Sunday, January 6, 2013

SIMBA KUTUPA KARATA YAKE YA MWISHO LEO KOMBE LA MAPINDUZI.KIHWERO AAHIDI KUJIUZURU KAMA HATOSHINDA

http://api.ning.com/files/0bnJKNMhrJ2gW2JFpoEn08Z8xkUF418miS9GjSb*3yFiZ9iKsKGxldggDuFuPrwisfxby9YGM9KI9cmfLoxDUCJHSOLiDrt6/julio.jpg?width=500
Kocha Msaidizi wa Simba Jamhuri Kihwero



Michuano ya kuwania Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar inaendelea tena hii leo kwa Timu ya Soka ya Simba kushuka Dimbani kumenyana na Bandari ya Zanzibar majira ya saa 2;30 usiku

Mchezo huo kwa simba toka kundi A ni wa Mwisho kwao ambapo inahitaji ushindi wa hali na mali ili kuweza kujihakikishia kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ya komvbe la Mapinduzi kwani hadi hivi sasa Simba ina pointi 4 sawa na vinara wa kundi hilo Timu ya Tusker Fc ya Kenya ambao wao wako mbele kwa wastamni wa mambo ya kufunga

Kocha Msaidizi wa Simba SC, Jamhuri Mussa Kihwelo ameahidi kujiuzulu leo iwapo timu hiyo itafungwa na Bandari leo.

Katika mchezo uliopita, Simba SC ilionyesha kuimarika kiuchezaji na kutoa sare dhidi ya timu ngumu, Tusker ya Kenya ya kufungana bao 1-1 kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa.

Kwenye mchezo huo, hadi mapumziko timu hizo zilikuwa zimekwishafungana bao 1-1, Simba wakitangulia kupata bao dakika ya 18 mfungaji Haruna Moshi Shaaban, maarufu kama Boban au Balotelli wa Bongo kabla ya Tusker kusawazisha dakika ya 39, mfungaji Khalid Aucho.

Boban alifunga bao tamu sana kwa ufundi wa hali juu akiwa amedhibitiwa na beki ngongoti wa Tusker, Joseph Shikokoti na kuirukia pasi ya Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kuitumbukiza nyavuni.

Baada ya kufunga bao hilo, Boban aliangukia mkono na kuumia, hivyo hakushangilia bao lake na moja kwa moja alianza kutibiwa na Daktari Cossmas Kapinga wa Simba.

Baada ya bao hilo, Simba iliongeza mashambulizi langoni mwa Tusker na Boban alikaribia kufunga tena dakika ya 30 kama si shuti lake kutoka nje sentimita chache.

Aucho alifunga bao lake akiunganisha krosi ya Jeremiah Bright kutoka upande wa kushoto wa Uwanja.

Baada ya hapo, timu zilianza kushambuliana kwa zamu hadi refa Ramadhani Kibo alipopuliza kipyenga cha kuhitimisha ngwe ya kwanza.

Kipindi cha pili timu zote zilirudi vizuri na kucheza kwa umakini wa hali ya juu, jambo ambalo lilisababisha dakika 90 zimalizike zikiwa zimefungana 1-1.

Katika mchezo wa leo, kikosi cha Simba kinatarajiwa kuwa kile kile kilichotoa sare ya 1-1 na Tusker; William Mweta, Miraj Adam, Paul Ngalema, Shomary Kapombe, Komabil Keita, Jonas Mkude, Haroun Athumani, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi na Ramadhan Chombo ‘Redondo’.