|
simba |
CHAMA cha Soka
Zanzibar (ZFA), kimefanya marekebisho ya ratiba ya michuano ya Kombe la
Mapinduzi na sasa Simba SC itamenyana na Azam FC katika Nusu Fainali ya kwanza
leo kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Awali, leo
ilikuwa Tusker FC icheze na Miembeni kwenye Uwanja huo, lakini sasa timu hizo zitamenyana
kesho katika Nusu Fainali ya pili.
Mchezo huo
utakuwa ni marudio ya Nusu Fainali ya mwaka jana, ambayo Azam FC waliitoa Simba
SC kwa kuichapa mabao 2-1.
Kocha Msaidizi
wa Azam FC, Muingereza Kalimangonga Sam Daniel Ongala, maarufu kama Kali,
amesema kwamba wamefurahia kukutana na Simba SC katika Nusu Fainali kuliko
Tusker ya Kenya, kwa sababu hiyo itakuwa njia ya mkato kwao kuingia Fainali.
Kuelekea mchezo
wa kesho, Kocha wa Miembeni, Salum Bausi amesema hawahofii Tusker na watawaonyesha
kwamba mpira ni zaidi yua nguvu
Nahodha wa
Tusker, Joseph Shikokoti amesema kwamba haoni timu ya kuwazuia kutwaa Kombe la
Mapinduzi.
Shikokoti
aliyewahi kuchezea Yanga alisema kwamba anafahamu Simba na Azam ni wazuri na
anajua mojawapo watakutana nayo fainali, lakini amesistiza hakuna kati yao
inayoweza kuwazuia wasitwae Kombe.
“Hili Kombe
letu, tumeona uwezo wa timu zote, hata Simba na Azam ni wazuri, lakini
tutawafunga wote tukikutana nao, hawana uwezo wa kutuzuia,”alisema Shikokoti.
|
azam |