Sunday, January 27, 2013

PINDA ,NCHIMBI KUWASILI MTWARA LEO

kutokana na hali ilivo hivi sasa nimlezimika kuweka hata habari za kijamaii ili kuwapa updates wadau wangu wa mtandao huuu.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda
Tariifa ilizotibitishwa asubuhi ya leo na kamnda wa polisi Mkoa wa Mtwara Mary Nzuki ni kwamba waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Mambo Ya Ndani Emanuel Nchimbi wanawasili leo Mkoani Mtwara kwa ajili ya kujionea hali halisi ilivo hivi sasa
Dk Emanuel Nchimbi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
"kwa sasa siwezi kukupa taarifa zilizo nzuri zidi juu ya matukio kwa kuwa niko barabarani kuelekea uwanja wa ndege kuwapokea viongozi wakubwa wa nchi ambao ni waziri mkuu na waiziri wa mambo ya ndani labda ukinipigia baadae nitakupa taarifa nzuri zaidi" alisema kamnda nzuki

YANGA NA PRISONS YA EMMANUEL GABRIEL TAIFA LEO, ITAKUWAJE?

YANGA

 Na Idrisa bandali



Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC leo wanashuka dimbani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na Tanzania Prisons ya Mbeya katika mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili wa ligi hiyo. 


Yanga inayoongoza ligi hiyo kwa pointi zake 29, baada ya kucheza mechi 13, ikiizidi mbili Azam iliyocheza mechi 14 na tatu Simba SC iliyocheza 14 pia, ikishinda leo itaongeza idadi ya pointi za kuwazidi wapinzani wake hao katika mbio za ubingwa kama ilivyokuwa baada ya mzunguko wa kwanza. 

Katika mchezo wa kwanza wa ligi hiyo baina ya timu hizo mjini Mbeya, Yanga ililalizimishwa sare ya bila kufungana na Maafande hao wa Jeshi la Magereza. 

 Mambo yatakuwaje leo Uwanja wa Taifa, ikikumbukwa Yanga iliweka kambi ya wiki Uturuki, kujiandaa na hatua hii ya salama? twendeni Taifa tukashuhudia jioni ya leo, Prisons ikiongozwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba na timu ya taifa, Emmanuel Gabriel Mwakyusa aliyekuwa mwiba kwa wana Jangwani hao, enzi zake akivaa jezi nyekundu ya Msimbazi.

Monday, January 21, 2013

NDANDA KUONDOKA JANUARY 25

Idrisa bandali afisa habari wa Ndanda

Timu ya Soka ya Ndanda Fc ya Mtwara inayocheza Ligi Daraja la Kwanza Taifa inatarajia kuondoka Mkoani Mtwara Ijumaa ya January 25 mwaka huu kuelekea Dar es salaam tayari kwa mechi zao mbili za ligi darja la kwanza

Akizungumza na SWIRATY BLOG katibu Mkuu wa Ndanda Fc Kachele amesema kuwa timu itaondoka mkoani mtwara ikiwa na wachezaji 12 huku wakitarajia kuungana na wachezji wengine mara baada ya kufika dar es salaam

Kachele amesema kulingana na taarifa zilizopo ni kwamba Ndanda watacheza mechi ya kwanza na timu ya Jeshi ya Transit Camp n baadae kuumana na green worious kabla ya kurejea Mtwara tayari kwa mechi zao tano zitakazobakia katika uwanja wa nangwanda

Miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kuingoza ndanda katika mzunguko wa pili wa ligi daraja la kwanza taifa ni pamoja na slumu Minel ambaye mzunguko wa kwanza aliiwezesha timu hiyo kushika nafasi ya tano baada ya kuifungia magoli muhimu katika mechi zake kadha

Ndanda inaondoka Mtwara huku Mashabiki wake waliokuwa wengi wakiwa wamepoteza imani ya timu hiyo kutinga ligi kuu kutokana na nafsi iliyopo na msimamo wa kundi lake

YANGA KURUDIANA NA WASAUZI JUMATANO MWANZA

 

Timu ya Young Africans Sports Club kesho alfajiri inatarajiwa kusafiri kuelekea jijini Mwanza ambapo siku ya jumatano itacheza mchezo wa kirafiki wa marudiano dhidi ya timu ya Black leopard kutoka nchini Afrika Kusini katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Mchezo huo wa jumatano utakua ni fursa kwa wakazi, wapenzi wa soka wa kanda ya ziwa kuweza kuiona timu yao kwani tangu irejee nchini kutoka Uturuki imecheza mchezo mmoja tu wa kirafiki katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, hivyo ni fursa nzuri kwa wapenzi wa soka kanda ziwa kuiona timu yao.

Katika mchezo wa kwanza Young Africans iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Black leopard huku mabao ya Yanga yakifungwa na Jerson Tegete mabao mawili na Frank Domayo akifunga bao moja na pia kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.

Kocha Mkuu Ernest aliomba kupata michezo miwili ya kirafiki kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa wikii hii katika viwanja tofauti, Yanga ikianza na timu ya Prisons siku ya jumapili.

Aidha Black Leopard ambayo iko nchini Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu nchini Afrika kusini PSL imesifia mchezo wa juzi dhidi ya Yanga na kusema ulikuwa mchezo mzuri na wakuvutia japokuwa walifungwa, lakini watajitahid kupata ushindi katika mchezo wao wa marudiano siku ya jumamosi.

Young Africans ambayo itatumia mchezo huo kama maandalizi yake ya mwisho, itaondoka kesho alfajiri na msafara wa watu 37, wachezaji 27, benchi la ufundi 7 na viongozi 3. 

Timu itarejea Dar es salaam siku ya alhamis jion tayari kabisa kwa kujiandaa na mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili wa ligi Kuu ya Vodacpm dhidi ya timu ya Prisons ya Mbeya.

