisha hoja ya kutokuwa na imani na Spika Makinda.
Chanzo chetu kutoka katika kikao hicho cha wabunge kilibainisha kuwa Kigwangalla alihoji kuhusiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge (CCM-Bariadi Magharibi) kuteuliwa na Spika wakati katika kamati nyingine wenyeviti na makamu huchaguliwa na wajumbe wa kamati husika.(P.T)
Pia Dk Kigwangala alisema Spika Makinda alivunja kanuni kwa kuwapa posho ya Sh430,000 kwa siku wajumbe wa kamati inayoongozwa na Chenge wakati wajumbe wa kamati nyingine wamekuwa wakipewa Sh130,000.
"Anachokifanya Spika ni matumizi mabaya ya fedha za umma, inakuwaje wengine wafanye kazi hata bila posho lakini wao (Kamati ya Bajeti), walipwe posho ya Sh430,000 kwa siku?" chanzo hicho kilimkariri Dk Kigwangalla akihoji.
Hata hivyo, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah akizungumza na gazeti hili jana alisema mazingira ya kamati fulani kupata malipo ya ziada tofauti na viwango vya kawaida hutokea pale uongozi wa kamati husika unapoomba kwa Spika.
"Si kweli kwamba Kamati ya Bajeti inalipwa fedha za ziada kila wakati, hapana, ni pale tu wanapoomba malipo hayo kutokana na sababu ambazo lazima Spika aridhike nazo.
Ieleweke kuwa siyo kamati hiyo tu, kwa sasa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ambayo inachambua miswada mingi nayo imekuwa ikiomba na baada ya Spika kuridhia basi nao wanapewa," alisema Dk Kashililah.
Katibu huyo wa Bunge alieleza kuwa zaidi ya kamati nane zimewahi kuomba malipo ya ziada kwa maana ya kutaka posho zaidi, ulinzi, usafiri na hata chakula, ikiwa zinakabiliwa na majukumu ya ziada pia katika mazingira tofauti nje ya utaratibu wa kawaida.
"Kimsingi, kamati nyingi zinapewa malipo tofauti, watu wanaweza kuwa na kazi mpaka saa saba au nane usiku, au wanakwenda kufanya kazi katika mazingira yasiyokuwa ya kawaida, taratibu zinamruhusu Spika kama akiridhika na maelezo ya kazi husika, basi anaruhusu kutekelezwa kwa maombi hayo," alisema Dk Kashililah.
Kuhusu Serukamba
Aidha, Dk Kigwangalla alinukuliwa akisema Spika amekiuka kanuni kwa kumchagua Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, Peter Serukamba (Kigoma Mjini-CCM), kuwa mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti.
"Hakuna mbunge yeyote aliyepo katika kamati mbili lakini hata kungekuwa na sababu maalumu basi wa kuteuliwa angekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, Mahmoud Mgimwa (Mufindi Kaskazini-CCM) ambaye TRA (Mamlaka ya Mapato Nchini) ipo chini ya kamati yake," kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kilisema Dk Kigwangalla alisema badala ya kumweka karibu katika ushiriki, Mgimwa alipokwenda katika kamati hiyo aliambulia kufukuzwa.
Akizungumzia suala hilo, Dk Kashililah alisema Serukamba pamoja na wabunge wengine kadhaa waliteuliwa na Spika kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kamati hiyo wakati wa kipindi cha Bajeti Kuu ya Serikali.
Aliwataja wabunge wengine walioteuliwa kushiriki katika Kamati ya Bunge ya Bajeti kuwa ni John Cheyo (Bariadi Mashariki-UDP), Salahe Pamba (Pangani - CCM) na Hamadi Rashid Mohamed (Wawi - CUF).
Kanuni za Bunge
Kwa mujibu wa kanuni za Bunge katika toleo la mwaka 2007, kifungu cha 137(1), ili kumwondoa Spika madarakani, mbunge anayetaka kuwasilisha hoja hiyo atatakiwa kuwasilisha taarifa ya maandishi ya kusudio hilo kwa Katibu, akieleza sababu kamili ya kutaka kuleta hoja hiyo.
Kifungu kidogo cha pili kinasema baada ya kupokea taarifa ya maandishi ya kusudio la kumwondoa Spika kwenye madaraka, Katibu atapeleka taarifa hiyo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa ajili ya kujadiliwa.
Kifungu cha tatu kinabainisha kuwa endapo kamati hiyo itaridhika kuwa zipo tuhuma mahususi dhidi ya Spika zinazohusu uvunjaji wa masharti ya ibara husika za Katiba, sheria au kanuni zinazoongoza shughuli za Bunge, basi kamati hiyo itaidhinisha hoja hiyo ipelekwe bungeni ili iamuliwe.
Kanuni zinasema Naibu Spika, atakalia Kiti cha Spika wakati wa kujadili hoja ya kutaka kumwondoa Spika madarakani na Spika atakuwa na haki ya kujitetea wakati wa mjadala na kwamba ili kumwondoa zinahitajika kura zisizopungua theluthi mbili ya idadi ya wabunge wote.


