|
Tegete kushoto akiwa na Kiiza |
YANGA SC
imefungwa mabao 2-1 jioni hii na Denizlispor FC ya Denizli, nchini Uturuki
katika mchezo wake wa pili wa kujipima nguvu katika ziara yake ya Uturuki, bao
la kufutia machozi likifungwa na Jerry Tegete.
Pamoja na
kufungwa na timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, iitwayo Bank Asya 1.
Lig, ambayo msimu uliopita ilimaliza katika nafasi ya 10, Yanga ilicheza soka
ya kuvutia.
Denizlispor
Football iliyoanzishwa mwaka 1966, inatumia Uwanja wenye kuingiza mashabiki
19,500 wa Denzili Ataturk na mafanikio yake makubwa hivi karibuni ilikuwa mwaka
2002 waliposhika nafasi ya tano katika Ligi Kuu ya nchini humo na kufuzu kwenye
mchujo wa Kombe la UEFA.
Mwaka huo,
ilifanya maajabu kwa kuzifunga timu zenye majina Ulaya kama FC Lorient, Sparta
Prague na Olympique Lyonnais, kabla ya kufungwa katika Raundi ya Nne na FC
Porto ya Ureno, ambao walitwaa ubingwa wa michuano hiyo mwishowe.
Katika mchezo
wake wa kwanza wa kujipima nguvu, Yanga ilitoka 1-1 na DSC Arminia Bielefeld ya
Ujerumani, bao la timu hiyo ya Jangwani likifungwa na Tegete.
Kikosi cha
Yanga leo kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdu, Kabange Twite, Kevin Yondan,
Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Athumani Iddi ‘Chuji’, Haruna Niyonzima, Nurdin
Bakari, Jerry Tegete/Didier Kavumbangu, Said Bahanuzi/Hamisi Kiiza na Simon Msuva.