Kuhusu viingilo vya mchezo huo ni vitakua ni Jukwaa Kuu Tshs 10,000/=,  na mzunguko Tshs 3,500/=(source: http://www.youngafricans.co.tz)

KIIZA TAYARI KUREJEA UWANJANI

hamisi kiiza

Na Idrisa Bandali
KIPA wa tatu wa Yanga SC, Yussuf Abdul na mshambuliaji Mganda, Hamisi Kiiza ‘Diego’ waliokuwa wanasumbuliwa na Malaria, wamepona na leo wamefanya mazoezi na wenzao kwenye Uwanja wa Mabatini, Kijitonyama, Dar es Salaam.
Wawili hao walikosa mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya Black Leopard ya Afrika Kusini juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambao timu yao ilishinda mabao 3-2.
Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizguto ameiambia SWIRARTY BLOG leo kwamba, timu imeendelea na mazoezi leo na wachezaji wote wameshiriki wakiwemo Abdul na Kiiza.
Alisema kwa sasa Yanga haina majeruhi hata mmoja na inaendelea vema na mazoezi yake kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu hya Vodacom Tanzania Bara unaoanza mwishoni mwa wiki.
Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati, katika kujiandaa na mzunguko huo wa pili wa Ligi Kuu, waliweka kambi ya wiki mbili Jijini Antalya, Uturuki kuanzia Desemba 30 mwaka jana hadi Januari 12 mwaka huu.
Katika kambi hiyo, pamoja na kufanya mazoezi ya nguvu ya ufukweni, uwanjani na gym, Yanga ilipata mechi tatu za kujipima nguvu dhidi ya Ariminia Bielefed ya Daraja la Nne Ujerumani waliyotoka nayo sare ya 1-1, kabla ya kufungwa 2-1 na Denizlispor FC ya Daraja la Kwanza Uturuki na 2-0 na Emmen FC ya Daraja la Kwanza Uholanzi.
Yanga ilimaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, ikiwa inaongoza ligi hiyo kwa pointi zake 29, baada ya kucheza mechi 13, ikifuatiwa na Azam iliyomaliza na pointi zake 24 na mabingwa watetezi, Simba SC waliomaliza na pointi 23. 

PINGAMIZI DHIDI YA WAGOMBEA TFF ZAITWA HARAKA

Malinzi Mgombea Urais TFF



Na Idrisa Bandali

BAADA ya kupitia fomu za waombaji uongozi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Kamati ya Uchaguzi ya shirikisho hilo leo inaanza mchakato wa pingamizi dhidi ya wagombea.

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo amesema kwamba, leo saa 10:00 jioni Kamati ya Uchaguzi itabandika kwenye ubao wa matangazo wa TFF majina ya waombaji ili kutoa fursa kwa kipindi cha pingamizi.

Wambura amesema mwisho wa kupokea pingamizi dhidi ya waombaji uongozi ni Januari 26, mwajka huu saa 10:00 jioni.

Jumla ya watu 50 kati ya 52 waliochukua fomu kuomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa TFF utakaofanyika Februari 24, mwaka huu wamerejesha fomu hizo.

Waombaji ambao hawakurejesha fomu ni Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ aliyekuwa akiomba ujumbe wa Kamati ya Utendaji kuwakilisha mikoa ya Morogoro na Pwani, na Shufaa Jumanne aliyekuwa akiomba kuwakilisha Kanda ya Dar es Salaam.

Orodha kamili ya wagombea waliorejesha fomu ni Athumani Nyamlani, Jamal Malinzi, Omari Nkwarulo na Richard Rukambura wanaogombea Urais, nafasi inayoachwa wazi na Leodegar Tenga anayeng’atuka, Michael Wambura, Ramadhani Nassib na Wallace Karia wanaogombea Makamu wa Rais, nafasi inayoachwa wazi na Nyamlani, anayehamia kwenye Urais.

Kwa upande wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Abdallah Musa, Salum Chama na Kaliro Samson (Kagera na Geita), Jumbe Magati, Mugisha Galibona, Richard Rukambura, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).

Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na Omari Walii (Arusha na Manyara), Ahmed Mgoyi na Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama na Stanley Lugenge (Njombe na Ruvuma).

Athuman Kambi, Francis Ndulane na Zafarani Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Hassan Othman Hassanoo, Riziki Majala na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), David Lugenge, Elias Mwanjala, Eliud Mvella na John Kiteve (Iringa na Mbeya), Davis Mosha, Khalid Mohamed na Kusiaga Kiata (Kilimanjaro na Tanga) na Alex Kamuzelya, Juma Pinto, Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih Dauda (Dar es Salaam).

Aidha, waombaji wote sita wa uongozi katika Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) ambayo uchaguzi wake utafanyika Februari 22 mwaka huu wamerejesha fomu.

Kwa upande wa Mwenyekiti waombaji ni Hamad Yahya wa Kagera Sugar na Yusuph Manji wa Yanga wakati Makamu Mwenyekiti aliyeomba ni Said Mohamed wa Azam.

Nafasi mbili za ujumbe wa Bodi ya Ligi Kuu kwa klabu za Daraja la Kwanza zimeombwa na watu watatu. Waombaji hao ni Christopher Peter Lunkonde wa Moro United, Kazimoto Miraji Muzo wa Pamba ya Mwanza na Omari Khatibu Mwindadi.

Friday, January 18, 2013

BRANDTS KUINGOZA YANGA LEO KATIKA MECHI YA 14

http://www.nectoday.nl/userfiles/nectoday/image/Brandts%20Ernie.jpg
Ernie Blandts

Na idrisa bandali

KOCHA Mholanzi, Ernie Brandts leo anatarajiwa kuiongoza Yanga katika mechi ya 14 tangu ajiunge nayo Septemba mwaka huu, akitokea APR ya Rwanda wakati itakapomenyana na Black Leopard ya Afrika Kusini katika mchezo wa kirafiki, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga SC iliyorejea wiki Jumapili kutoka Uturuki kwenye kambi ya wiki mbili mjini Antalya, imekuwa ikijifua katika Uwanja wa Mabatini, Kijitonyama tangu Jumatano kwa ujumla kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Yanga leo itakutana na Black Leopard inayoshika nafasi ya 12 katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini yenye timu 16, iliyowasili jana Dar es Salaam ikiwa na msafara wa watu 42 na kufikia katika hoteli ya White Sands, Mbezi Beach, Dar es Salaam.

Wachezaji wote walifanya mazoezi jana, kasoro kipa wa tatu, Yussuf Abdul na mshambuliaji Hamisi Kiiza 'Diego' wanaosumbuliwa na Malaria.

Katika mechi 13 ambazo Brandts ameiongoza Yanga hadi sasa tangu arithi mikoba ya Mbelgiji, Tom Saintfiet, ameshinda saba, kafungwa nne na kutoka sare mbili.

Kati ya hizo, mechi tisa ni za Ligi Kuu, ambazo amefungwa moja tu dhidi ya Kagera Sugar mjini Bukoba, wakati nyingine dhidi ya watani wa jadi, Simba SC alitoa sare ya 1-1 na saba ameshinda dhidi ya Toto African 3-1, Ruvu Shooting 3-2, Polisi Moro 3-0, JKT Oljoro 1-0, JKT Mgambo 3-0, Azam FC 2-0 na Coastal Union 2-0.

