Msanii Dully Sykes ambaye mitaa inasubiri kazi mpya kutoka kwake ambayo inakwenda kwa jina Kabinti Special ambayo ataiachia rasmi mapema mwezi huu katika nafasi yake kama mkongwe wa sanaa ya muziki hapa Tanzania, ametoa maoni yake kuhusiana na wasanii wenzake wanaojiita Ma-rais.
Ujumbe huu mpya na mkali wa Prince Dully Sykes umeelekezwa haswa kwa wasanii Madee pamoja na Ney wa Mitego ambao kwa muda mrefu sasa wamekuwa na ubishi endelevu kati yao juu ya ni nani Rais wa Manzese ambapo ndipo wanapotokea.
Dully amesema kuwa anawashangaa sana wasanii hawa ambao amewataja kama wadogo zake kwa kugombania Urais hewa ambao hauna maslahi zaidi ya kulazimisha heshima wakati Tanzania kuna rais mmoja tu ambaye ni Rais Kikwete.
Kwa sasa tunaendelea kusuburi kwa hamu kusikia majibu ya Ma Rais hao wa muziki Madee pamoja na Ney wa Mitego ambao wanakalia kiti kimoja kuiendesha nchi ya kitongoji cha Manzese Jijini Dar es Salaam.