Wanachama wa Yanga wamepewa muda wa mwezi mzima kupiga kura ya kuamua
klabu yao kuendeshwa kwa mfumo wa kampuni au la.
Utaratibu huo unaanza leo hadi Novemba 10, mwaka huu na Katibu Mkuu,
Lawrence Mwalusako ameeleza boksi maalum la kupigia kura limewekwa makao makuu
ya klau hiyo.
“Kila mwanachama afike akiwa na kadi yake ya uanachama kwa ajili ya
kazi hiyo ya kupiga kura. Hii itasaidia watu kutopiga kura mara mbili,”
alisema.
Katika mkutano wa Januari, mwaka huu wanachama walipewa pendekezo la
kuchagua kuhusiana na kampuni au mfumo wa sasa na mwenyekiti wa kamati ya
utendaji akawaeleza kwamba atawapa nafasi ambayo sasa imetolewa.