Nyingine zote za kirafiki kama ya leo, Yanga walifungwa 1-0 na Tusker Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya kwenda Uturuki, ambako walianza kwa sare ya 1-1 Ariminia Bielefed ya Daraja la Nne Ujerumani, kabla ya kufungwa 2-1 na Denizlispor FC ya Daraja la Kwanza Uturuki na 2-0 na Emmen FC ya Daraja la Kwanza Uholanzi.

REKODI YA ERNIE BRANDTS YANGA

Yanga 1-1 Simba SC            (Ligi Kuu)

Yanga 0-1 Kagera Sugar    (Ligi Kuu)

Yanga 3-1 Toto African      (Ligi Kuu)

Yanga 3-2 Ruvu Shooting  (Ligi Kuu)

Yanga 3-0 Polisi Moro       (Ligi Kuu)

Yanga 1-0 JKT Oljoro          (Ligi Kuu)

Yanga 3-0 JKT Mgambo     (Ligi Kuu)

Yanga 2-0 Azam FC             (Ligi Kuu)

Yanga 2-0 Coastal               (Ligi Kuu)

Yanga 0-1 Tusker                (Kirafiki)

Yanga 1-1 Ariminia Bielefed (Kirafiki)

Yanga SC 1-2 Denizlispor FC (Kirafiki)

Yanga SC 0-2 Emmen FC   (Kirafiki)

Yanga SC Vs Black Leopard (Kirafiki)

ROMA,AFANDE SELE KUPAGAWISHA WANANCHI WA MTWARA LEO

http://api.ning.com/files/-c-NQZ6C0h1Uue8RBdhRum8e0Q1PhqdTIAJhHmQfg8TE2kixVLU*-YNu0eatwW5*XlAWWLTXOlkOltjj0m5TRP*dQhoVZZs5/RomaMkatoliki.jpg?width=640&height=427
roma mkatoliki



 Na idrisa bandali
Msanii Mkongwe wa kizazi kipya Nchini Afande Sele leo atawaongoza wasanii wenzake watatu katika kuwapa burudani wananchi wa Mtwara katika viwanja vya mashujaa Mkoani Mtwara

Afande sele ama Mfalme wa Rhymes atatumbuiza wananchi wa Mtwara baada ya kuombwa na chama cha wananchi CUF ambao leo wanafanya Mkutano Mkubwa katika viwanja hivyo

wasanii wengine ambao wanatarajia kuwepo katika viwanja hivyo ni pamoja na Roma Mkatoliki,kundambanda na kalapina

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjr3CploW5YkegdewmzKb_Vpqvc7QvObd8yHaeMak-wGsWbaZLQ2fCImHTwMo6XA9Pm20IZ7BJxBjgWB4j7paC7xTfWiYBtyKkAh1CjdfTH4Kzx58jE8ky0bM0LEsorppssNtGY8dIZ9h-W/s1600/afande-sele.jpg
afandesele
ujaji wa wasanii hao inasemekana kutachangia harakati za wanamtwara katika kudai haki zao za msingi kuhusu gesi






Tuesday, January 15, 2013

SUNZU AUZWA READING KWA BILLION 7 - AENDA KUFANYA VIPIMO VYA AFYA


Stopilla Sunzu

Sentahafu wa Zambia Stopilla Sunzu amechukua likizo fupi kutoka kwenye kambi ya timu ya taifa kwa ajili ya michuano ya AFCON 2013 ili apate nafasi ya kwenda nchini England kwenda kufanya vipimo vya afya kwa ajili ya kujiunga na klabu hiyo.


Sunzu ambaye anachezea klabu ya TP Mazembe ya DRC ambayo imeandika kwenye mtandao wake kwamba ada ya uhamisho ya $4.8million imeshakubaliwa na kilichobakia ni mchezaji kukamilisha vipimo vya afya. 

Mfungaji huyo wa penati ya ushindi ya Zambia dhidi ya Ivory Coast katika AFCON 2012, anatarajia kurudi Afrika ya kusini January 19, siku mbili kabla ya mabingwa watetezi kuchuana na Ethiopia katika mechi ya ufunguzi.

NDANDA YASHINDWA KUONDOKA

Timu ya soka ya Ndanda iliyokuwa iondoke leo kuelekea dar es salaam kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya ligi daraja la kwanza Tanzania bara imeshindwa kuondoka hii leo

Akizngumza na Swiraty Blog Mwalimu msaidizi wa Timu hiyo Masoud maarufu kama morinyo amesema kuwa wameshindwa kuondoka leo na hawajuwi wataondka lini kutokana na kushindwa kupata taarifa rasmi toka kwa viongozi wa timu hiyo

"unajua sisi tulitakiwa kuondoka leo kwa mujibu wa kauli za viongozi hapo wali kwenda dar es salaam kwa ajii ya kambi kabla ya kucheza mechi zetu mbili za kwanza kule dar , sasa sijaua kilichosababisha tushindwe kuondoka leo" alisema masoud

Swiraty blog ilifamya jitihada za kumtafuta Moja kati ya wahisani wa timu hiyo MAMU mmiliki wa kiwanda cha maji ndanda ambapo alidai kuwa yeye yuko tayari hata sasa hivi timu kuondoka kwenda dar esa salaam lakini mtu wa mwisho kutoa kauli ni mwenyekiti wa Chama cha soka Mkoa Athumani Kambi

Kwa upande wake Mwenyekiti huyo wa chama cha soka mkoa wa Mtwara MTWAREFA Athumani Kambi hakuwea kuaptikana kuzungumzia sakata hilo la kushindwa kuondoka kwa timu hiyo ambayo ndio mwakilishi pekee wa mkoa wa Mtwara katika ligi daraja la kwanza

Monday, January 14, 2013

TFF YAIPONGEZA AZAM KWA KUTWAA KOMBE LA MAPINDUZI

azam fc na kombe lao la mapinduzi
  Na Idrisa bandali
 

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeipongeza uongozi wa klabu ya Azam kwa timu yao kufanikiwa kutwaa Kombe la Mapinduzi mwaka huu.

Taarifa ya TFF, imesema kwamba Azam kufanikiwa kutetea ubingwa huo inaonyesha jinsi klabu hiyo ilivyojipanga kabla ya kuingia katika mashindano hayo ambapo ilicheza fainali dhidi ya Tusker FC ya Kenya.

“Pia ushindi huo utakuwa changamoto kwa timu nyingine za Tanzania Bara zitakazopata fursa ya kushiriki michuano hiyo ya Kombe la Mapinduzi mwakani. Michuano hiyo iko kwenye Kalenda ya Matukio ya TFF,”imesema taarifa hiyo.

