yanga |
Young
Africans imepoteza mchezo wake wa mwisho wa kirafiki dhidi ya timu ya
timu ya Emmen FC ya ligi daraja la kwanza nchini Uholanzi baada ya
kufungwa kwa mabo 2-0 katika mchezo uliofanyika katika mji wa Bereke
kwenye viwanja vya Arcuda foootball Antalya.
Young
Africans ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na kutengeneza nafasi za
kufunga lakini kutokua makini kwa washambuliaji wake Nizar Khalfani,
George Banda na Saimon Msuva kuliinyima Yanga kupata bao katika dakika
15 za kwanza,
Dakika
ya 23 Saimon Msuva alishindwa kuipatia Yanga bao baada ya kushindwa
kumalizia pasi safi nzuri ya Nizar Khalfani ambapo Msuva aliupiga mpira
na kuokukolewa na mlinda mlango wa timu ya Emmen FC.
George
Banda ambaye leo alianza kama mshambuliaji wa kati akisaidiana na Nizar
Khalfani alishindwa pia kuipatia Yanga bao baada ya kushindwa kumalizia
mpira uliopigwa na Haruna Niyonzima akitokea upande wa kushoto wa
uwanja.
Mlinda
mlango wa Yanga Said Mohamed alifanya kazi ya ziada kuokoa mipira
miwili ya hatari langoni mwake baada ya washambuliaji wa Emmen
kugongeana vizuri na kuwatoka walinzi wa Yanga lakini mashuti yao
walikuta yakiishia mikononi mwake.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans 0 - 0 Emmen FC.
Kipindi
cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko ya kikosi chote ambapo
waliingia, Yusuph Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Ladslaus Mbogo,
Kelvin Yondani, Athuman Idd, Godfrey Taita, Omgea Seme, Didier
Kavumbagu, Jerson Tegete na David Luhende.
Yanga
ilianza tena mchezo kwa utulivu huku ikipanga mbinu za kuweza kupata
bao la mapema lakini umakini wa walinzi wa Emmen Fc ulikuwa kikwazo kwa
washambuliaji wa Yanga kuweza kuipita ngome hiyo.
Emmen
FC waliitawala zaidi sehemu ya kiungo hali iliyopelekea kufanya
mashambulizi mengi langoni mwa timu ya Yanga, na katika dakika ya 73
waliweza kujipatia bao la kwanza baada ya mfungaji kumalizia krosi
iliyowapita walinzi wa Yanga.
Dakika
nne (4) baadae, Emmen FC walijiapati bao la pili ikiwa ni dakika ya 77
baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo wa Emmen FC kumponyoka
mlinda mlango Yusuph Abdul na kugonga mwamba wa juu kabla ya
mshambuliaji wa Emmen FC haujaukwmishwa wavuni na kuhesabu bao la pili.
Jerson
Tegete aliumia dakika ya 79 katika harakati za kfunga na nafasi yake
kuchukuliwa na Rehani Kibingu laikini mabadiliko hayo hayakuisadia Yanga
kubadilisha matokeo.
Mpaka dakika 90 zinamalizika Young Africans 0 - 2 Emmen FC.
Mara
baada ya mchezo kocha mkuu Ernest Brandts alisema amesikitishwa na
matokeo hayo, timu yangu ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na kuwabana
vizuri wapinzani wetu lakini kipindi cha pili umakini ulikosekana hali
iliyopelekea kufungwa mabao mawili ya haraka haraka.
Makosa
yaliyojitokeza katika kipindi cha pili tumeyaona kwa pamoja na benchi
zima la ufundi hivyo tutayafanyia kazi yasijitokeze tena katika michezo
itakayofuata alisema 'Brandts' .
Yanga
kesho itafanya mazoezi ya mwisho asubuhi kabla ya kuanza kujiandaa na
safari ya nchini Tanzania siku ya jumapili mchana ambapo itarajiwa
kufika Dar es salaam majira ya saa 10 kasoro ikiwa ni siku ya jumatatu
alfajiri.
Kikosi kilichoanza kipindi cha kwanza:
Said Mohamed, Juma Abdul, Stephano Mwasika, Nadir Haroub 'Cannavaro',
Shadrack Nsajigwa, Nurdin Bakari, Saimon Msuva, Frank Domayo, Geroge
Banda, Nizar Khalfani, Haruna Niyonzima
Kikosi cha kipindi cha pili: Yusuph
Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Ladislaus Mbogo, Kelvin Yondani,
Athuman Idd 'Chuji, Godfrey Taita, Omega Seme, Didier Kavumbagu, Jerson
Tegete/Rehani Kibingu, David Luhende