Tuesday, October 8, 2013

11 wakamatwa wakijifunza mafunzo ya ujeshi Mtwara

IMG_0250


POLISI mkoani Mtwara inawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kupata mafunzo ya kijeshi mstuni kwa kutumia CDs za Al shabab.

Tukio hilo la aina yake limetokea katika mlima Makolionga wilaya ya Nanyumbu mkoani hapa ambapo pia CDs zenye mafunzo mbalimbali ya kijeshi 25 zimekamatwa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Zellothe Stephen ameuambia mtandao wa KUSINI leo kuwa watuhumiwa hao walikamatwa wiki moja iliyopita baada ya jeshi lake kupata taarifa kutoka kwa wasamalia wema.

“CD hizo zilikuwa zinatoa mafunzo ya Al Shabab ya kuchinja watu, Mauaji wa Osama Bin Laden, Zindukeni Zanzibar, Kuandaa Majeshi, Mauaji wa Idd Amin na Mogadishu Sniper” alisema Stephen
Alisema watuhumiwa wote ni wakazi wawilaya ya Nanyumbu mkoani hapa na kwamba walikuwa wakiongoza na Mohamed Makande 39, mkazi wa kijiji cha sengenya ambaye pia anashikiliwa na jeshi hilo.

Aliwataja wengine waliokamatwa kuwani Hassan Omary 39, mkazi wa kijiji cha Nanyulu, Rashid Ismail 27, Abdallah Y. Hamisi 32, Salum Wadi 38, Fadhili rajabu 20, Abbas muhidini 32, Ismail Chande 18, Said Mawazo and Issa Abeid 21, Ramadhani Issa 26 wote wakazi wa kijiji cha Likokona.

“Tumekamata mapanga mawili, Decki ya DVD, Sola, Visu, Tochi, Betri, simu za kiganjani tano, vyombo mbalimbali vya kulia chakula, baiskeli tatu, vitabu mbalimbali wa dini ya kiislam, unga wa mahindi kilo 50, mahidi kilo 150 na vilago vya kulalia” alitaja kamanda huyo vitu vingine walivyokamata.

“vingine ni mfuko wa kijani unaosadikiwa wa kijeshi wenye nembo ya nanga ya meli yenye mistari kulia na kushoto na nyoka katikati”
Alisema jeshi lake licha ya kuwafikisha watuhumiwa mahakamani linaendelea na uchunguzi wa kinakwa kusirikiana na polisi makao makuu kwa lengo la kufanikisha kuunasa mtandao mzima

Chanzo Kusini.wordpress.com