Azam FC Jumamosi usiku walitetea Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar baada ya kuifunga Tusker FC ya Kenya mabao 2-1.

Kwa ushindi huo, Azam walizawadiwa Sh. Milioni 10, wakati washindi wa pili Tusker wamepata Sh. Milioni 5.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Ramadhan Rajab Ibada ‘Kibo’ aliyesaidiwa na Mwanahija Makame Mfumo na Mgaza Kindundi, hadi mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao.

Azam ndio walioshambulia zaidi katika kipindi hicho, lakini hawakuwa na bahati ya kufunga bao japo moja. Gaudence Mwaikimba alipewa pasi nzuri na Brian Umony dakika ya 44, lakini shuti lake kali lilidakwa na kipa Samuel Odhiambo.

Kipindi cha pili, Tusker walirudi na moto mkali na kuanza kusukuma mashambulizi mfululizo langoni mwa Azam.

Hiyo iliwasaidia mabingwa hao wa Kenya kupata bao dakika ya 60, lililofungwa na Jesse Were aliyeunganisha kwa shuti kali la kimo cha mbuzi pasi ya Robert Omunok.

Hata hivyo, bao hilo halikudumu sana, kwani Azam FC walisawazisha dakika ya 72 lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na beki Mkenya, Joackins Atudo baada ya beki wa Tusker, Luke Ochieng kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.

Katika dakika mbili za nyongeza baada ya kutimu kwa dakika 90 za mchezo huo, alijitokeza binti mwenye umri kati ya 14 na 16 na kukatiza uwanjani akitokea jukwaa la Urusi.

Refa refa Ramadhan Rajab Ibada ‘Kibo’ alijaribu kumsimamisha, lakini aliendelea kukatiza Uwanja hadi nje ambako alipokewa na askari Polisi na kutolewa nje kabisa ya Uwanja. Mtangazaji wa Uwanja wa Amaan, Farouk Karim aliwatuliza mashabiki akisema binti huyo ametoroka hospitali ya vichaa, Kidongo Chekundu na tayari Polisi wamemkamata na kumrejesha huko.

Hadi dakika 90 zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1 na ndipo zikaongezwa dakika 30.

Gaudence Exavery Mwaikimba aliipatia Azam bao la ushindi dakika ya pili tu tangu kuanza kwa muda wa nyongeza baada ya kuwazidi nguvu na maarifa mabeki wa Tusker.

Aidha, Jesse Were mshambuliaji wa Tusker aliibuka mfungaji bora kwa mabao yake matano na kuzawadiwa Sh. 300,000, akifuatiwa na Joackins Atudo wa Azam aliyefunga mabao matatu sawa na Adeyum Saleh Ahmed wa Miembeni.

Friday, January 11, 2013

YANGA YAPIGWA 2 - 0NA EMMEN FC

yanga
Young Africans imepoteza mchezo wake wa mwisho wa  kirafiki dhidi ya timu ya timu ya Emmen FC ya ligi daraja la kwanza nchini Uholanzi baada ya kufungwa kwa mabo 2-0 katika mchezo uliofanyika katika mji wa Bereke kwenye viwanja vya Arcuda foootball Antalya. 

Young Africans ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na kutengeneza nafasi za kufunga lakini kutokua makini kwa washambuliaji wake Nizar Khalfani, George Banda na Saimon Msuva kuliinyima Yanga kupata bao katika dakika 15 za kwanza,
Dakika ya 23 Saimon Msuva alishindwa kuipatia Yanga bao baada ya kushindwa kumalizia pasi safi nzuri ya Nizar Khalfani ambapo Msuva aliupiga mpira na kuokukolewa na mlinda mlango wa timu ya Emmen FC.
George Banda ambaye leo alianza kama mshambuliaji wa kati akisaidiana na Nizar Khalfani alishindwa pia kuipatia Yanga bao baada ya kushindwa kumalizia mpira uliopigwa na Haruna Niyonzima akitokea upande wa kushoto wa uwanja.
Mlinda mlango wa Yanga Said Mohamed alifanya kazi ya ziada kuokoa mipira miwili ya hatari langoni mwake baada ya washambuliaji wa Emmen kugongeana vizuri na kuwatoka walinzi wa Yanga lakini mashuti yao walikuta yakiishia mikononi mwake. 
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans 0 - 0 Emmen FC.

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko ya kikosi chote ambapo waliingia, Yusuph Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Ladslaus Mbogo, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Godfrey Taita, Omgea Seme, Didier Kavumbagu, Jerson Tegete na David Luhende.
Yanga ilianza tena mchezo kwa utulivu huku ikipanga mbinu za kuweza kupata bao la mapema lakini umakini wa walinzi wa Emmen Fc ulikuwa kikwazo kwa washambuliaji wa Yanga kuweza kuipita ngome hiyo.
Emmen FC waliitawala zaidi sehemu ya kiungo hali iliyopelekea kufanya mashambulizi mengi langoni mwa timu ya Yanga, na katika dakika ya 73 waliweza kujipatia bao la kwanza baada ya mfungaji kumalizia krosi iliyowapita walinzi wa Yanga.

Dakika nne (4) baadae, Emmen FC walijiapati bao la pili ikiwa ni dakika ya 77 baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo wa Emmen FC kumponyoka mlinda mlango Yusuph Abdul na kugonga mwamba wa juu kabla ya mshambuliaji wa Emmen FC haujaukwmishwa wavuni na kuhesabu bao la pili.
Jerson Tegete aliumia dakika ya 79 katika harakati za kfunga na nafasi yake kuchukuliwa na Rehani Kibingu laikini mabadiliko hayo hayakuisadia Yanga kubadilisha matokeo.
Mpaka dakika 90 zinamalizika Young Africans 0 - 2 Emmen FC.
Mara baada ya mchezo kocha mkuu Ernest Brandts alisema amesikitishwa na matokeo hayo, timu yangu ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na kuwabana vizuri wapinzani wetu lakini kipindi cha pili umakini ulikosekana hali iliyopelekea kufungwa mabao mawili ya haraka haraka.
Makosa yaliyojitokeza katika kipindi cha pili tumeyaona kwa pamoja na benchi zima la ufundi hivyo tutayafanyia kazi yasijitokeze tena katika michezo itakayofuata alisema 'Brandts' .
Yanga kesho itafanya mazoezi ya mwisho asubuhi kabla ya kuanza kujiandaa na safari ya nchini Tanzania siku ya jumapili mchana ambapo itarajiwa kufika Dar es salaam majira ya saa 10 kasoro ikiwa ni siku ya jumatatu alfajiri.
Kikosi kilichoanza kipindi cha kwanza: Said Mohamed, Juma Abdul, Stephano Mwasika,  Nadir Haroub 'Cannavaro', Shadrack Nsajigwa, Nurdin Bakari, Saimon Msuva, Frank Domayo, Geroge Banda, Nizar Khalfani,  Haruna Niyonzima
Kikosi cha kipindi cha pili: Yusuph Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Ladislaus Mbogo, Kelvin Yondani, Athuman Idd 'Chuji, Godfrey Taita, Omega Seme, Didier Kavumbagu, Jerson Tegete/Rehani Kibingu, David Luhende