Tanzania; Tunaweza kujitoa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Serikali ya Tanzania imesema inatafakari ushiriki wake ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na inaweza kujitoa ndani ya Jumuiya hiyo iwapo itaendelea kutengwa katika baadhi ya vikao.
Aidha imesema Tanzania haitambui vikao vinavyofanywa na nchi tatu zilizopo ndani ya Jumuiya hiyo ambazo zimekuwa zikizitenga Tanzania na Burundi.
Waziri anayehusika na masuala ya Afrika Mashariki wa Tanzania Samwel Sitta ameliambia Bunge la Tanzania kuwa makubaliano ya vikao hivyo vinavyofanywa na nchi za Kenya, Rwanda na Uganda yatatekelezwa na nchi hizo zinazofanya vikao hivyo kwa sababu vinafanyika nje ya utaratibu wa mkataba wa jumuiya hiyo
Katika mikutano iliyofanyika hivi karibuni Tanzania na Burundi hazikualikwa kwenye vikao hivyo.
Kwa mujibu wa Waziri Sitta mikutano ya wakuu wa nchi za Rwanda, Kenya na Uganda ambayo ilianza kwa kuitenga Tanzania ilifanyika Entebbe nchini Uganda mwezi Juni mwaka huu na kufuatiwa na mkutano wa pili uliofanyika Agosti mwaka huu huko Mombasa nchini Kenya ambapo nchi hizo tatu bila kuishirikisha Tanzania walizungumzia uanzishaji wa himaya moja ya forodha.
Mambo mengine waliyozungumza wakuu hao ilikuwa uanzishaji wa visa moja ya utalii kwa nchi zao na matumizi ya vitambulisho vya uraia ambavyo vitatumika kama hati za kusafiria miongoni mwa nchi hizo.
Aidha Waziri Sitta amesema ndani ya mikutano hiyo pia walizungumzia kuanzisha mchakato wa kuanzisha shirikisho la nchi hizo.
Tayari Tanzania imeanza mazungumzo na nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuangalia ni kwa namna gani zitaanzisha ushirikiano nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kama zinavyofanya nchi za Rwanda, Uganda na Kenya


Wednesday, October 16, 2013

Wanachama wa Yanga kupiga kura kuamua Yanga kampuni au Vinginevyo

Wanachama wa Yanga wamepewa muda wa mwezi mzima kupiga kura ya kuamua klabu yao kuendeshwa kwa mfumo wa kampuni au la.


Utaratibu huo unaanza leo hadi Novemba 10, mwaka huu na Katibu Mkuu, Lawrence Mwalusako ameeleza boksi maalum la kupigia kura limewekwa makao makuu ya klau hiyo.


“Kila mwanachama afike akiwa na kadi yake ya uanachama kwa ajili ya kazi hiyo ya kupiga kura. Hii itasaidia watu kutopiga kura mara mbili,” alisema.

Katika mkutano wa Januari, mwaka huu wanachama walipewa pendekezo la kuchagua kuhusiana na kampuni au mfumo wa sasa na mwenyekiti wa kamati ya utendaji akawaeleza kwamba atawapa nafasi ambayo sasa imetolewa.

Sikukuu Njema

Uongozi wa Swiraty.blogsport.com unawatakia wasomaji wake wote siku kuu njema ya Idd Alhaji musherekee kwa amani na utulivu

                                           
                                 .................IDD MUBARAK..........

Tuesday, October 8, 2013

P Square kuwania tuzo zaidi ya Moja

Kundi la muziki ambalo ndilo gumzo kwa sasa Africa, P Square ambao mwezi ujao wanatarajia kudondosha onyesho la aina yake hapa Bongo, kutokana na ubora wa kazi zao wametajwa kuwania tuzo kubwa zaidi ya mbili ambazo zitatolewa kabla ya kuisha kwa mwaka huu.

