Maji Ndanda Spring |
Kiwanda cha Maji cha Ndanda
Springs kilichopo kijiji cha Mwena , eneo la Ndanda wilayani Masasi mkoani
Mtwara kimefungiwa kuzalisha maji hayo kutokana na madai ya kushuka kwa ubora
wake.
Ofisa Afya wa
Mkoa wa Mtwara, Jamal Mbava alisema katika ukaguzi uliofanywa Agosti, 12 na 13
mwaka huu wilaya ya Newala mkoani hapa ulibaini uwepo wa takataka zinazoelea na
kuonekana kwa macho katika katoni 93 Mussa Kazibure.
Kwa mujibu wa
barua ya ofisa huyo kwenda kwa mkurugenzi wa kiwanda hicho ya tarehe 23/09/2013
yenye kumbukumbu Na: RHO/TFDA/5/63 maji hayo kukutwa na takataka ndani ni
kukiuka kifungu cha sheria Na 30 (2) cha TFDA
Alisema katoni
hizo zikiwa na batch namba tofauti yaani 040912/160812 na 030912 zilikamatwa na
kuwekwa katika ofisi ya afya ya wilaya hiyo huku sampuli za maji hayo
zikipelekwa kwa mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA) Dar es Salaam kwa
uchunguzi zaidi.
“ Kwa mamlaka
niliyonayo chini ya sheria za Tanzania No. 1 ya chakula, dawana vipodozi ya
mwaka 2003 kifungu cha 106 (F), nikaandika na kutoa mari ya kufunga kiwanda
hicho mkapa hapo tutakapopata majibu ya kimaabara kutoka TFDA DSM” alisema
Mbava
Aliongeza kuwa “
Kwa taarifa hii ambayo naitoa kwenu naomba wananchi kuchukua taadhari wakati wa
kutumia maji hayo ya kunywa , popote pale maji hayo yanapofika na pindi
wakibaini hasa batch hizo na zinginezo ambao chupa zake zitaonekana kuwa na
taka zinazoelea ambazo kitaalamu zinaitwa kwa ujumla kwa jina moja tu la
‘Impurities’ watoetaarifa katika ofisi za afya zilizo karibu yao”
Chanzo: Kusini.word press.com
|