STARS YAPIGWA 2 - 1 NA ETHIOPIA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhD74n0ABawn2qwNapOpQCWwOG9F1o5SA8I5dmiVvSFcNDfRnusL7xh86USICzI-NhI8QY3UArBWd-UouKYsGlI_Kb2fwjmiLULSBlKPIE_W0a9Dgay14_bBzTXRINNEAehb9SU4FtnKTXg/s1600/TAIFA+STARS.jpg
Taifa Stars

 
Na Boniface Wambura, Addis Ababa

TIMU ya soka ya ya taifa ya Tanzania, imepoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ethiopia uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Addis Ababa hapa mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Mechi hiyo iliyochezeshwa na Bamlak Tesema wa Ethiopia ilikuwa ya kusisimua, hasa kutokana na timu zote kucheza kwa kasi kwa muda wote. Wenyeji Ethiopia ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 13 lililofungwa na Fuad Ibrahim akiwa wastani wa hatua sita kutoka kwa mlinda mlango Juma Kaseja wa Taifa Stars.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kama kilivyokuwa cha kwanza, huku Ethiopia wakiwa wamefanya mabadiliko kwa wachezaji watano. Tanzania ilifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 50 likifungwa na Mbwana Samata baada ya kumzidi maarifa beki mmoja wa Ethiopia.

Bao la ushindi kwa Ethiopia lilifungwa kwa kichwa dakika ya 69 na mshambuliaji Shemelis Bekele aliyeingia kipindi cha pili akiunganisha mpira wa krosi uliopigwa na winga Yossuf Sallah kutoka upande wa kushoto.

Taifa Stars inarejea nyumbani kesho (Jumamosi, Januari 12 mwaka huu) ambapo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7 kamili mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines.

Taifa Stars: Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Issa Rashid, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Amri Kiemba, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, Thomas Ulimwengu/Khamis Mcha, mwinyi Kazimoto na Mbwana Samata.

TUSKER NA AZAM FAINALI YA MAPINDUZI LEO

BINGWA wa 11 wa Kombe la Mapinduzi, anatarajiwa kupatikana leo kwenye Uwanja wa Amaan, visiwani hapa wakati Tusker FC ya Kenya itakapomenyana na Azam FC ya Dar es Salaam.

Azam FC ambao ndio mabingwa watetezi wa michuano hii, waliingia fainali baada ya kuwatoa Simba kwa penalti 5-4, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 120, wakati Tusker dakika 90 ziliwatosha kuwang’oa Miembeni ya hapa kwa kuwachapa 2-0.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kutokana na ubora wa soka wa timu zote katika mashindano haya tangu yanaanza Januari 2, Tusker wakitokea A lililokuwa na timu kali kama Simba na Jamhuri, Azam kundi B lililokuwa na timu kali pia za Miembeni, Mtibwa Sugar na Coastal Union.

Nahodha wa Tusker, Joseph Shikokoti amerudia kusema kwamba Azam hawatawazuia kutwaa Kombe leo.


“Tutawafunga Azam, hawawezi kutuzuia kutwaa hili Kombe, tumewaona wanavyocheza na tunakiri ni timu nzuri, lakini tutawafunga tu,”alisema beki huyo wa zamani wa Yanga alipozungumza na SWIRATY BLOG jana.   

Kwa upande wake, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Muingereza Kali Ongala amesema kwamba wana matumaini ya kubeba Kombe la Mapinduzi leo, ingawa anakiri utakuwa mtihani mzito kwa sababu wapinzani wao, Tusker FC ya Kenya ni timu nzuri.

Akizungumza na SWIRATY BLOG jana, Kali alisema kwamba Wakenya wanawazidi Watanzania mambo mengi sana kisoka, lakini kwa hali yoyote Azam itapambana kubakisha taji nyumbani.

“Itakuwa mechi ngumu, kama ulivyoiona Tusker ni timu nzuri kwa kweli, imekamilika kila idara, lakini sisi pia tuna timu nzuri na tutapigana kufa na kupona,”alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga SC.

Pamoja na hayo, Kali ameomba wapenzi wa soka Zanzibar kujitokeza kwa wingi leo uwanjani kuishangilia Azam FC kwa sababu ni timu ya nyumbani, ili iweze kubakiza taji hilo.

“Sisi ni timu ya Tanzania, na Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, hivyo tunaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kutushangilia ili tuweze kubakiza taji hapa nyumbani,”alisema.

Azam wanatumia mfumo wa kushambulia moja kwa moja mipira mirefu na viungo wake karibu wote wanakuwa na jukumu la kukaba zaidi ya viungo wa pembeni ambao hushambulia moja kwa moja.

Tusker wao wanapiga mipira mirefu na ni hatari sana kwa mipira ya kutokea pembezoni mwa Uwanja.

Timu zote zina safu imara za ulinzi na kiungo na mabeki wake wana desturi ya kupanda kusaidia mashambulizi wakati wa mipira ya kona kwenye lango la wapinzani.

Safu ya ushambuliaji ya Azam leo itamtegemea Mganda Brian Umony kwani hakuna uhakika wa Gaudence Mwaikimba kuanzishwa kutokana na kuonekana kupoteza nafasi nyingi za kufunga katika mashindano haya, ambayo hadi sasa amefunga bao moja tu.

Tusker watakuwa na kinara wa mabao wa mashindano haya, Jesse Were ambaye hadi sasa amefunga mara nne.

Kwa ujumla, kikosi cha Azam leo kinatarajiwa kuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Samir Hajji Nuhu, David Mwantika, Joackins Atudo, Kipre Balou, Uhuru Suleiman, Abdulhalim Humud, Brian Umony, Humphrey Mieno na Uhuru Suleiman.

Tusker FC; Samuel Odhiambo, Luke Ochieng, Bright Jeremiah, Mark Odhiambo, Joseph Shikokoti, Frederick Onyango, Justine Monga, Khalid Aucho, Jesse Were, Ismail Dunga na Robert Omonok.