Orodha hii inaweka wazi kuwa wasanii hawa wanawania tuzo ya Best African Act kutoka kituo maarufu cha Televisheni kinachorusha matangazo ya muziki, na sherehe kubwa za ugawaji wa tuzo hizi utafanyika tarehe 10 mwezi Novemba mwaka huu.

Kwa upande mwingine pia P Square wanawania tuzo maarufu za Soul Train za BET, na hii ni kutokana na hit yao inayotikisa dunia ya Personally ambayo imewaingiza katika kipengele cha Best International Performance, na tuzo hizi zitatolewa tarehe 1 mwezi Desemba.

Wakati huu huu Afrika Mashariki inajipanga kwa ujio mzito wa P Square ndani ya Jiji la Dar es Salaam , kumbuka siku hiyo muhimu itakuwa ni tarehe 23 Novemba,

Profesa Jay; Mimi ni Composer

Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya hapa Tanzania, Professor Jay ameongea na Swiraty Blog kuhusiana na studio yake mpya ya Mwanalizombe ambayo itaanza kufanya kazi hivi karibuni pamoja na kufafanua swala zima la Producer wa Studio hii na namna studio itakavyokuwa ikifanya kazi.

Jay amesema kuwa kutakuwa na mchango wake mkubwa katika kusuka kazi za studio kutokana na kuwa yeye ni 'composer' wa midundo japo pia kutakuwa na producer ambaye hakuwa tayari kumuweka wazi, na ameahidi kuanda kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na production na producers wakali wa muziki hapa Bongo.

Kwa upande mwingine pia, Professor Jay amegusia swala la yeye na kolabo za kimataifa ambapo amesema kuwa baada ya kupata studio hii sasa, kutokana na ukweli kuwa ni watu wengi wanaopenda kazi zake na ni wasanii wengi kutoka Afrika Mashariki wanapenda kufanya kazi naye, Mipango itafanyika nao na kuanza kuzipika kazi hizi katika siku za karibuni

11 wakamatwa wakijifunza mafunzo ya ujeshi Mtwara

IMG_0250


POLISI mkoani Mtwara inawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kupata mafunzo ya kijeshi mstuni kwa kutumia CDs za Al shabab.

Tukio hilo la aina yake limetokea katika mlima Makolionga wilaya ya Nanyumbu mkoani hapa ambapo pia CDs zenye mafunzo mbalimbali ya kijeshi 25 zimekamatwa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Zellothe Stephen ameuambia mtandao wa KUSINI leo kuwa watuhumiwa hao walikamatwa wiki moja iliyopita baada ya jeshi lake kupata taarifa kutoka kwa wasamalia wema.

“CD hizo zilikuwa zinatoa mafunzo ya Al Shabab ya kuchinja watu, Mauaji wa Osama Bin Laden, Zindukeni Zanzibar, Kuandaa Majeshi, Mauaji wa Idd Amin na Mogadishu Sniper” alisema Stephen
Alisema watuhumiwa wote ni wakazi wawilaya ya Nanyumbu mkoani hapa na kwamba walikuwa wakiongoza na Mohamed Makande 39, mkazi wa kijiji cha sengenya ambaye pia anashikiliwa na jeshi hilo.

Aliwataja wengine waliokamatwa kuwani Hassan Omary 39, mkazi wa kijiji cha Nanyulu, Rashid Ismail 27, Abdallah Y. Hamisi 32, Salum Wadi 38, Fadhili rajabu 20, Abbas muhidini 32, Ismail Chande 18, Said Mawazo and Issa Abeid 21, Ramadhani Issa 26 wote wakazi wa kijiji cha Likokona.

“Tumekamata mapanga mawili, Decki ya DVD, Sola, Visu, Tochi, Betri, simu za kiganjani tano, vyombo mbalimbali vya kulia chakula, baiskeli tatu, vitabu mbalimbali wa dini ya kiislam, unga wa mahindi kilo 50, mahidi kilo 150 na vilago vya kulalia” alitaja kamanda huyo vitu vingine walivyokamata.

