Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca Cola imewaonyesha wadau mfululizo wa vipindi vya televisheni vya Coke Studio vilivyorekodiwa vinavyowahusisha wasanii wanaofanya vizuri barani Afrika.
Mfululizo wa vipindi hivyo vya televisheni, umetambulishwa rasmi jana usiku Jijini ambapo baadhi ya washiriki, wasanii na wadau mbalimbali waliohudhuria kujionea kazi hiyo, katika uzinduzi huo uliopambwa na burudani ya muziki kutoka B Band.
Wadau waliohudhuria walipata nafasi ya kutazama sehemu ya kwanza ya kipindi kutoka Coke Studio, na eNewz ilikuwepo kufuatilia kwa karibu ambapo pia tulipata nafasi ya kuongea na wasanii washiriki walioiwakilisha Tanzania, Diamond pamoja na Lady Jay Dee ambao wamesema wamefurahi sana kupata nafasi hii kubwa ya kuendelea kuupanua muziki wao Afrika na duniani kwa ujumla.
Kwa upande wake, Meneja Bidhaa Coca Cola Tanzania Maurice Njowoka na amesema kuwa kampuni ya Coka Cola imejitoa kuwapatia nafasi watanzania hususan vijana nafasi ya kuendelea kunufaika na kufurahia burudani ya muziki pamoja na kuunganisha tamaduni za kiafrika.
Coke Studio Africa imeweza kuwaweka pamoja wasanii 24 wakubwa kabisa Afrika kutoka nchi 8 tofauti na kutengeneza nyimbo zipatazo 50 zilizowapagiwisha vilivyo wapenzi wa muziki.