Wednesday, January 9, 2013

MTWARA KIDS YAJIANDAA KWA ZIARA

Timu ya Soka ya Vijana ya Mtwara Kids iko katika maandalizi makali kwa ziara yao ya kisoka katika mikoa ya dar es salaam na Arusha

Kocha Mkuu wa Timu hiyo dominick Prospa amesema vijana wake wako mazoezini kwa ajili ya maandalizi hayo ambayo wanatarajia kufanay ziara katika mikoa hiyo siku chache zijazo

Prospa amesema kuna baadhi ya wachezaji ambaon wamekwisha wasilin mazoezini na wengine bado hivyo amesisitiza wachezaji waliobaki kuwahi mazoezini ili kuweza kwenda sabamba na program zilizopo

Mtwara kids ni tim u ya vijana iliyopo Mkoani Mtwara ambayo imejijengea umaarufu mubwa kutokana na aina ya uchezaji wake sambamba na kuchukua vikombe mmvbalimbali vikiwemo vya copacocacola,Jimbo Cup na vinginecyo..

TEGETE ON FIRE UTUTRUKI

Tegete kushoto akiwa na Kiiza

YANGA SC imefungwa mabao 2-1 jioni hii na Denizlispor FC ya Denizli, nchini Uturuki katika mchezo wake wa pili wa kujipima nguvu katika ziara yake ya Uturuki, bao la kufutia machozi likifungwa na Jerry Tegete.

Pamoja na kufungwa na timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, iitwayo Bank Asya 1. Lig, ambayo msimu uliopita ilimaliza katika nafasi ya 10, Yanga ilicheza soka ya kuvutia.

Denizlispor Football iliyoanzishwa mwaka 1966, inatumia Uwanja wenye kuingiza mashabiki 19,500 wa Denzili Ataturk na mafanikio yake makubwa hivi karibuni ilikuwa mwaka 2002 waliposhika nafasi ya tano katika Ligi Kuu ya nchini humo na kufuzu kwenye mchujo wa Kombe la UEFA.

Mwaka huo, ilifanya maajabu kwa kuzifunga timu zenye majina Ulaya kama FC Lorient, Sparta Prague na Olympique Lyonnais, kabla ya kufungwa katika Raundi ya Nne na FC Porto ya Ureno, ambao walitwaa ubingwa wa michuano hiyo mwishowe.

Katika mchezo wake wa kwanza wa kujipima nguvu, Yanga ilitoka 1-1 na DSC Arminia Bielefeld ya Ujerumani, bao la timu hiyo ya Jangwani likifungwa na Tegete.

Kikosi cha Yanga leo kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdu, Kabange Twite, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Athumani Iddi ‘Chuji’, Haruna Niyonzima, Nurdin Bakari, Jerry Tegete/Didier Kavumbangu, Said Bahanuzi/Hamisi Kiiza na Simon Msuva.

MAISHA YA MTUKUTU CHUJI UMANGANI

Kiungo wa Yanga, Athumani Iddi ‘Chuji’ akisalimiana na Mturuki mmoja aliyezimia soka yake, katika hoteli ya Fame Residence Lara & Spa mjini Antalya. Yanga imeweka kambi huko tangu wiki iliyopita na inafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Fame Residence.

Kiungo wa Yanga, Athumani Iddi ‘Chuji’ akiwa na kiungo mwenzake wa timu hiyo, Haruna Niyonzima kwenye Uwanja wa Fame Residence.
Kiungo wa Yanga, Athumani Iddi ‘Chuji’ akipiga gumzo na kipa wa timu hiyo, Said Mohamed katika ufukwe wa hoteli ya Fame Residence Lara & Spa mjini Antalya.  
Kiungo wa Yanga, Athumani Iddi ‘Chuji’ (katikati) akiwa na wachezaji wenzake, kiungo Nurdin Bakari kulia na beki Godfrey Taita kushoto katika ufukwe wa hoteli ya Fame Residence Lara & Spa mjini Antalya.  
Kiungo wa Yanga, Athumani Iddi ‘Chuji’ akiwa na beki Godfrey Taita kwenye Uwanja wa Fame Residence.
Kiungo wa Yanga, Athumani Iddi ‘Chuji’ akiwa na beki Kevin yonda wakipata mlo wa asubuhi katika hoteli ya Fame Residence Lara & Spa mjini Antalya. 
Chuji kwa raha zake
Kiungo wa Yanga, Athumani Iddi ‘Chuji’ akiwa na swahiba wake beki Kevin Yondan, wakipata mlo wa asubuhi katika hoteli ya Fame Residence Lara & Spa mjini Antalya. Yanga imeweka kambi huko tangu wiki iliyopita na inafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Fame Residence.

CHUJI ASEMA DENIZLISPOR LILIKUWA BONGE LA KIPIMO YANGA JANA

Chuji

KIUNGO wa Yanga, Athumani Iddi ‘Chuji’ amesema kwamba Denizlispor FC waliyocheza nayo jana mchezo wa kirafiki kilikuwa kipimo kizuri kwao, kwani timu hiyo ni nzuri zaidi ya ile waliyocheza nayo awali, DSC Arminia Bielefeld ya Ujerumani.

Akizungumza naSWIRATY BLOG kutoka Uturuki jana, Chuji alisema kwamba mechi ya jana imewasaidia sana kujua mapungufu na ubora wao kwa kuwa walicheza na timu nzuri iliyowazidi uwezo.

“Hii timu ni nzuri sana, kwa kweli imetupa changamoto nzuri na sisi wenyewe kama wachezaji tumeona hicho kitu,”alisema Chuji.

Yanga SC jana ilifungwa mabao 2-1 na Denizlispor FC ya Denizli, nchini Uturuki katika mchezo wake wa pili wa kujipima nguvu katika ziara yake ya Uturuki, bao la kufutia machozi likifungwa na Jerry Tegete.

Pamoja na kufungwa na timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, iitwayo Bank Asya 1. Lig, ambayo msimu uliopita ilimaliza katika nafasi ya 10, imeelezwa Yanga ilicheza soka ya kuvutia.

Denizlispor Football iliyoanzishwa mwaka 1966, inatumia Uwanja wenye kuingiza mashabiki 19,500 wa Denzili Ataturk na mafanikio yake makubwa hivi karibuni ilikuwa mwaka 2002 waliposhika nafasi ya tano katika Ligi Kuu ya nchini humo na kufuzu kwenye mchujo wa Kombe la UEFA.

