|
Ernie Blandts |
Na idrisa bandali
KOCHA Mholanzi,
Ernie Brandts leo anatarajiwa kuiongoza Yanga katika mechi ya 14 tangu ajiunge
nayo Septemba mwaka huu, akitokea APR ya Rwanda wakati itakapomenyana na Black
Leopard ya Afrika Kusini katika mchezo wa kirafiki, Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Yanga SC
iliyorejea wiki Jumapili kutoka Uturuki kwenye kambi ya wiki mbili mjini Antalya,
imekuwa ikijifua katika Uwanja wa Mabatini, Kijitonyama tangu Jumatano kwa
ujumla kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Yanga leo
itakutana na Black Leopard inayoshika nafasi ya 12 katika Ligi Kuu ya Afrika
Kusini yenye timu 16, iliyowasili jana Dar es Salaam ikiwa na msafara wa watu
42 na kufikia katika hoteli ya White Sands, Mbezi Beach, Dar es Salaam.
Wachezaji
wote walifanya mazoezi jana, kasoro kipa wa tatu, Yussuf Abdul na mshambuliaji Hamisi
Kiiza 'Diego' wanaosumbuliwa na Malaria.
Katika mechi
13 ambazo Brandts ameiongoza Yanga hadi sasa tangu arithi mikoba ya Mbelgiji,
Tom Saintfiet, ameshinda saba, kafungwa nne na kutoka sare mbili.
Kati ya
hizo, mechi tisa ni za Ligi Kuu, ambazo amefungwa moja tu dhidi ya Kagera Sugar
mjini Bukoba, wakati nyingine dhidi ya watani wa jadi, Simba SC alitoa sare ya
1-1 na saba ameshinda dhidi ya Toto African 3-1, Ruvu Shooting 3-2, Polisi Moro 3-0, JKT
Oljoro 1-0, JKT Mgambo 3-0, Azam FC 2-0 na Coastal Union 2-0.
Nyingine zote za kirafiki kama ya leo, Yanga walifungwa 1-0
na Tusker Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya kwenda Uturuki, ambako walianza
kwa sare ya 1-1 Ariminia Bielefed ya Daraja la Nne Ujerumani, kabla ya kufungwa 2-1 na Denizlispor FC ya
Daraja la Kwanza Uturuki na 2-0 na Emmen FC ya Daraja la Kwanza Uholanzi.
REKODI YA
ERNIE BRANDTS YANGA
Yanga 1-1 Simba SC (Ligi
Kuu)
Yanga 0-1 Kagera Sugar (Ligi
Kuu)
Yanga 3-1 Toto African
(Ligi
Kuu)
Yanga 3-2 Ruvu Shooting
(Ligi
Kuu)
Yanga 3-0 Polisi Moro (Ligi
Kuu)
Yanga 1-0 JKT Oljoro (Ligi Kuu)
Yanga 3-0 JKT Mgambo (Ligi
Kuu)
Yanga 2-0 Azam FC (Ligi
Kuu)
Yanga 2-0 Coastal (Ligi
Kuu)
Yanga 0-1 Tusker (Kirafiki)
Yanga 1-1 Ariminia Bielefed (Kirafiki)
Yanga SC 1-2
Denizlispor FC (Kirafiki)
Yanga SC 0-2 Emmen FC (Kirafiki)
Yanga SC Vs
Black Leopard (Kirafiki)