“vingine ni mfuko wa kijani unaosadikiwa wa kijeshi wenye nembo ya nanga ya meli yenye mistari kulia na kushoto na nyoka katikati”
Alisema jeshi lake licha ya kuwafikisha watuhumiwa mahakamani linaendelea na uchunguzi wa kinakwa kusirikiana na polisi makao makuu kwa lengo la kufanikisha kuunasa mtandao mzima

Chanzo Kusini.wordpress.com

Kiwanda cha Uzalishaji Maji cha Ndanda Chafungiwa

IMG_0921
Maji Ndanda Spring
Kiwanda cha Maji cha Ndanda Springs kilichopo kijiji cha Mwena , eneo la Ndanda wilayani Masasi mkoani Mtwara kimefungiwa kuzalisha maji hayo kutokana na madai ya kushuka kwa ubora wake.
Ofisa Afya wa Mkoa wa Mtwara, Jamal Mbava alisema katika ukaguzi uliofanywa Agosti, 12 na 13 mwaka huu wilaya ya Newala mkoani hapa ulibaini uwepo wa takataka zinazoelea na kuonekana kwa macho katika katoni 93 Mussa Kazibure.
Kwa mujibu wa barua ya ofisa huyo kwenda kwa mkurugenzi wa kiwanda hicho ya tarehe 23/09/2013 yenye kumbukumbu Na: RHO/TFDA/5/63 maji hayo kukutwa na takataka ndani ni kukiuka kifungu cha sheria Na 30 (2) cha TFDA
Alisema katoni hizo zikiwa na batch namba tofauti yaani 040912/160812 na 030912 zilikamatwa na kuwekwa katika ofisi ya afya ya wilaya hiyo huku sampuli za maji hayo zikipelekwa kwa mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA) Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi.
“ Kwa mamlaka niliyonayo chini ya sheria za Tanzania No. 1 ya chakula, dawana vipodozi ya mwaka 2003 kifungu cha 106 (F), nikaandika na kutoa mari ya kufunga kiwanda hicho mkapa hapo tutakapopata majibu ya kimaabara kutoka TFDA DSM” alisema Mbava
Aliongeza kuwa “ Kwa taarifa hii ambayo naitoa kwenu naomba wananchi kuchukua taadhari wakati wa kutumia maji hayo ya kunywa , popote pale maji hayo yanapofika na pindi wakibaini hasa batch hizo na zinginezo ambao chupa zake zitaonekana kuwa na taka zinazoelea ambazo kitaalamu zinaitwa kwa ujumla kwa jina moja tu la ‘Impurities’ watoetaarifa katika ofisi za afya zilizo karibu yao”
Chanzo: Kusini.word press.com

Friday, October 4, 2013

Picha ya siku

PIX4b
Waziri wa habari Vijana utamaduni na Michezo Fenella Mukangala akipiga mpiara katika moja ya matumio yake