Mwaka huo, ilifanya maajabu kwa kuzifunga timu zenye majina Ulaya kama FC Lorient, Sparta Prague na Olympique Lyonnais, kabla ya kufungwa katika Raundi ya Nne na FC Porto ya Ureno, ambao walitwaa ubingwa wa michuano hiyo mwishowe.

Katika mchezo wake wa kwanza wa kujipima nguvu, Yanga ilitoka 1-1 na DSC Arminia Bielefeld ya Ujerumani, bao la timu hiyo ya Jangwani likifungwa na Tegete.

Kikosi cha Yanga jana kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdu, Kabange Twite, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Athumani Iddi ‘Chuji’, Haruna Niyonzima, Nurdin Bakari, Jerry Tegete/Didier Kavumbangu, Said Bahanuzi/Hamisi Kiiza na Simon Msuva.

AZAM vs SIMBA LEO KOMBE LA MAPINDUZI

simba

CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA), kimefanya marekebisho ya ratiba ya michuano ya Kombe la Mapinduzi na sasa Simba SC itamenyana na Azam FC katika Nusu Fainali ya kwanza leo kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Awali, leo ilikuwa Tusker FC icheze na Miembeni kwenye Uwanja huo, lakini sasa timu hizo zitamenyana kesho katika Nusu Fainali ya pili.

Mchezo huo utakuwa ni marudio ya Nusu Fainali ya mwaka jana, ambayo Azam FC waliitoa Simba SC kwa kuichapa mabao 2-1.

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Muingereza Kalimangonga Sam Daniel Ongala, maarufu kama Kali, amesema kwamba wamefurahia kukutana na Simba SC katika Nusu Fainali kuliko Tusker ya Kenya, kwa sababu hiyo itakuwa njia ya mkato kwao kuingia Fainali.

Kuelekea mchezo wa kesho, Kocha wa Miembeni, Salum Bausi amesema hawahofii Tusker na watawaonyesha kwamba mpira ni zaidi yua nguvu 

Nahodha wa Tusker, Joseph Shikokoti amesema kwamba haoni timu ya kuwazuia kutwaa Kombe la Mapinduzi.

Shikokoti aliyewahi kuchezea Yanga alisema kwamba anafahamu Simba na Azam ni wazuri na anajua mojawapo watakutana nayo fainali, lakini amesistiza hakuna kati yao inayoweza kuwazuia wasitwae Kombe.

“Hili Kombe letu, tumeona uwezo wa timu zote, hata Simba na Azam ni wazuri, lakini tutawafunga wote tukikutana nao, hawana uwezo wa kutuzuia,”alisema Shikokoti.

azam

Sunday, January 6, 2013

Q CHIEF; CHIFU KIUMBE KWA HII VIDEO ANGEJIACHIA TU AKAWASAIDIA AKINA SHETTA

 


Q chief ambae ameshaachia ngoma kadhaa tangu alivyorudi kwenye game chini ya Chief Kiumbe ambae alikua akijitolea kumsaidia katika kutengenza na kulipia video zake, alifikia hatua ya kuzungumza juu ya biff lililopo kati yake na producer mkubwa Tanzania Adam Juma, kwa kudai kuacha kutengeneza video yake na badala yake kutengeneza video ya Shetta kwa pesa za video yake aliyokuwa kasaidiwa na Chief Kiumbe na kuonyesha hisia zake jinsi ilivyomuuma 

lakini Kiumbe alisema yuko tayari kumlipia video nyingine akairekodie Nairobi, lakini leo hii Chilla amesema 

"kwa miaka minne nimekua nikiwapigia magoti, nikitu kizuri amekuja amejitolea lakini nahisi kama kuna hasada katikati, so hata Chief pia naona kwenye hii video angejiacha tu akawasaidia akina Shetta na wengine. kama kuna mtanzania yuko tayari kuwekeza kwenye hii video na carrier ya Q chief na katika biashara kwa nia ya kufika pale 1. asahau yaliyopita 2. awe tayari kutoa nafasi 3. asiwe mbahili na mfuko wake, kwasababu when u invest you get more money..............lakini Chief Kiumbe right now is not the source, nimemsubiri sana, kama nilivyosema sitasubiri kusubiri watu, anaeajiriwa ataajiriwa asiekuwa na  ajiri atatoka nje ya ajira, ni muda wa mapinduzi ya fikra potofu, this is it." Chilla

THE MOST CLASSIC COMBINATION KUFANYA SHOW KALI YA KUTAMBULISHA KUNDI

the most classic combination(MC DINO $ KAPOSSA)


Kundi linalofanya vizuri katika mziki wa kizazi kipya mkoani mtwara The Most Classic Combination Chini ya meneja wake Idrisa bandali linatarajia kufanya show kali ya kufungua mwaka 2013 katikati ya mwezi huu

 

Akizungumza na SWIRATY BLOG meneja wa Kundi hilo Idrisa Bandali amesema kuwa lengo la show hiyo ni kutoa shukrani zao za dhati kwa mashabiki wao waliowasapoti mwaka uliopita na kuukaribisha mwaka mpya wa 2013

"mwaka uliopita kwetu ulikuwa sana wa kutoa nyimbo na ni show chache ambazo tumefanya za kualikwa ,sasa mwaka huu katikati ya mwezi huu lazima tuafnye show ambayo tutaiandaa wenyewe na hapo ndipo rasmi tutatambulisha rasmi kundi letu kwa wadau wetu" alisema Bandali

Kundi hilo ambalo linaundwa na waimbaji Mc Dino na Kaposa tayari lieshatoa nyimbo kadhaa ikiwemo AFRIKA MOTO ambayo inafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya radio nchini

Kwa mujibu wa meneja Bandali amesema bado hawajajua wataifanyia wapi show yao lakini wanatarajia kualika msadii mmoja mkubwa ambaye atawasindikiza katika show hiyo

LIGI ZA LALIGA NA SERIA A ZARUDI TENA

wachezaji wa Real Madrid wakiwa mazoezini


Na Idrisa Bandali

BAADA KUWA LIKIZO  Ligi kali za Ulaya, Serie A huko Italy na La Liga huko Spain, zimeanza tena na hapo jana huko Italy, Lazio, ambayo ipo nafasi ya Pili, iliifunga Cagliari 2-0 na kuinyemelea Juventus iliyo kileleni na sasa kuwa Pointi 5 nyuma yao.

Huko Spain, La Liga ilianza tena juzi Ijumaa kwa Real Zaragoza kuchapwa nyumbani na Real Betis Bao 2-1 na kuendelea tena jana huku leo Vinara wake, Barcelona, watakuwa nyumbani kucheza Mechi yao ya kwanza ya Mwaka 2013 na Espanyol hii ikiwa Dabi ya Jiji la Barcelona.

