Msanii mkongwe wa
muziki wa kizazi kipya hapa Tanzania, Professor Jay ameongea na Swiraty Blog kuhusiana na studio yake mpya ya Mwanalizombe ambayo
itaanza kufanya kazi hivi karibuni pamoja na kufafanua swala zima la Producer
wa Studio hii na namna studio itakavyokuwa ikifanya kazi.
Jay amesema kuwa kutakuwa na mchango wake mkubwa katika kusuka kazi za studio kutokana na kuwa yeye ni 'composer' wa midundo japo pia kutakuwa na producer ambaye hakuwa tayari kumuweka wazi, na ameahidi kuanda kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na production na producers wakali wa muziki hapa Bongo.
Kwa upande mwingine pia, Professor Jay amegusia swala la yeye na kolabo za kimataifa ambapo amesema kuwa baada ya kupata studio hii sasa, kutokana na ukweli kuwa ni watu wengi wanaopenda kazi zake na ni wasanii wengi kutoka Afrika Mashariki wanapenda kufanya kazi naye, Mipango itafanyika nao na kuanza kuzipika kazi hizi katika siku za karibuni