WANAKIJIJI 752,000 WAMEPATIWA MAJI KUTOKANA NA MATOKEO MAKUBWA SASA (MMS) KWA KIPINDI CHA MIEZI MITATU

IMG_0160


Wizara ya Maji ikishirikiana na OWM -TAMISEMI, Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Wilaya mbalimbali zimepata mafanikio makubwa katika utekelezaji wa mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa kwa kuwapatia maji wananchi waishio vijijini wapatao 752,000 wa ziada katika kipindi cha miezi mitatu tangu tarehe 1 Julai mwaka huu.
Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 2 ya wakazi wote wanaoishi vijijini kupata huduma ya maji safi kwa kipindi hicho cha miezi mitatu. Baadhi ya miradi iliyokamilika ni ya vijiji vya Mtandi, Rondo, na Kineng’ene vilivyopo Mkoani Lindi; Vijiji vya Engagile, Gedamar, Mtuka vilivyopo Mkoani Manyara; na Vijiji vya Iwalanje, na Maninga vilivyopo Mkoani Mbeya. Hivi ni baadhi tu ya vijiji ambavyo miradi imekamilika na wanavijiji wanapata huduma ya majisafi na salama karibu na makazi yao.
Akizungumzia mafanikio hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Christopher Sayi amesema “Nina imani kubwa tutadumisha usambazaji wa maji safi na salama kwa wananchi 15,200,000 ndani ya kipindi kilichopangwa cha miaka mitatu ya utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (MMS) kuanzia 2013/2014 hadi 2015/2016”
Mafanikio haya yamewezekana kutokana na MMS kugatua madaraka kwa watendaji, jambo ambalo limewafanya watendaji kuwajibika na kuharakisha utendaji wao wa kazi za kila siku. Katika kuhakikisha mafanikio ya MMS na kutimiza lengo, Wizara ya Maji imeongeza ufanisi katika masuala ya ununuzi wa huduma, ikiwemo ujenzi na vifaa vyake, kutoka siku 265 za hapo awali hadi siku 90 za sasa.
Aidha Afisa Mwandamizi katika Wizara hiyo, Mhandisi Goyagoya Mbenna, alisema “Mpango huu wa MMS umetuwezesha sisi Wahandisi kufanya kazi kwa umakini na umeleta mafanikio katika kuharakisha utendaji wetu wa kazi”
Kwa upande wake Bwana Omari Issa, Mtendaji Mkuu wa PDB alisema, “Nimefurahi sana kuona utaratibu huu wa MMS umepokelewa vizuri na watendaji na wananchi. Nawashauri wahusika wote waendelee kuufuatilia na kuutekeleza kwa makini kwa kuwa unaleta fursa ya kipekee ya kuleta maendeleo ya haraka nchini mwetu”.
Hapo awali ongezeko la idadi ya wananchi wanaopata huduma ya majisafi vijijini ilikuwa ni kati ya asilimia 0.5 hadi 1.0 kwa mwaka, sawa na ongezeko la watu kati ya 300,000 – 500,000 kwa kipindi hicho. Kwa kupitia mfumo huu wa sasa wa MMS, Wizara ya Maji itatekeleza jumla ya miradi 1,810 (sawa na vituo 26,720 vya kuchotea maji) na kuunda vyombo vya watumia maji 2,728 nchi nzima kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2013/2014 – 2015/2016. Miradi hii itazidisha usambazaji wa maji kwa wakazi 7,000,000 waishio vijijini ili jumla ya wananchi 22,300,000 ambayo ni sawa na zaidi ya asilimia 67 ya wakazi wote vijijini wawe wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao ifikapo Juni 2016.
Hadi kufikia mwezi Septemba 2013, jumla ya vituo vya kuchotea maji 3,008 vimekamilika na kutoa huduma ambapo jumla ya wakazi 15,952,000 vijijini wanapata huduma hiyo ya maji safi. Aidha, vyombo vya watumia maji 228 vimeundwa na kuanza kufanya kazi. Wizara ya Maji ikishirikiana na OWM- TAMISEMI, Halmashauri inaendelea na ujenzi, upanuzi na ukarabati wa miundombinu ya maji pamoja na shughuli za uendeshaji na matengenezo ya miradi ya maji katika vijiji mbalimbali nchini. Kwa kulingana na juhudi zinazoendelea Matokeo Makubwa yatapatikana kama ilivyokusudiwa.
Mara kwa mara Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe amekuwa akiwataka wafanyakazi wa sekta ya maji kuhakikisha wanaongeza jitihada katika kazi sambamba na kwenda na kasi ya MMS. Katika kikao chake cha hivi karibuni na wafanyakazi wa Wizara ya Maji alisema, “Sitaki yale maneno ya kawia ufike, mwendapole hajikwai” Sisi tunasema “Haraka haraka ndiyo mwendo”. Hivyo nataka tufanyekazi kwa bidii, na kwa ufanisi wa hali ya juu” Alisisitiza Waziri.
Wizara ya Maji kwa upande wake inashirikiana na OWM-TAMISEMI kusimamia na kufuatilia utekelezaji ili kujiridhisha kuwa miradi ya Maji inatalekelezwa kwa kiwango kilichowekwa.

Shilole afuata nyayo za Lady Gaga



Kutokana na kuwa gumzo kubwa kila anapopata nafasi ya kupanda jukwaani kufanya onyesho, msanii wa muziki Shilole ameongea na swiraty blog kuhusiana na malengo hasa pamoja na nguvu ambayo huwa inamsukuma kufanya vile anavyofanya katika perfomance zake.

Shilole amefichua kuwa, role model wake katika muziki kwa sasa ni nyota Lady Gaga ambaye kitu kikubwa alichojifunza kutoka kwake ni kujiachia pindi anapokuwa jukwaani, na kuwaridhisha wale ambao wametoa pesa zao ili kushuhudia burudani kutoka kwake.

Shilole pia amewataka mashabiki wake kukaa tayari na kolabo ambayo aliwaahidi kuwa atafanya na mwanamuziki Jennifer Lopez ambayo anatarajia kuikamilisha mwisho wa mwaka huu atakapokwenda tena ziarani Marekani.