Mabingwa watetezi, Real Madrid, walio nafasi ya 3, pia wapo nyumbani kucheza na Real Sociedad.

Huko Italy, Serie A itaendelea kunguruma leo kwa Mabingwa, ambao pia ni vinara, Juventus, kucheza na Sampdoria pamoja na kuwepo Mechi nyingine za Timu Vigogo kama vile AC Milan, Inter Milan huku Mechi ya mvuto ni kati ya Napoli na AS Roma.

SERIE A

RATIBA/MATOKEO:

Jumamosi Januari 5

Catania 0 Torino 0

Lazio 2 Cagliari 0

Jumapili Januari 6

AC Milan v Siena

Chievo Verona v Atalanta

Juventus v Sampdoria

Parma v Palermo

Udinese v Inter Milan

Napoli v AS Roma

Genoa v Bologna

Fiorentina v Pescara

LA LIGA

RATIBA/MATOKEO:

Ijumaa Januari 4

Real Zaragoza 1 Real Betis 2

Jumamosi Januari 5

Sevilla FC 1 Osasuna 0

Levante 3 Athletic de Bilbao 1

Granada CF 1 Valencia 2

Deportivo La Coruna 1 Malaga CF 0

Jumapili Januari 6

FC Barcelona v RCD Espanyol

Celta de Vigo v Real Valladolid

Real Mallorca v Atletico de Madrid

Real Madrid CF v Real Sociedad

Jumatatu Januari 7

Rayo Vallecano v Getafe CF

KAI AWAASA WACHEZAJI WA NDANDA..

mohamedi kai kulia akiwa na afisa habari wake bandali na mchezaji mwenzake ramandani wakati akiitumikia Ndanda FC


Na Idrisa Bandali

Mchezaji wa Zamani wa Ndanda ambaye kwa sasa amejiunga na Prisons ya mbeya kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania Bara Mohamedi Kai amewatala wachezaji wa Ndanda kujituma ipasavyo ili waweze kipandisha daraja timu hiyo 

Kai ambaye alikuwa nahodha mkuu wa timu hiyo amesema kuwa wana Mtwara wameshindwa kuiona ligi kuu muda mrefu katika ardhi yao baada ya kushuka kwa Timu ya Bandari na hivo amewataka wachezaji waliobakia kutambua kuwa wanakazi kubwa ya kuibeba Mtwara kwa kuhakikisha wanashinda mechi zote saba zilizosalia ili kuwa na nafasi nzuri ya kutinga ligi kuu msimu ujao

Kai ameichezea Ndanda Fc  tangu ligi ya kanda na mpaka ligi daraja la kwanza ambapo alionesha kiwango kizuri kilichowqavutia Prisons ya Mbeya na kumsajili

Timu ya Ndanda kwa sasa iko katika maandalizi ya kucheza ligi daraja la kwanza mzunguko wa pili baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza mwaka jana ambapo Ndanda Fc ilimaliza ikiwa nafasi ya Tano ikiwa na pointi zake 7

SIMBA KUTUPA KARATA YAKE YA MWISHO LEO KOMBE LA MAPINDUZI.KIHWERO AAHIDI KUJIUZURU KAMA HATOSHINDA

http://api.ning.com/files/0bnJKNMhrJ2gW2JFpoEn08Z8xkUF418miS9GjSb*3yFiZ9iKsKGxldggDuFuPrwisfxby9YGM9KI9cmfLoxDUCJHSOLiDrt6/julio.jpg?width=500
Kocha Msaidizi wa Simba Jamhuri Kihwero



Michuano ya kuwania Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar inaendelea tena hii leo kwa Timu ya Soka ya Simba kushuka Dimbani kumenyana na Bandari ya Zanzibar majira ya saa 2;30 usiku

Mchezo huo kwa simba toka kundi A ni wa Mwisho kwao ambapo inahitaji ushindi wa hali na mali ili kuweza kujihakikishia kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ya komvbe la Mapinduzi kwani hadi hivi sasa Simba ina pointi 4 sawa na vinara wa kundi hilo Timu ya Tusker Fc ya Kenya ambao wao wako mbele kwa wastamni wa mambo ya kufunga

Kocha Msaidizi wa Simba SC, Jamhuri Mussa Kihwelo ameahidi kujiuzulu leo iwapo timu hiyo itafungwa na Bandari leo.

Katika mchezo uliopita, Simba SC ilionyesha kuimarika kiuchezaji na kutoa sare dhidi ya timu ngumu, Tusker ya Kenya ya kufungana bao 1-1 kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa.

Kwenye mchezo huo, hadi mapumziko timu hizo zilikuwa zimekwishafungana bao 1-1, Simba wakitangulia kupata bao dakika ya 18 mfungaji Haruna Moshi Shaaban, maarufu kama Boban au Balotelli wa Bongo kabla ya Tusker kusawazisha dakika ya 39, mfungaji Khalid Aucho.

Boban alifunga bao tamu sana kwa ufundi wa hali juu akiwa amedhibitiwa na beki ngongoti wa Tusker, Joseph Shikokoti na kuirukia pasi ya Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kuitumbukiza nyavuni.

Baada ya kufunga bao hilo, Boban aliangukia mkono na kuumia, hivyo hakushangilia bao lake na moja kwa moja alianza kutibiwa na Daktari Cossmas Kapinga wa Simba.

Baada ya bao hilo, Simba iliongeza mashambulizi langoni mwa Tusker na Boban alikaribia kufunga tena dakika ya 30 kama si shuti lake kutoka nje sentimita chache.

Aucho alifunga bao lake akiunganisha krosi ya Jeremiah Bright kutoka upande wa kushoto wa Uwanja.

Baada ya hapo, timu zilianza kushambuliana kwa zamu hadi refa Ramadhani Kibo alipopuliza kipyenga cha kuhitimisha ngwe ya kwanza.

Kipindi cha pili timu zote zilirudi vizuri na kucheza kwa umakini wa hali ya juu, jambo ambalo lilisababisha dakika 90 zimalizike zikiwa zimefungana 1-1.

Katika mchezo wa leo, kikosi cha Simba kinatarajiwa kuwa kile kile kilichotoa sare ya 1-1 na Tusker; William Mweta, Miraj Adam, Paul Ngalema, Shomary Kapombe, Komabil Keita, Jonas Mkude, Haroun Athumani, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi na Ramadhan Chombo ‘Redondo’.