Timu
ya Young Africans Sports Club kesho alfajiri inatarajiwa kusafiri
kuelekea jijini Mwanza ambapo siku ya jumatano itacheza mchezo wa
kirafiki wa marudiano dhidi ya timu ya Black leopard kutoka nchini
Afrika Kusini katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Mchezo huo wa jumatano
utakua ni fursa kwa wakazi, wapenzi wa soka wa kanda ya ziwa kuweza
kuiona timu yao kwani tangu irejee nchini kutoka Uturuki imecheza mchezo
mmoja tu wa kirafiki katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, hivyo
ni fursa nzuri kwa wapenzi wa soka kanda ziwa kuiona timu yao.
Katika
mchezo wa kwanza Young Africans iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi
ya Black leopard huku mabao ya Yanga yakifungwa na Jerson Tegete mabao
mawili na Frank Domayo akifunga bao moja na pia kuchaguliwa kuwa
mchezaji bora wa mechi hiyo.
Kocha Mkuu Ernest
aliomba kupata michezo miwili ya kirafiki kabla ya kuanza kwa mzunguko
wa pili wa ligi kuu ya Vodacom ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi
mwishoni mwa wikii hii katika viwanja tofauti, Yanga ikianza na timu ya
Prisons siku ya jumapili.
Aidha Black Leopard
ambayo iko nchini Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili
wa ligi kuu nchini Afrika kusini PSL imesifia mchezo wa juzi dhidi ya
Yanga na kusema ulikuwa mchezo mzuri na wakuvutia japokuwa walifungwa,
lakini watajitahid kupata ushindi katika mchezo wao wa marudiano siku ya
jumamosi.
Young
Africans ambayo itatumia mchezo huo kama maandalizi yake ya mwisho,
itaondoka kesho alfajiri na msafara wa watu 37, wachezaji 27, benchi la
ufundi 7 na viongozi 3.
Timu itarejea Dar
es salaam siku ya alhamis jion tayari kabisa kwa kujiandaa na mchezo wa
kwanza wa mzunguko wa pili wa ligi Kuu ya Vodacpm dhidi ya timu ya
Prisons ya Mbeya.
Kuhusu viingilo vya mchezo huo ni vitakua ni Jukwaa Kuu Tshs 10,000/=, na mzunguko Tshs 3,500/=(source: http://www.youngafricans.co.tz)